chuwaalbert
JF-Expert Member
- Sep 17, 2010
- 3,598
- 2,115
Naam, NAKULABYE (maana yake Nimekuona). Iko karibu na Kasubi,, makao ya Kabaka (ukiwa kwenye kilima cha Nakulabye, unakuwa unaikabili Ikulu ya Mfalme, ndo maana ya nimekuona Kabaka). Bombo iko karibu na Namirembe (Makao Makuu ya Kanisa Anglikana Uganda). Neno hili lina maanisha HURUMA za MUNGU. Kanisa hili (Cathedral)liko Kusini mwa Chuo Kikuu cha Makelele (kilicho eneo la Wandegeya).....Tulipita eneo lililoandikwa Nakulabye na baadae tukaelekea barabara inayoelekea eneo liitwalo Bombo lakini tulipofika eneo la Namirembe, lori likaanza kupunguza mwendo, nikahisi linakaribia kusimama. Niliruka haraka na kuanza kutembea kufuata barabara ya Balintuma hadi kwenye mzunguko wa barabara iliyooneshwa kwa kibao inaelekea Chuo Kikuu cha Makerere.