Jasusi la kitanzania lilivyowatoka wanajeshi Uganda

Pole jamaa! ungekua hapa Mwanza ungekuja nikupe ofa ya samaki wa kuchoma hapa Vila Park ujipoze
SI unajua mitandao inaingiliwa siku hizi utakuta mtu unaweka kitu kwa nia nzuri tuuu wengine wanazani labda unataka kuaribu mambo yao...ngo maana ata ukiangalia sikuianzia mwanzo nia yangu ilikuwa ni kuwaonjesha watu kisha wafuate wakamalizie kwenye kitabu....
 
nata
Hiki kitabu kinaingia lini mtaani? Gazeti la Raia Mwema walikuwa wanarun hii story ila ikafika sehemu wakastop na kusema watu wasubiri kitabu tu
ka sana hicho kitabu bamoja na kila cha kina bwana Tamimu ya kutaka kupindia serikali ya mwalimu miaka ya mwanzoni mwa themanini
 
itabu cha ukachero wa kachero wa Tanzania – 8
Habari Zinazoendana
Share
MAWIO yalipokaribia ndege nao wakaanza kuimba kwa sauti zao nzuri kuashiria kwamba mwanga sasa unataka kuchukua nafasi ya giza. Pamoja na dalili hiyo ya mapambazuko mimi sikutoka nje mpaka nilipoona kumepambazuka kabisa. Nikafunga mlango polepole na kuchungulia nje kama kuna mtu yeyote lakini hakukuwa na mtu bali magari yaliyokuwa yameegeshwa.
Nikatoka na kuliendelea bomba la maji lililokuwa mita chache kutoka katika chumba hicho ambako nilipiga mswaki na kunawa uso. Baadaye nikarudi kwenye chumba hicho kuweka vitu vyangu sawa na kuondoka zangu kuelekea kwenye mlango mkubwa wa kuingilia katika eneo hilo la kanisa.
“Habari za asubuhi” aliniuliza mlinzi wa hapo mlangoni. “Nzuri, naondoka,” nilimjibu haraka kmlangoni kuepusha maswali zaidi.
“Ngoja nikufungulie, naona una haraka sana,” alitamka huku akiuendea mlango na kuufungua bila kunihoji zaidi labda alishajulishwa na wenyewe. “Asante, kwa heri,” nilitamka na kuondoka zangu.
Hatua chache tu kutoka hapo mlangoni kuna barabara inayoitwa Cathedral, nikaifuata barabara hiyo kuelekea upande wa kulia. Nikaipita hospitali iitwayo Mengo na kuendelea mbele hadi nikatokea katika barabara iitwayo Natete. Wakati huo maeneo yote hayo yalikuwa tulivu bila pilikapilika za watu au magari.
Kutoka Natete nikajikuta nipo katika barabara iitwayo Namirembe ambayo niliifuata mpaka kutokea viwanja vya michezo. Kwa kweli mpaka muda huo nilikuwa najiendea tu bila ya kujua wapi naelekea lakini nilijivunia uzoefu wangu katika Jiji la Dar es Salaam. Ukiwa mzoefu wa jiji kama la Nairobi na ukaja Dar e s Salaam kwa mara ya kwanza ukaachwa mahali kama Manzese au Buguruni kwa vyovyote utajua ufuate njia ipi ili ufike katikati ya jiji.
Kwa hiyo na mimi ilikuwa hivyo hivyo, kadiri nilivyoona nikienda mbele idadi fulani ya watu na magari inaongezeka nikajua huko ndiko mjini. Nilikatiza katika uwanja mmoja wa michezo na kutokea mahali panapoitwa ngome kongwe ya Kampala (Kampala Old Fort) na baadaye nikapita kwenye njia ndogo ya miguu nikatokea barabara inayoitwa Martin.
Nikapita kando ya msikiti mmoja mkubwa ambao kando yake kuna hospitali na kujikuta nimetokea barabara ya Mackai ambayo nilipoifuata nikajikuta nimetokea kwenye kituo cha mabasi kilichopo karibu na uwanja maarufu wa mpira wa miguu uitwao Nakivubo.
Hapo katika kituo cha mabasi kulikuwa na mabasi mengi yaliyokuwa yakielekea sehemu mbalimbali. Kilichonishangaza ni kuona kwamba mabaso hayo yalikuwa hayajazi abiria kama yalivyo mabasi ya nyumbani Tanzania.
Aidha nilishangaa kuona wanafunzi wa shule hawakubughudhiwa walipokuwa wakiingia kwenye mabasi hayo, tofauti sana na nyumbani Tanzania ambako wanafunzi huonekana kama maadui wa wenye mabasi, hasa ya daladala.
Nilizubaa hapo kwenye stendi ya mabasi nikiangalia watu wanavyopanda na kuteremka kutoka kwenye mabasi, nikagundua kuna tofauti kubwa sana na utaratibu wa kupanda mabasi wa nyumbani Tanzania. Abiria walipanda mabasi bila kusukumana na wanafunzi walikaa kwenye viti vya mabasi bila bughudha yoyote. Mbali na hilo nikagundua mji wa Kampala ni msafi kuliko Dar es Salaam, hakukuwa na taka zilizotupwa hovyo hovyo wala taka zilizotelekezwa, hali ambayo ilisababisha hata inzi waonekane kwa nadra.
Baada ya kushangaa shangaa hapo stendi kwa karibu saa moja nzima nilimsogelea kijana mmoja ambaye nilimuomba anielekeze mahali penye nyumba ya kulala wageni ya karibu na yenye bei nafuu. Kijana huyo bila ya kinyongo alinijibu kwa kiingereza kizuri kama ilivyo kwa wananchi wengi wa Uganda, kwamba nyumba za kulala wageni zipo daraja tofauti kutegemea uzuri na ubora wake. Alisema zipo nyumba za hali ya chini sana, hali ya kati na hali ya juu ambayo inakaribia hadhi ya hoteli.
“Nielekeze ilipo ya hali ya kati,” nilimwambia haraka. “Unalijua soko la Owino?” “Mimi ni mgeni, sijui,” nilimjibu. “Ukipita ule uwanja wa mpira wa Nakivubo utafuata barabara ya Nakivubo Palace wa mwendo wa kama kilomita mbili halafu tazama upande wa kushoto utaliona soko kubwa liitwalo Owino.” “Enhee! Baada ya kulikuta soko la Owino?” “Baada ya kulikuta soko hilo kwa mbele kidogo utakuta Owino Guest House na mbele ake kuna hoteli ya Kisenyi.” “Asante sana,” nilijibu na kuondoka zangu.
Nilitembea kwa miguu kwa zaidi ya dakika kumi hivi nikajikuta nimefika katika soko la Owino ambalo kwa kweli linafanana sana na soko kuu la mjini Morogoro. Mbele ya soko hilo nikaikuta nyumba ya kulala wageni iitwayo Owino na mbele kidogo nikaiona hoteli ya Kisenyi.
Niliingia katika hoteli ya Kisenyi kuulizia malipo yake kwa siku, nikaona siyo ghali lakini walinitaka nionyeshe pasipoti kabla ya kupangishwa kitu ambacho sikufikiria kabisa, kwa hiyo nikaiacha hoteli hiyo licha ya uzuri wake nikaendelea nyumba ya kulala wageni ya Owino. Nilipofika Owino nilipokelewa kwa shauku na kinadada watatu ambao walikuwa wamekaa nje ya nyumba hiyo wakiwa wanakunywa supu.
“Unakaribishwa” alitamka mmoja wao ambaye ni mnene zaidi kuliko wenzake. “Ahsante” nilijibu na kuingia ndani hadi sehemu ya mapokezi ambako nilimkuta kijana mmoja wa kiume. Kijana huyo alinieleza masharti na malipo ya kupanga chumba, nami nikaridhika kwamba patanifaa. Hata hivyo wasiwasi wangu ulikuwa juu ya wanawake wale watatu mashangingi ambao nilihisi wanaweza kutumiwa kunichunguza au kunimaliza fedha zangu chache nilizokuwa nazo.
“Usalama wake ukoje hapa? Hakuna wizi?” nilimuuliza kijana huyo. “Nyumba hii ina usalama mkubwa, lakini usipende kuingiza wanawake chumbani mwako,” alinieleza kijana huyo kwa kiingiereza murua. Wananchi wengi nchini Uganda wanaongea kiingereza vizuri kwa sababu ni moja ya rasmi za nchi hiyo. Lugha nyingine rasmi ni kinyankole na kiswahili. Hata redio Uganda hutumia lugha zote hizo tatu katika matangazo yake. Wananchi wa Tanzania huzungumza sana Kiswahili na ndiyo lugha rasmi.
Nipoafikiana na kijana huyo nikapanga chumba kwa siku mbili kwa hiyo nikalipia kabisa fedha zote ili kama nikikurupushwa niondoke bila ya deni. Baada ya kulipia chumba hicho nikapewa fomu kujaza majina yangu, uraia, ninakotoka na niendako. Tofauti na kule katika hoteli ya Kisenyi hapa sikudaiwa pasipoti wala kuulizwa.
Nilionyeshwa chumba change namba tisa ambacho kilikuwa na meza ndogo moja, feni ya mezani, kitanda cha futi tatu na nusu chenye chandarua, kiti kimoja na chini kulikuwa na zulia lililoanza kuchakaa. Humo chumbani nilipumzika katika kiti kwa dakika kama kumi hivi na baadaye nikavua nyuo zangu na kuvaa taulo la humo chumbani ambalo halikuwa zuri ingawa lilionekana limefuliwa. Baadaye nikatoka kwenda kwenye vyoo ambavyo vilikuwa nje ya vyumba, nikaoga haraka kisha nikarudi chumbani kwangu na kujilaza kitandani kupata buraha.
Mara nyingi nyumba za kulala wageni zenye vyoo vya nje hutokea sana matukio ya wizi na hasa wakati mpangaji anapotoka kwenda chooni, hata kama umefunga chumba chako kwa funguo. Nililala kwa starehe mpaka karibu saa sita hivi nipo nilipoamka na kutoka nje kwenda kutembetembea maeneo ya jirani ambako nilijikuta nimefika katika uwanja wa mpira wa Nakivubo ambako kulikuwa na watu wengi wakisubiri kuingia ndani ya uwanja. Nilihisi kulikuwa na mechi kubwa jioni bdiyo maana wapenzi wanaingia mapema ndani ya uwanja.
Baadaya kupita hapo Nakivubo nikajikuta nimetokea kwenye mzunguko uliopo karibu na kituo cha mabasi na teksi ambapo nikaufuata mtaa wa Luwum na kulikuta kanisa zuri la katoliki liitwalo “Christ the King”. Ndani ya uwa wa kanisa hilo niliona nyumba nzuri za mapadre na masista. Mbele ya kanisa hilo nikaona Kampala Casino ambayo wakati huo ilikuwa imefungwa vinginevyo ningeingia ndani nicheze kamari.
Kutoka hapo Kampala Casino nikarudi nilikotoka na kuifikia hoteli iitwayo Royal ambayo kwa kwlei inapendeza sana kutokana na mandhari yake nzuri. Nikaingia kwenye hoteli hiyo ili nile chakula cha mchana lakini nilipozisoma bei za vyakula ziliniogopesha, kwa hiyo nikanywa kahawa na keki mbili tu.
Nilipomaliza kufungua kinywa muda huo ambao ni muda wa kula chakula cha mchana niliendelea kukaa kwneye hoteli hiyo ambayo wakati huo ilikuwa ikipiga muziki mzuri aina ya fanki ya polepole. Hata hivyo niliamua kuendelea kukaa mahali hapo zaidi kwa kuwa nilifikiri huenda ningemuona mtu yeyote ninayemfahamu kutoka nyumbani Tanzania.
Wazo langu hili liligonga ukuta baada ya kukaa hapo hotelini kwa saa nzima bila ya kuona sura hata moja ninayoifahamu au japo kuifananisha tu. Nilijiona mjinga, nikaamua kurudi ili kujipumzisha.
Nilipofika nikauchapa usingizi mpaka niliposhtuka jioni sana. Nafikiri uchovu niliokuwa nao ndio ulionifanya nilale foofofoo. Baada ya kuamka nikaenda tena kuoga na baadaye nikala mikate na nyama iliyokuwa kwenye kopo na kisha nikarudi tena kule kwenye hoteliu ya Royal ambako miziki ilinivutia sana. Nilipofika sikuamini macho yangu, watu walikuwa wengi hotelini hapo na palichangamka sana. Taa za rangi zilizokuwa zinawaka kwa kupokezana na miziki mizuri iliyokuwa ikipigwa ilipafanya mahali hapo paonekane pa kuvutia sana.
Nilitafuta nafasi ya kukaa lakini kila meza ilikuwa na watu wanne au sita wakila nyama za kuchoma na kunywa bia na waragi. Hii waragi ni pombe inayopendwa sana huko Kampala ambayo ni sawa sawa na konyagi ya Tanzania. Zunguka zukunka yangu ya kutafuta mahali pa kukaa nikajikuta nimekaa kwenye kiti cha meza ya peke yangu.
Hatua chache au niseme umbali wa kama mita mbili hivi kulikuwa na meza nyingine iliyokuwa na mtu mmoja ambaye macho yangu yaliganda kwake kama macho ya kinyonga anapotaka kumnasa mdudu amle.
Mtu huyo alikuwa mwanamke na alionekana kama vile anamsubiri mtu kwa sababu mara kwa mara alikuwa akiitazama saa yake nzuri iliyokuwa inang’ara ambayo nilihisi ni ya dhahabu. Mwanamke huyo mrefu kidogo mwenye unene wa wanawake wa Kihaya, Kinyakyusa au Kinyamwezi alikuwa amevaa vitenge maridadi ambavyo kwa kweli vilimpendeza sana.
Kichwani alikuwa amejifunga kilemba ambacho kililingana rangi na vitenge alivyovaa. Masikioni, shingoni na vidoleni alijipamba kwa dhahabu tupu. Hakika alionekana ni mwanamke mwenye uwezo kifedha. Wengi walimtazama lakini mimi nilitia for a.
Baada ya pilikapilika za ‘unywaji’ hatimaye nilifanikiwa kukaa pamoja na mwanamke huyo ambaye alijitambulisha kwangu kuwa ni Elizabeth Byarugaba. “Mbona jina la baba yako ni kama la watu wa mkoa wa Kagera nchini Tanzania, umewahi kuishi huko au ni mzaliwa wa huko?”
“Ni kweli kuna kina Byarugaba wengi mkoani Kagera lakini mimi siyo wa huko na wala sijafika huko. Hata hivyo Wahaya wengi wameingiliana na Waganda ndiyo maana desturi zetu, vyakula, maumbile, majina na hata lugha zinafanana kidogo.”
Baada ya maongezi na vinywaji, nilifanikiwa kuondoka hadi nyumbani kwa Elizabeth ambapo tuliendelea na vinywaji sambamba na mazungumzo ya hapa na pale, huku nikibaini viashiria kuwa Elizabeth ni mtumishi wa serikali, hasa kwa sababu eneo analoishi ujenzi wa nyumba zake ni mithili ya watumishi wa umma.
“Ni vyema ukaoge tukalale,” aliniambia. Niliingia maliwatoni na kujitumbukiza kwenye dishi maalumu la kuogea lakini wakati huo nikamsikia Elizabeth akipiga simu.
Itaendelea
Raia Mwema
Read more
Top 10 Tanzania Today Today Breaking News,Tanzania World News 14-October-2016 in Tanzania
Trending Now
KUMBUKUMBU YA MIAKA 17 YA MWALIMU NYERERE
Zinazosomwa Sasa
Makamu wa Rais kuanza ziara Dodoma kesho
1
Diwani, mke washikiliwa kwa kumiliki gobori na bangi
2
RPC aagiza watumia barabara kufuata sheria
3
Are EU trawlers taking too many Mauritanian fish?
4
WAZIRI MKUU APOKEA MSAADA WA SH. MILIONI 27.62
5
BARABARA YA DODOMA-MAYAMAYA KUKAMILIKA NOVEMBA
6
RAIS WA ZANZIBAR DK ALI MOHAMED SHEIN AONGOZA...
7
‘Ingieni darasani mkague kinachofundishwa’
8
‘Mipango ihuishe malengo ya maendeleo endelevu’
9
Mke wa Rais asaidia wazee wasiojiweza
10
Soma Habari kuu leo
Habari za Mikoani
Arusha Dar es Salaam
Dodoma Iringa
Kagera Kigoma
Kilimanjaro Lindi
Manyara Mara
Mbeya Morogoro
Mtwara Mwanza
Pemba Pwani
Rukwa Ruvuma
Shinyanga Singida
Tabora Tanga
Unguja Zanzibar
Used TOYOTA Cars for Sale
NYERERE 1
MWALIMU 2
Arusha 3
Polisi 4
Makamu 5
ZANZIBAR 6
Shule 7
Salaam 8
MSAADA 9
Wanawake 10
1
NEWS ALERT : LORI LA MAFUTA LAWAKA MOTO MBAGALA JIJINI DAR USIKU WA KUAMKIA LEO
2
Lissu: Marehemu Amepiga Kura Katiba Ya Sitta
3
Rais Kikwete Atoa Hotuba Kilele Cha Mbio Za Mwenge Mkoani Tabora
23 friends like this
Tanzaniatoday
18 , 874 likes
Like Page Sign Up
ABOUT TANZANIA TODAY»
Company
Advertise
Feedback
OUR SERVICES»
Company
Advertise
Feedback
TALK TO US»
Email: info@tanzaniatoday.co.tz
Privacy
Sitemap
Help
NEWSLETTER»
1 month ago
Raia Mwema
31
AUG
…………….
KATIKA wiki mbili zilizopita tumechapisha sehemu mbili za uchambuzi wa wa kitabu kipya kinachoitwa MATEKA MPAKANI kilichoandikwa na kachero wa Tanzania, Frown Kageuka (pichani) kumuenzi mwenzake aliyeuawa mpakani mwa Tanzania na Uganda na majasusi wa aliyekuwa Rais wa Uganda, Idi Amin. Leo tunaendelea na sehemu ya tatu ya mfululizo wa uchambuzi wa kitabu hicho.
……………
TULIFIKA Makindye usiku, eneo hilo lilifanana sana na Manzese ya Dar es Salaam. Kwa
 
SI unajua mitandao inaingiliwa siku hizi utakuta mtu unaweka kitu kwa nia nzuri tuuu wengine wanazani labda unataka kuaribu mambo yao...ngo maana ata ukiangalia sikuianzia mwanzo nia yangu ilikuwa ni kuwaonjesha watu kisha wafuate wakamalizie kwenye kitabu....


Kwahiyo Ndugu eddy_mhando mchezo ndio umeishiwa hapo??

Hutaendelea tena kutushushia hii story? Acha hizo bhana mie nakipata wapi hicho kitabu huku Mtwivila? Kama vipi ongea na mhusika akiweke online tukinunue kwa Mpesa siku hizi mambo ya teknohama ndio mpango mzima.

Au tupm tutume mpunga then unatupa link tunakidowload na kwa njia hiyo atauza sana tu na kwa gharama nafuu bila longolongo.

Sema nae basi utupe marejesho.
 
"...Tulifungwa pingu mikononi na kupelekwa kwenye uwanja ambao bila ya kuambiwa nilijua ni sehemu ya kuulia watu kwa kupigwa risasi.
Tulifungwa katika miti iliyokuwa mbele ya magunia mengi ya mchanga ambayo ni maalumu kwa kuzuia risasi isiende mbali.
Koplo Sudi na Sajini Binda walianza kulia kama watoto wadogo. Dakika kama mbili baadae wanajeshi watatu walisimama hatua kama tano mbele yetu na kutulenga kwa bunduki zao.
Wakati nikianza kumuomba Mungu anisamehe makosa yangu ili anipokee huko mbinguni, ghafla ilifika gari aina ya Jeep ikiwa na askari mmoja mwenye cheo cha Kanali na mwingine aliyevaa kaunda suti ya rangi ya kijivu ambaye nilimuhisi afisa wa Idara ya Usalama Taifa ya Iddi Amin inayoitwa SRB".
SAJINI BINDA ATOA SIRI BAADA YA KUTISHWA
"Nani mkubwa kati yenu kwa cheo? Alituuliza ofisa aliyevaa kiraia.
"Nataka niwahakikishieni kitu kimoja, atakayekuwa mkweli hatutamuua ila atakayejifanya mjeuri hapa utakuwa mwisho wake. Fungua hawa wawili na abakie huyu" aliamuru afisa aliyevaa kiraia.
Mimi na Koplo Sudi tulifunguliwa na kurudishwa mahabusu huku Sajini Binda tukimwacha amefungwa.
Baada ya muda tulisikia mlio wa risasi tatu. Punde mlango ulifunguliwa na Polisi Jeshi(MP).
"Nani ndiye Koplo Sudi? Aliuliza MP huyo akiwa mlangoni. Alimchukua na kuondoka naye ndani nikabaki peke yangu. Sasa nikajua siri zimeanza kutoka, kama wamemjua Koplo Sudi bila shaka Sajini Binda amekwisha waeleza mengi.
JASUSI LA TANZANIA LAMZIDI UJANJA KANALI WA KIGANDA
"Dakika kama 20 baadae nikasikia mlio wa risasi, nikajua Koplo Sudi nae ameshauawa.
"Wewe ndiyo Luteni, siyo?" aliniuliza MP aliyekuja kuniita.
"Umetumwa uniite au uniulize swali?" nilimjibu kwa upole.
"Haya unaitwa," alitamka huku akitabasamu.
Niliongozana nae mpaka kwenye uwanja wa mauaji, nikafungwa kamba kwenye mti kama ilivyokuwa awali kisha askari wanne wenye siraha wakajipanga mbele yangu wakisubiri amri ya kunifyatulia risasi.
Mara nikaona ile Jeep ya awali ikisimama mbele yangu kisha wakashuka yule Kanali wa mwanzo na mwenzake na kunisogelea.
Muda wote huo nilikuwa naichunguza ile miti nione kama ina ishara ya damu AU kama wenzangu kweli wameuawa. Hata hivyo sikuona damu yoyote, nikahisi umetumika ujanja wa kututisha lakini kama wametumia njia hiyo basi watakuwa wamesahau kupaka miti hiyo japo rangi inayofanana na damu.
UJASIRI WA JASUSI WA KITANZANIA WAMSHANGAZA KANALI WA KIGANDA
"Wewe ndiye Luteni Nyata? Aliniuliza afisa aliyevaa kiraia.
"Unaniuliza au unaniambia?" nilimjibu bila hofu.
"Wewe tumeambiwa ndiye kiongozi wa wenzako na cheo chako ni Luteni, ni kweli?".
"Kweli" nilimjibu kwa upole huku nikimkazia macho.
"Unaongoza askari wangapi pale Murongo?" aliniuliza afisa huyo aliyevaa kiraia.
"Nawaongoza hao hao wawili waliowaambia mimi ni kiongozi wao".
"Yaani wewe ni kiongozi wa askari wawili?" aliniuliza Kanali.
"Kwani wamewaambia tupo wangapi?" niliwauliza.
"Ah! Yani badala ya kutujibu maswali yetu, unatuuliza sisi maswali?" walinifokea.
"Pale Murongo kuna redio ya mawasiliano?" aliniuliza afisa huyo huku akiandika. "Ipo" nilimjibu nikijua wenzangu wameshawaeleza kila kitu.
"Ipo sehemu gani pale Murongo?" aliniuliza Kanali.
"Kwa kweli ni vigumu kuwaelekeza labda twendeni nikawaoneshe huko huko", nilijibu na kuwafanya wacheke sana.
"Wewe mjanja sana, kweli wewe ni afisa wa jeshi" alinisifu afisa aliyevaa kiraia.

WAFUNGWA VITAMBAA VYEUSI USONI NA KUPELEKWA WASIPOPAJUA
"Jioni ilipofika tulitolewa mahabusu tukiwa tumefungwa vitambaa vyeusi usoni na pingu mikononi tukaingizwa ndani ya lori na safari ya kwenda tusipopafahamu ikaanza.
Baada ya dakika kama 20 au 25 lori lilisimama na tuliteremshwa na kuongozwa hadi kwenye ngazi fulani ambako tuliteremshwa chini hadi kwenye chumba kimoja chenye hewa nzito, harufu mbaya ya mikojo na damu.
Tulifunguliwa vitambaa usoni lakini hatukuweza kuona kitu kutokana na giza la humo ndani.
Tulikaa humo bila ya kufahamu kama ni jioni, usiku au asubuhi.
"Luteni Nyata na Sajini Binda kuja nje haraka." Sauti kali kutoka nje ilituamrisha na wakati huo huo mlango mzito wa chuma ulifunguliwa tukaona mwanga kidogo mbele yetu.
Mimi na Sajini Binda tuliinuka na kuuendea mlango lakini Koplo Sudi alimshika Sajini Binda huku akilia sana akimuomba asimuache".
Muendelezo wa nukuu ya jasusi wa Kitanzania aliyetekwa nyara na wanajeshi wa Uganda wakati ikiongozwa na Idd Amini mara baada ya kuwekewa mtego alipovuka mpaka wa Tanzania na kuingia Uganda akiwa sambamba na askari polisi wawili; Sajini Binda na Koplo Sudi.
 
eddy_mhando!

Hiyo post ya mwisho tuliishapita kitambo bhana, endelea pale kuanzia alipoambiwa akaoge akiwa na mwanamke wa kiganda aliye mpata kwy mgahawa aliyevaa gauni la vitenge

Endelea sasa nadhani dondoo zinatosha
 
eddy_mhando vipi mbona kimya?

Au na wewe unasoma kwanza kisha ndio utuwekee??
Rusha ivoivooo kama salio inshu ni pm namba nikumegee mpunga.
 
wadau hiki kitabu kimeshatoka
 

Attachments

  • 16114498_1541518625860031_9088835666711210726_n.jpg
    16114498_1541518625860031_9088835666711210726_n.jpg
    21.9 KB · Views: 179
Back
Top Bottom