Chakorii
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 18,586
- 50,683
Aiseeh...mambo ni mazitoRIWAYA : MPANGO WA CONGO
SEHEMU YA 28
*****
Sundi alirejea nyumbani kwake jua likiwa linaelekea kuwa la utosi.
Alifanya haraka haraka na kuelekea jikoni kupika chakula.
Alipokwisha kupika alihitaji kwenda kufungua na kusafisha majeraha ya Salomoni.
Alivaa mavazi maalumu na kuvaa kitambaa maalumu chenye kamba zilizoenda kushika masikio huku kikiwa kimeziba mdomo na pua.
Sundi alifunua mapazia yaliokuwa yamekizunguka kitanda alicholalia Solomoni Bukaba.
Alikuta Solomoni akiwa ameshazinduka kutoka usingizini.
"Wajisikiaje mpenzi!" aliuliza Sundi huku akimtizama Solomoni usoni.
Macho yao yalipogongana yaliongea Lugha ya upendo wa hali ya juu.
Walipendana kiukweli.
"Naendelea vyema hivi sasa mpenzi wangu" alijibu Solomoni kwa uchovu.
"mmh pole,ngoja nikusafishe ili uendelee kupumzika" alisema Sundi huku akimwanamia Solomoni.
Macho yao yaligongana tena.
Solomoni aliona kitu.
Kitu hicho ndicho alichokiona siku anavamiwa ndani kwake.
Macho!!
Uangaliaji ule ulifanana sawasawa na ule alioangaliwa na mwanamke aliekuwa amevaa kininja.
Macho yalikuwa ni yale yale.
Alikumbuka sawia.
.
Akajikaza bila kuuliza hilo jambo.
Sundi aliendelea kumshugulikia Solomoni.
Alimaliza kumsafisha majeraha kisha akavua mavazi aliokuwa amevaa na kuyatundika mle chumbani kisha akamuomba Solomoni aende sebuleni kwa ajili ya chakula.
Solomoni aliamka kivivu na kwenda sebuleni.
Dakika kadhaa badae walikuwa wanakula chakula kitamu alichopika Sundi huku kila mara Sundi akimsaidia Solomoni kumlisha.
Walikuwa wakitaniana hapa na pale ili mradi kila mtu anaonesha kumjali mwenzie.
Walipomaliza kula walielekea bafuni ambako Sundi alimwogesha Solomoni huku wakitaniana hapa na pale huko bafuni.
Walimaliza kuogeshana wakaelekea chumbani na kujilaza kitandani.
"Mpenzi sijakuuliza kilichokupata jana mana niliona ulikuwa hujiwezi kabisa" alisema Sundi.
"Kwani hujasoma magazeti leo!? Nyumba yangu iliungua moto ila kabla nilivamiwa na watu walionishambulia namna hii kama unavyoona" alijibu Solomoni huku akimtizama Sundi usoni.
Sundi alitazama pembeni.
"hao watu walisema wanataka nini kwako?" aliuliza Sundi.
"Hawakusema wanachotaka" alijibu Solomoni alijibu huku akiwa bado anamtazama usoni.
Sundi alikaa kimya kidogo kisha akamchumu midomoni na kumpa ulimi Solomoni ambae nae aliupokea na wakagandana huku mikono yao ikitalii kwenye miili yao.
"Mmh unaumwa Solo wangu, tuishie hapa" alisema Sundi huku akijinasua Mikononi mwa Solomoni.
Kabla Solomoni hajasema lolote kengele ikalia.
Wakaangaliana.
Kengele ikaendelea kulia kwa fujo.
Sundi akatupa kanga aliokuwa amevaa,harakaharaka akavaa suruali aliokota chini na shati pana jeupe hakujali kuvaa hata chupi akaenda kufungua mlango.
Alipigwa na butwaa!!
"Mbona nyinyi leo mnamabalaa hivi" alisema na mtu aliekuwa getini.
"Mambo yanazidi kuwa mabaya tu" alijibu mtu aliekuwa getini.
"Duh afu niliwambiaje kuingia hapa kabla hatujawasiliana?" alihoji Sundi huku akifungua geti.
Alimfungulia Mwasu.
Mwasu alikuwa anamajeraha mwili mzima ya kuchanika chanika hasa usoni.
Haraka akapelekwa kwenye chumba kilichokuwa na vifaa tiba na kuanza kuhudumiwa.
Huduma ilichukua si zaidi ya saa mbili tayari majeraha yalikuwa yamesafishwa na kushonwa vizuri.
Hakuwa na majeraha makubwa sana hivyo akawa yupo timamu kimwili.
Walitoka kukaa sebuleni.
Walimkuta Solomoni akiwa ametulia akitazama runinga.
Mwasu akamtazama Sundi.
Sundi akatoa ishara ya kuwa asijali.
Wakaenda kukaa wote sebuleni huku Mwasu akipeana salamu na Solomoni.
Kitu ambacho Sundi alikijua na Mwasu hakujua kama Sundi anajua ni kuwa katika mipango yao endapo akitokea mtu hatarishi wa kushugulikiwa basi picha yake husambazwa kwa wote na akishakufa pia taarifa hufika kwa wote.
Hivyo Mwasu alishangaa sana kumkuta Solomoni nyumbani kwa Sundi.
Alimchukulia Sundi kama ni msaliti kati yao.
Akapanda kufanya jambo.
Waliendelea kuangalia runinga huku wakisemezana hili na lile.
Mwasu akaomba kutoka nje kidogo akapunge upepo kwa madai amechoka kukaa na majeraha yalimuuma.
Alikubaliwa huku Sundi akijua ni nini Mwasu anaenda kufanya huko nje.
Hakutaka alilowaza litokee.
Mwasu alipofika nje tu akatoa simu yake harakaharaka akatafuta namba za Elchapo ili apige.
Ni wakati simu yake inaita ndipo akajikuta yupo chini bila kupenda.
Sundi alikuwa amempiga teke la mgongoni.
Ngumi zikapangwa na watu walianza kupigana vita ya hatari.
Solomoni Bukaba akisikia vishindo huko nje,mwanzo alipotezea lakini vishindo viliongezeka.
Nae akatoka.
Alijikuta akishuhudia mpambano safi wa wanawake wanaojua vizuri mchezo wa ngumi.
Sundi alikuwa anacheka ili kumgadhabisha Mwasu.
Kicheko chake kilielea vyema kwenye ngome za masikio ya Solomoni.
Alikumbuka kicheko kile.
Ni cha yule yule mwanamke aliemvamia usiku wa balaa kwake.
Ebana eeh!
"Sundi ni nani na anashirikiana na nani!?" alijiuliza Solomoni.
Ni hadi pale alipoona Mwasu akichomoa kisu kutoka maungoni mwake na kwa ustadi wa hali ya juu akakirusha kumwendea Sundi. Na Sundi nae kwa wepesi wa ajabu akajikunja na kisu kikampita sentimita chache tu.
Solomoni hakujua kama Sundi wake laini laini anaweza kuzichapa kiasi kile.
Ilikuwa ni ajabu ila ndivyo ilikuwa.
Sundi alienda juu kama nyani na aliporudi akaachia teke safi lililoishia shingoni kwa Mwasu na kumsambaratisha chini kama mzigo.
Sundi aliona kumwachia Mwasu ni kujizika zaidi yeye hivyo akachomoa bastola ambayo Solomoni hakujua ilitokea wapi mana Sundi alivaa wakati yeye akiwepo na hakuiona.
Hatari hii.
Kisha akashuhudia Sundi akiachia risasi sita bila huruma ambazo zote zilijaa kifuani kwa Mwasu na kumwacha akiwa hana uhai.
"Why!!" aliuliza Solomoni baada ya kuona Sundi amegeuka na kumnyooshea bastola yeye.
Sundi alitamani apasue kichwa cha Solomoni ila nguvu ya mapendo ilizidi utimamu wa akili.
Akajikuta akishusha silaha chini.
"Tuondoke hapa hakutufai" alisema Sandi huku akiishindilia risasi simu ya Mwasu iliokuwa chini.
Iliwabidi kuondoka eneo lile.
Hekaheka za Komando Zedi Wimba na Jasusi Honda huko Somalia - JamiiForums