Jasusi Honda ndani ya mpango wa Congo

Kudo

JF-Expert Member
Nov 2, 2017
1,809
6,081
RIWAYA: MPANGO WA KONGO

NA, BAHATI MWAMBA

SIMU: 0758573660.


1
MAUAJI

Ilikuwa ni ndani ya majengo ya ubalozi wa Tanzania yalioko pembeni kidogo mwa mji wa mji mkuu wa Congo DRC katikakati ya mji mdogo wa Ivuba.

Katika moja ya meza zilizokuwa ndani ya vyumba vya juu kabisa ndani ya ubalozi huo kulikuwa kuna mtu amesimama kando ya meza hiyo huku kila mara akijaribu kukuna kichwa chake ambacho hakikuwa na unywele hata mmoja.

Mtu yule hakuwa mtulivu wa nafsi,akili na mwili.Bila shaka kwa sababu kadhaa alizozijua yeye na muda wote aliokuwa amesimama kando ya meza ile alikuwa akitazama dirishani,dirisha ambalo wakati huo lilikuwa lipo wazi na halikuwa limefungwa wala kushushwa pazia kubwa na zito ambalo wakati huo lilikuwa limekunjwa kwa namna fulani hivi kisha likashikizwa na kibanio maalumu ambacho kiliacha pazia lile likiwa limejikunja katikati na kujiachia chini.

Ingekuwa siku zingine bwana huyu angeliweza kumuita mfanya usafi na kumkanya juu ya kusahau kufunga dirisha na kushusha pazia,lakini leo hii hilo hakukumbuka kabisa na badala yake akawa amejielekeza kuwaza na kuwazua jambo fulani tata ambalo kamwe hakudhani linafanyika katika nchi ile ya Congo.

Macho yake yalitazama dirishani tena na hapo akashuhudia jengo lingine refu lililokuwa likitazamana na ofisi zake zile,jengo lile lilikuwa ni hoteli kubwa kabisa ndani ya jiji la Kinshasa na mji ule wa Ivuba.

Tofauti na siku zote ambazo huwa analitazama mara kadhaa huku akiwa na kikombe cha kahawa mkononi,lakini leo hii hakuwa na kikombe na hata yale mawazo yake ya kutaka siku moja yeye au mwanae ajenge jengo kama lile nchini Tanzania hayakuwa kabisa akilini mwake.


Akajikuna kichwa na kujiegemeza kwenye meza iliokuwa kando yake kisha akaketi huku sasa mwili wake ukianza kuhisi joto la ajabu ambalo hakujua ni la uoga ama la joto la ahsubuhi ile ya ajabu kwake.

Akiwa bado anatizama pale dirishani mara mlango wa ofisi yake ukafunguliwa bila mfunguaji kubisha hodi.

Akaingia mwanaume mkakamavu mwenye misuli imara na kusimama nyuma yake.

Balozi Ally Sapi akageuka kutoka kule alikokuwa anaangalia na kumgeukia mwanaume yule.

Walitazamana kwa muda kidogo kisha Balozi Sapi akavuta pumzi nyingi na kuzishusha kwa mkupuo.

“Alikuwa sahihi yule bwana mdogo” alisema Balozi huku akimtizama usoni mwanaume yule aliekuwa amesimama mbele yake.

“ina maana ndicho kilichotokea kwako sivyo!”alisaili mwanaume yule.

“Haswaa na tena kinaeza kuniondoa duniani masaa machache yajayo!” alisema Balozi huku akimtizama yule mwanaume na kuuona mshituko wa wazi usoni pake.
Ikawa zamu ya yule mwanaume mkakamavu kujikuna kichwa na kushangaa huku nae kichwa kikijaa moto wa joto ambalo hakujua limetokea wapi ahsubuhi ile.

“aaah ina…” akataka kusema yule mwanume baada ya kuwa anahitaji maelezo zaidi kutoka kwa balozi Ally Sapi,lakini hakumaliza kauli yake tayari balozi Sapi alishaanza kusema.

“Nilipokea ugeni jana jioni wakati natoka hapa ofisini,na kabla sijafika nyumbani yakanipita magari sita kwa kasi na kwenda kusimama mbele kisha gari la mwisho likaanza kupunguza mwendo hali ilionifanya nipunguze na mimi pia na kisha nikaona ishara kutoka kwa dereva wa gari la mwisho kati ya yale magari sita akiniashiria nisimame nami nikatii kwa kusimama pembeni hasa kwa kuhisi inaeza kuwa ni heri tu. Kutoka katika magari yale wakashuka wanaume wanne wakaja karibu na gari langu na bila kusema kwa maneno wakanipa ishara nishuke ndani ya gari,nami nikatii,wakaniongoza hadi kwenye gari moja wapo na humo ndani ya gari sikuamini kabisa nilichokiona aisee” alimalizia kwa kusikitika balozi Sapi.

“kwa ikawa vile tulivyowaza na ulichokiona ni kile kile alichosema marehemu Bulembo!” alisema tena yule mwanaume na hapo ikawa ni zamu ya Balozi Sapi kutumbua macho kwa kutoamini alichokisikia.

“ina maana Bulembo amefariki,lini na wapi!” alihoji Balozi Sapi huku macho yake yakiwa bado yapo yanamtazama mwanaume yule bila kupepesa huku moyo wake ukiruka sarakasi kifuani kwake.
Mwanaume yule akajikuna kichwa na kurudi kumtazama Balozi Sapi huku akijaribu kukwepa kumbukumbu mbaya zilizoanza kumrudia kichwani.

“Nilifika kwake leo mapema kabisa, baada ya kuniandikia ujumbe wakunitaka nifike kwake,nikawahi kufika lakini ikawa kazi bure,nilikutana na maiti yake ikiwa imelala sakafuni na tundu kubwa la risasi shingoni lakini pia nilikuta nyumba yake yote imepekuliwa” alisema mtu yule huku kwa mbali machozi yakizilenga mboni za macho yake,akatumia mgongo wa kiganja chake kujifuta.

“sikijua kama inaeza kuwa namna hii na kwa uharaka mkubwa hivyo” alisema Balozi sapi.

“Hakuna namna lazima tutoe taarifa mapema ofisi kuu mheshimiwa” alisema yule mtu.

Balozi akainama kidogo chini ya meza na alipoinuka alikuwa na mkoba mweusi wa ngozi na bila kutoa kilichomo akamkabidhi yule mwanaume.

“kuuawa kwa Bulembo unamaanisha kuwa kuna msaliti kati yetu hapa ubalozini na pia ni ishara kwetu kuwa tayari tunawindwa tusiifikishe taarifa kunakotakiwa,lakini jitihada za Bulembo zimetuongezea uelewa wa hili jambo,hivyo peleka hivi vielelezo ofisi kuu na hakikisha wanahusika na uzuiaji wa hili jambo,msaliti acha aendelee kuwapo hapa ipo siku kiama kitakuwa juu yake…” Balozi Ally Sapi alisema huku akimkabidhi ule mkoba ambao ulikuwa na nyaraka muhimu sana zilizohusu kile walichokuwa wanakizungumzia pale wakati ule.

“kwa walivyokuteka walitaka uwe miongoni mwao sivyo!” alihoji yule bwana huku akipokea ule mkoba na kuutazama.

“Ndio na nilikataa licha ya kuahidiwa mazuri na bwana yule na kukataa kwangu kunamaanisha kifo kwangu hivi karibuni,hivyo basi hakikisha mpango huo unakoma mara moja,nakuamini Honda” alimalizia kusema Balozi Ally Sapi kisha akageuka na kumwacha Honda akigeuka ili atoke ndani ya ofisi zile za ubalozi wa Tanzania nchini Congo.

****

“kuliaa nyuzi sabiniii…hapo!”

“usijali Mimi ndie Kizibo,hata bila ramani yako tayari wamejaa kwenye jicho la mzungu” alijinadi Kizibo huku mkono wake wa kushoto ukiwa unachezea lenzi ndogo iliokuwa inefungwa juu ya bunduki ya kupiga masafa marefu na mkono wake wa kulia ulikuwa umekamata vyema eneo la kufyatulia risasi ya bunduki ile aina ya K2Lapua magnum rifle,bunduki safi ya kisasa ya kudungulia ukiwa umbali wowote ule. Kizibo hakuwa peke yake alikuwa na mtu mwingine eneo lile ambae yeye akikosa kazi huwa anashika kiona mbali na kisha humsaidia Kizibo kusoma masafa ya windo lao.

“Kojo hawa jamaa wanaongea sana,bila shaka wanajadili hii inshu Mzee” alisema Kizibo huku akijitahidi kufinya jicho lake ili kuhakiisha jicho moja linapata nguvu ya kutazama taswira iliojiweka ndani ya lenzi ya bunduki ile ya kudungulia.

Watu hawa walikuwa kwenye lile lile jengo lililokuwa likitazamana na dirisha la ofisi ya balozi Ally Sapi na wakati huu Kojo na Kizibo walikuwa kwenye moja ya vyumba vya jengo hilo la hoteli huku wakiwa wamekwisha kuweka mtego wao usawa wa lile dirisha ambamo kulikuwa kunafanyika mazungumzo kati ya Balozi Ally Sapi na Honda Makubi,mpelelezi na mfanyakazi ndani ya ofisi za ubalozi.

“Huu nao ni mwanya inabidi uzibwe Kizibo”alisema Kojo huku akishusha kiona mbali.

“Yule bwege anae toka na ule mkoba nenda uuchukue kisha utajua cha kumfanya,huyu kipara mimi bamzibua sasa hivi” alisema Kizibo huku akitema mate pembeni na kidole kikielekea kwenye kifyatulio cha bunduki yake alioipenda na kuihusudu sana.

***
Honda Makubi alifika nje baada ya kuwa ameshasaini kitabu cha mahudhurio na wakati huo huo alikuwa anapitisha mawazo ya kurudi nyumbani kwa marehemu Bulembo ama aendelee na taratibu za kupeleka zile nyaraka kuzihifadhi na kufanya utaratibu wa kuzituma ofisi kuu jijini Dar es laam na wao watajua cha kuzifanyia.

Akaingia ndani ya gari lake na kuliondoa kwenye maegesho maalumu kwa ajili ya wafanyakazi wa pale ubalozini,lakini ambacho hakujua japo alihisi ni kuwa watu wawili ndani ya ofisi zile walikuwa wakimtizama wakati akitoka eneo lile na mmoja kati yao akanyanyua simu na kupiga pahali kisha akarudi kuendelea na taratibu zake za kufanya usafi.

***
Baada ya kuhakikisha Honda ametoka ndani ya ofisi zake balozi Ally Sapi alichukua simu yake na kujaribu kumpigia Rais wa Tanzania,lakini ajabu simu yake ilikataa kutoa mawasiliano nje ya nchi ile ya Congo,akachukua tena simu nyingine maalumu ambayo hutumia kuwasiliana na mkurugenzi wa usalama wa Taifa nayo ikagoma.

Akiwa kashikwa na mashangao na hamaki ya kutoamini,Balozi akaanza kuzunguka ofisi yake kama asie amani uwepo wake mle ndani na hapo ndipo akalikumbuka tena dirisha lake na haraka akataka kuwahi kuishusha pazia.
Doh
Alikuwa amechelewa.
Risasi yenye nguvu ikatua katikati ya paji la uso wake na kusambaratisha kichwa chake kisha kumsukuma nyuma kwa nguvu na mwili wake usio na mhimili wa utimamu ukajibwaga chini kwa kishindo kisha kwa jitihada kidogo ukajitikisa kidogo na kutulia na ukawa mwisho wa Balozi Sapi.

Kule risasi ilikotokea,Kizibo akatema mate mengi chini.
“pyutyaaa”
Kisha akajiramba midomo yake na kuinyanyua bunduki yake na kisha akaanza kuitawanya huku akipiga mluzi hafifu wa ushindi.

*****

Honda Makubi aliegesha gari yake ndani ya geti la la nyumba ya marehemu Bulembo ,kisha akashuka taratibu na huku akiangaza huku na huko kwa umakini wa hali ya juu.

Kama alivyokuwa amepaacha ahsubuh na ndivyo alivyopakuta pakiwa katika utulivu wa kifo huku maiti ya mmliki wa nyumba ile akiwa ndani hana uhai japo wa kupigia chafya.
Honda akasimama kuupisha utulivu katika akili yake na muda huo mikono yake ilikuwa ikifanya jitihada za kujivika mipira maalumu ya viganja vya mikono.

Alipohakikisha amevaa sawia mipira ile,akapiga hatua ndefu na kuufikia mlango kisha akaufungua taratibu huku utulivu ukiwa ni ngao yake muhimu wakati ule.
Taratibu akachungulia ndani kwa tuo, na kutoka pale alipokuwa aliona mwili wa mpelelezi Bulembo ukiwa umelala vilevile alivyouacha na pembeni yake aliona mparanganyiko wa sofa ukiwa kama alivyoacha hapo ahsubuhi,akapiga hatua nyingine kubwa na kwa haraka zaidi kisha katika uharaka huohuo mikono yake ikaurudishia mlango na kuacha ukijibamiza kwa nguvu nyuma yake huku yeye akiwa hana habari nao tena.
Akatazama mazingira ya mle ndani,hakuona mabadiliko yoyote wakati ule. Akapiga hatua na kuufikia mwili wa hayati Bulembo,kisha akainama na kuanza kupekua mifuko ya suruali aliokuwa amevaa hayati Bulembo.
Katika dakika za mwanzo hakuona la maana katika jitihada zake za upekuzi katika mwili ule uliolala bila uhai.
Akasimama huku akili yake ikianza kujutia muda aliopoteza kurudi nyumbani kwa hayati Bulembo.
Hakuwa sahihi katika mawazo yake,hadi pale macho yake yalipo elekea miguuni mwa maiti aliokuwa akiipekuwa wakati ule na hapo tena akili yake ikaganda bila kufanya jitihada zozote za kutaka kujilaumu kama mwanzo.
Bila kufikiri zaidi,mwili ukafanya vitendo.
Haraka akainama na kupeleka mikono yake kwenye mguu wa kulia ambao ulikuwa umevikwa soksi huku ule wa kushoto ukiwa hauna soksi.
Akaivuta ile soksi na wakati ikimalizikia kuvuka akaona kikaratasi kidogo kikianguka kutoka ndani ya soksi ile.
Honda Makubi alitabasamu huku sasa akili yake ikijipongeza kwa kuwaza kurudi tena ndani kwa hayati Bulembo.
Akainama kuikota ile katasi na wakati ikiwa imeenea kiganjani kwake na mwili ukifanya jitihada za kunyanyuka baada ya kuwa umeinamishwa kuanzia tumboni kwenda juu,mwili wa Honda haukumaliza hilo tendo na mara hiyo kikafanyika kitendo cha haraka na wepesi wa hali ya juu kutoka kwa Honda japo matokeo yalikuwa ni kukosea hesabu za gafla.
Wakati akitaka kusimama akaona kivuli kikiwa karibu yake na mara hiyo akasikia msukumo mkubwa kutokea kiunoni kwake na haraka akajirusha mzima mzima kwenda mbele na bahati mbaya hakuwa ameiona meza iliokuwa hatua chache kutoka pale alipokuwa na alipotaka kujigeuza ili aone kilichomsukuma akajikuta akisambaratika chini baada ya kuipamia meza na kusambaratika nayo chini.
Hakuzubaa
Muda huo huo akajigeuza kwa namna ya ajabu kabisa kisha akatumia mkono mmoja kukita chini huku umbo lake refu likiwa wima katika nukta iliofuata na macho yake yakashuhudia kasi ya ajabu ya kiumbe mweusi na mrefu akimfuata kwa kasi ya upepo na kabla hajasimama imara akajikuta akipokea mateke mawili yaliopigwa kwa mtindo wa tandika reli nae hakuwa amajiandaa kwa hilo akaenda chini mazima kwa mara ya pili.
Hakuzubaa tena mana alishaona kasi na ujuzi wa adui yake,haraka akajizoa na kusimama wima huku akisikia maumivu yakimtambaa mwili mzima kuanzia kifuani,na hapo akajikuta akimsifu adui yake yule kwa kuwa na kasi na nguvu ya kumtetemesha namna ile.
Akajipanga.
Adui akausoma usimamaji wa Honda na akajua anapambana na mtu wa kiwango chake nae akafanya haraka ya kuokoa muda na hilo likawa kosa upande wake.
Adui akarusha ngumi kwa ustadi kumwelekea Honda,lakini Honda aliiona na kama utani akahepa na ngumi ikapiga hewa kisha kwa usitadi mkubwa akaachia konde lenye uzani uliokadiriwa na likampata adui ubavu wa kushoto na adui akabweka kama malaya kichochoroni.
Honda akaachia tabasamu la upande kisha akachumpa na kusimama nyuma ya adui aliekuwa anafanya jitihada za kupambana na maumivu ya mbavu zake,kisha akaachia teke moja kali lililojikita usawa wa maungio ya kiuno na uti wa mgongo na adui akabweka tena kwa mara ya pili huku Honda akiachia tabasamu lingine la ushindi na akihepa tena kujiweka mbali na adui aliekuwa anageuka kwa gadhabu.
Kisu.
Honda aliona kisu mkononi mwa adui na hapo akajipongeza kwa zile hesabu zake za kuwa mbali na adui.
Adui alitupa mikono harakaharaka kumchanganya Honda kisha akaachia teke kali lililopanguliwa kistadi na Honda kisha adui akatumia nafasi ile kumchapa konde kali la mbavu kama malipizi na huku akiachia ukelele wa furaha kwa lipizi lake.
Honda akayumba kwa kupoteza malengo kisha akafanya jitihada kusimama imara.
Hakufanikiwa.
Adui akatumia nafasi ile kumshindilia tena mateke mawili ya kifua na kumtupa kwa kishindo sambamba na kabati la vioo lililokuwa sebuleni pale na kusambaratika chini huku vioo vikimjeruhi hapa na pale.
Kutoka pale alipokuwa ameangukia,Honda alimshuhudia adui yake akinesa kwa aina ya ajabu kabisa na kumfikia pale alipokuwa huku kisu kikiwa kimeshikwa imara mkononi,Honda hakutaka kufa kizembe kwa nguvu alizobakia nazo akasimama kwa kasi kisha akajirusha huku mikono yake ikimkumbatia adui usawa wa kiuno na bega likijikita katikati ya tumbo na kumbwaga kwa nguvu chini ya zulia.
Ingekuwa ni mieleka basi hii ingekuwa ni Roman spear,ila hii sasa wakati huo ilikuwa ni Honda spear.
Walipoanguka chini Honda alizisikia kelele za adui yake wazi wazi masikioni mwake na na yeye akajinasua haraka kutoka pale chini akabaki akiwa amesimama huku akitweta kwa maumivu ya majeraha ya kukatwa na vioo vya kabati.

“Bwege sana wewe”
Jamaa alibweka pale chini huku akijizoa zoa kutoka chini na hapo Honda akapata kumtazama vizuri adui yake na akaona kovu baya usoni pake ambalo dhahiri lilimpa tabu sana yule jamaa kuliuguza bila shaka na lilielekea kumtoa jicho upande wa kushoto.
Kovu lile liliongezea mvuto mbaya kabisa katika sura nyeusi ya shababi yule.

“aah nusura univunje kiuno haini wewe” jamaa alizidi kulalama huku akifanya jitihada za kuupata mhimili mzuri kwa kusimama.

“unataka nini kwangu!” hatimae Honda aliuliza.
Na hapo akashuhudia yule bwege akikenua vibaya na hapo Honda akapata kuona kinywa kibaya kutoka kwa yule jamaa.
Kinywani hakuwa na meno mawili ya mbele na ulimi ulikuwa mweusi tofauti na ndimi za binadamu wa kawaida.
“nautaka mkoba mweusi komredi”
Jamaa alijibu swali la Honda.
Honda akatumbua macho kwa umakini kisha akauliza tena.
“mkoba upi?”

“ule uliopewa na Balozi”
Eh bana eh
Honda akizubaa kwa nukta kadhaa za kutoamini kilichosemwa na adui yake.
Kwa nini!.

Kwa sababu alipewa mkoba na Balozi Sapi ndani ya nusu saa iliopita na hakuwa amemuonesha yeyote ule mkoba muhimu wakati ule.
Honda akakumbuka aliuacha ndani ya gari huko nje.
Hata!
Akaruka juu kisha akaachia teke kali lilokuwa likimwendea yule jamaa,jamaa akalegea kidogo na kulikwepa lakini hakujua hila za Honda akajikuta anapokea konde zito katikati ya kifua,jamaa akabweka kama ngedere anaeiba mahindi.
Adui akaenda chini mazima.
Honda akamwendea huku akiunguruma kwa gadhabu lakini hakufika kwa adui yake ambae alijiinua kwa mtindo wa aina yake kisha akaruka kama kima na kuufikia mlango na kutokomea nje kwa kasi ya umeme.
Honda hakukubali Nae akapiga tambo kubwa na kuufikia mlango,haraka akatoka,lakini kasi yake haikumpa matunda aliotaka,isipokuwa kitu pekee alichoambulia ni kuona namna yule jamaa alivyokuwa akimalizikia nje ya geti na kuliacha likijipigiza kwa nguvu.
“Mkoba!!” Honda alijisemea huku haraka akikimbilia gari lake na kujilaumu kwa uzembe wa kutokutembea nao.
Akafungua mlango wa gari lake na kitu cha kwanza ni kuelekeza macho yake pale ulipokuwa mkoba ule ambao sasa alianza kuupa manani kwa kuwa kuna adui asie mjua akiuwinda.
Kwanini! Hakujua japo alihisi.
“kina nani hawa?” alijiuliza huku akianza kutoka ndani ya ile nyumba ya hayati Bulembo.
Akiwa tayari ametoka nje ya uzio wa nyumba ile,mara akasikia ving’ora vya magari ya polisi vikielekea kule alikotokea.
“shiit!!!” alimaka kwa gadhabu kwa kutoelewa ni nani aliewapigia polisi wa Congo katika uharaka wa namna ile.
“Mambo yanazidi kunoga aisee” alijisemea huku akiongeza mwendo wa gari lake kurudi kwa balozi Sapi kumpa taarifa ya alichokiona kule kwa Hayati Bulembo.
Hakujua yajayo…
***

Soma hapa pia
Hekaheka za Komando Zedi Wimba na Jasusi Honda huko Somalia - JamiiForums
 
Riwaya : Mpango wa Congo

Sehemu ya pili


akasikia ving’ora vya magari ya polisi vikielekea kule alikotokea.
“shiit!!!” alimaka kwa gadhabu kwa kutoelewa ni nani aliewapigia polisi wa Congo katika uharaka wa namna ile.
“Mambo yanazidi kunoga aisee” alijisemea huku akiongeza mwendo wa gari lake kurudi kwa balozi Sapi kumpa taarifa ya alichokiona kule kwa Hayati Bulembo.
Hakujua yajayo…
***
Kizibo alishuka ngazi taratibu na begi lake mgongoni huku akipiga mluzi wa wimbo usioeleweka na mara kwa mara akisitisha mluzi na kujisukutua pembe za meno yake kwa kutumia ulimi.
Ungemuona ungejua katoka kupata stafutahi ahsubuh ile ila sivyo,kwake hiyo ilikuwa ni furaha ya kukamilisha jambo fulani kwa uhakika.
Alizidi kupiga hatua zake kwa uhakika kabisa huku mluzi usioeleweka ukisindikiza hatua zake kutoka nje ya hoteli ile ya kifahari na yenye hadhi kubwa katika mji wa Ivuba ndani ya jiji la Kinshasa.
Kizibo alizidi kupiga hatua kuelekea upande kulipokuwa na maegesho ya magari katika upande wa kushoto wa lango la kuingilia ndani ya hoteli ile,lakini mara akasita kuendelea kwenda kule alikokusudia.
Akaitazama saa yake,nayo ikamhakikishia zilikuwa zimepita dakika arobaini na tano bila ya Kojo kurejea na ndie alikuwa na gari la kuwatoa pale na kuendelea na majukumu mengine,sasa gari haikuwepo na bila taarifa ya Kojo.
Hisia zake zikashindana kumpa hisia kamili ya kinachotokea huko aliko Kojo.
Fikira zake zikakoma baada ya simu iliokuwa kwenye mfuko wake wa koti mchinjo aliokuwa amevaa kuita akaitoa na kutabasamu alipoona mpigaji..
“Nambie shetani!!” akatulia kidogo na kusikiliza upande wa pili kisha akasonya na kukata simu huku akianza kubadili uelekeo na kuchukua ule utakao mtoa kabisa nje ya himaya ya hoteli ile.

Nje kabisa aliiona gari yao ikiwa imepaki pembeni kidogo ya barabara,haraka akapiga hatua na kuindea ile gari huku akiwa amehamanika vibaya.

“wewe umekuwaje tena Kojo” aliuliza mara tu alipoingia ndani ya gari ile.
“aisee yule jamaa ndie shetani sasa bwana!!” Kojo alijibu huku mkono wake wa kuume ukifanya jitihada za kujichua upande wa juu kidogo wa jicho lake.
Kizibo akabaki ametumbua macho usoni kwa swahiba wake yule huku akiacha midomo ikimuanguka kwa fadhaa.

“inamaana yule boya ndo kakufanya hivi?” aliuliza Kizibo kwa kutoamini.

“sasa wafikiri nani mwingine!yule jamaa ananguvu sijapata kuona” alijibu Kojo kwa masikitiko ya kukubali kushindwa mbele ya swahiba wake yule wa kufa na kuzikana.

“Dah kwa hiyo ukaumwaga bila…” Akasema kizibo lakini alikatishwa na swahiba ake.

“Aisee bora kujipanga upya jamaa kaniotea vibaya”

“Aisee!!” Kizibo alistaajabu kuona swahiba wake anakubali kushindwa mbele ya windo lao kwa mara ya kwanza tangu waanze kufanya kazi yao hiyo ya umamluki.
Na hata wakati akiendelea kushangaa uso wa Kojo uliozidi kuharibiwa kwa vipigo,na ni wakati huo simu ya mwito maalumu ipopigwa..
Walitazamana.

Kizibo aliipokea na pasipo kusema kitu akawa anasikiliza maelekezo kutoka upande wa pili na maelekezo yalipokoma,Kizibo akaachia tabasamu la upande mmoja huku ulimi wake ukisukutua pembe za meno yake,kisha akaachia mluzi usioeleweka masikioni mwa Kojo.

“sasa tajiri anasema turudi kupumzika matokeo amepata ya kazi yangu,Mkoba ule na kilichomo kasema tumwachie yeye ataona cha kufanya katika mkakati wa pili” alifafanua kwa kirefu Kizibo.

“Bora nami nijitibu kidogo mana yule jamaa angenivunja leo”
Wakaliondoa gari.
Lakini kama walijua wanaenda kupumzika walijidanganya.

***
Mawazo yalikuwa yanampita kichwani kwa kasi sana ,kwa kutoelewa ukweli wa mambo ulivyo,mara kwa mara alikuwa anatizama nyuma kuona kama alikuwa hafuatiliwi na alipojiridhisha aliendelea na safari yake.
Nusu saa badae alikuwa anashugulika na kuiweka sawa gari yake kwenye maegesho yalio katika ofisi za ubalozi wa Tanzania nchini Congo.
Honda alitizama nje kabla ya kushuka ndani ya gari na alichokiona kikamtia mashaka.
Akashuka taratibu huku mkoba mweusi ukiwa ameushika katika mkono wake wa kulia.
Alitembea taratibu kuelekea eneo la mapokezi,na hapo akaushuhudia mshituko na taharuki kwa baadhi ya wafanyakazi wa ubalozi ule.
Akamakinika zaidi hasa alipoona polisi wa Jamhuri ya Kongo wakiwa ni miongoni mwa wafanyakazi wale.
Akaangaza macho yake,kumtafuta mtu muhimu wakati ule na akamuona nae akiwa ni miongoni mwa watu waliopagawa kupindukia.
Walitazamana kisha zikafuata ishara na hapo mtu yule agaeuka na kuelekea upande kulikokuwa na ofisi zake,Honda akamfuata.
Alikuwa ni mkurugenzi wa usalama ndani ya ubalozi japo wachache walijua hivyo na wengi ya wafanyakazi walijua ni Ofisa uhamiaji pale Ubalozini.

“Kuna nini Mndewa!” aliuliza Honda punde tu baada ya kuingia ndani ya ofisi ile.

“Balozi Ally Sapi kauwawa na pia taarifa nyingine ni kuwa Bulembo nae kauwawa leo ahsubuh” alijibu kwa kirefu Mndewa.

“Doh!!.. Bulembo taarifa zake ninazo ila hii dah..” Honda alishindwa kumalizia na hapo akajikuta anaangusha chozi bila kutoa sauti.

“wamewezaje kumuua Balozi aisee!” Honda aliuliza kwa kutoamini kabisa tukio lile.

“kwa haraka haraka inaonekana amedunguliwa aisee” alijibu kwa huzuni Mndewa.
Kimya kikapita.
“Sasa umeshatoa taarifa makao makuu!” aliuliza Honda.
“ Huwezi amini,simu tangu ahsubuh hazitoki eneo hili,ila tumejaribu kutuma ujumbe wa tarakirishi na bado hatujajibiwa kabisa Honda”
Mkurugenzi Papi Mndewa alionesha masikitiko yake katika hilo.
“Hujuma!” Honda alijiwazia kisha bila kutoa na kumshirikisha mkubwa wake juu ya mashaka yake hayo, akamuomba waelekee huko ofisini kwa Balozi Sapi.
***
Dakika tatu baadae walikuwa ndani ya ofisi za Balozi Sapi na kulikuwa na askari kadhaa kutoka kituo kikuu cha polisi Kinshasa waliokuwa wakiendelea na utaratibu wao ili kuhakikisha wanakuwa na ushahidi mzuri katika harakati za kumsaka muuaji.
Mbali na askari hao,pia walikuwapo wafanyakazi kadhaa wa ubalozini.

Honda akatembea taratibu na kuufikia mwili wa hayati Ally Sapi uliokuwa umeshafunikwa shuka jeupe.
Aliufunua na kutazama na alishuhudia namna risasi ya mdunguaji ilivyofanya kazi yake ipasavyo.
Akatikisa kichwa kisha akaufunika ule mwili na kuendelea kuangalia kwa jicho la upelelezi ndani ya ofisi ile.
Macho yake yakagota kwenye dirisha.
Hapo akaona mpasuko wa kioo,na moja kwa moja akili yake ikamwambia mdunguaji alikuwa upande ule wa ile Hoteli.
Lakini kuna kitu kingine akaona hakiko sawa katika dirisha lile.
Mwanzo hakutilia maanani wakati walipokuwa wakizungumza na Balozi Sapi ahsubuh ila sasa alianza kuhisi jambo katika dirisha lile.

Dirisha lilikuwa wazi.
Yaezekana uwazi ule usingemshitua,ila kilichomshitua ni namna lilivyokuwa kimefungwa na hapo akili yake ikakumbuka kuliona dirisha likiwa wazi wakati akiwa anazungumza na Balozi Sapi.
Makusudi hii!
Alijiwazia hivyo wakati akijua kabisa Balozi Sapi hakuwa na kawaida ya kuliacha wazi hilo dirisha hata mara moja.
Akawageukia wafanyakazi wachache waliokuwa mle ndani,akawatazama mmoja mmoja bila kujua msaliti ni yupi.

“Nani hapa Honda Makubi?”
.sauti ya askari mmoja ikaunguruma kutokea mlangoni alikokuwa anaingilia yule askari ambapo baada ya kugeuka,Honda na wenzie walijua fika cheo cha askari yule ni Sajini kulingana na vazi alilokuwa amevaa kumtambulisha kwa cheo hicho.

“watu wote mle ndani walitazamana huku wote wakizisikia hatua zilizokuwa zikipigwa na Sajini Kebu Habyirimana.

“jamani okoeni muda tuna majukumu mengi ya kufanya huko!” alikoroma Sajini Kebu.

Sajini Kebu alizidi kuzipiga hatua zake taratibu hadi ulipokuwa mwili wa Balozi Ally Sapi,akainama na kuufunua kidogo kisha akaufunika na kunyanyuka.

“nani mwenye ji…” Sajini Kebu hakumaliza kauli yake,akakatishwa na sauti ya mtu mle ofisini.

“Ni mimi hapa,naitwa Honda Makubi!”

Sajini akageuka taratibu na kuelekeza kule usawa wa dirishani alikosikia sauti ya mtu aliejitambulisha kama Honda Makubi,macho yao yakagongana na kila mmoja aliyasoma mengi yalioongelewa na macho yale.

Wakati Sajini Kebu yeye akiona macho makini na yenye kutaka kujua utata wa kifo kile cha Balozi Sapi,..
Honda yeye alikuwa anatazama macho yaliojaa uhalifu na ujivuni wa matukio mengi ya umwagaji damu,alihisi yote lakini hakuwa na sauti ya kusema mapema kiasi kile kumtuhumu Sajini Kebu kuhusika na masakata yote yale ndani ya mitaa ya Ivuba Kinshasa Congo.

“Bwana kwa maelezo yaliopatikana inaonekana mtuhumiwa wa kwanza ni wewe,hivyo tutaenda na wewe kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi!” alisema Sajini Kebu huku akipeperusha juu karatasi ya arresting order

Kaipata wapi muda mfupi hivi!!

Lilikuwa swali lilitambaa haraka kichwani mwa Mkurugenzi Papi na Honda Makubi kisha bila kutarajia na kama mawazo yao yalikua sawa wakajikuta wakitazamana na hapo wakapeana ishara ya kijasusi walioilewa wao wenyewe wakati ule.

“Sawa afande!!” alijibu Honda.
Kwa jibu lile ilikuwa ni zamu ya Sajini Kebu kushangaa.
Katika majibu rahisi aliotegemea kuyapata kutoka kwa Honda hili la kukubali bila kuhoji lilimshangaza sana,japo alijaribu kuuficha mshangao wake ila si kwa mtu makini kama Honda makubi na hilo alilitegemea.

“Nyakati kama hizi adui wa kwanza ni anaekukamata alietuma ukamatwe” alijiwazia Honda.

“Aah unampeleka kituo gani Sajini” alihoji Mkurugenzi Papi.

“Kituo kikuu hapo Ivuba” alijibu Sajini Kebu huku akianza kuondoka ndani ya ofisi ile na nyuma alifuatiwa na Honda Makubi.

Walitembea kwa dakika tatu nzima,kutoka zilipokuwa ofisi za Balozi Sapi hadi kutoka nje ya jengo lile la ubalozi.

Nje macho ya Honda yalikuwa yanatembea kwa hatua za uhakika na hapo yakatua kwenye gari aina Toyota defender ya kipolisi na ndani yake walikuwamo watu watano waliokuwa wamebeba silaha aina ya SMG na kila mmoja alikuwa amevaa fulana ya kuzuia risasi,mbali na hivyo kila mmoja alikuwa amevaa mipira mizito ya kufunika viganja vya mikono yake.
Yote haya aliyaona wakati wakizidi kupiga hatua kulifikia gari lile ambalo aliliona tangu akitoka ndani ya ubalozi.

Hatua kadhaa kabla hawajalifikia lile gari wawili Kati ya watu wale watano wakaruka chini katika namna ambayo ilimfurahisha Honda.
Ilimfurahisha kwa sababu aina ile isingeweza kuwa ya askari wa kawaida,aina ile ni ya makomando waliofuzu vizuri kabisa.
Kumekucha!!

Honda na Sajini Kebu walilifikia gari lile na hapo Sajini Kebu akaenda kukaa mbele upande wa pili wa dereva.

Honda hakuwa amefanya jitahada zozote kupanda katika karandinga lile na alikuwa na sababu zake za kufanya hivyo.
Haukupita Muda mrefu alichokitaka kikatimia na hii ni baada ya wale askari wawili waliokuwa wamesimama chini,mmoja wapo alimfuata kwa hatua za ajabu kabisa na alipomfikia akamshika suruali yake na kuinyanyua juu (huku kwetu tunaita Tanganyika jeki) na punde askari wa pili nae akamcharaza mtama safi kabisa kwa aina ya kidon,mapigano adhimu katika nyanja ya ujasusi na hapo Honda akajikuta anapaa juu bila kupenda na kabla hajaanza kushuka chini akadakwa na mikono imara ya askari mwingine aliekuwa ndani ya karandinga,kisha akamvutia juu kwa kasi na kumbwaga katikati ya miguu ya askari watatu waliokuwa wamebaki mle ndani ya karandinga ile na alipotaka kujizoa zoa kusimama akakutana na midomo miwili ya smg ikimtizama huku masikio yake yakinasa sauti ya mwendo wa karandinga lile na alipotizama kwa makini askari wote watano walikuwa ndani yake, hakujua wamepanda saa ngapi wale wawili kutoka kule chini walikomwadhibu.

Honda akatabasamu na hapo lengo la kutaka kujua uwezo wa askari wale lilikuwa limetimia,
“hakika hawa si askari polisi wa kawaida ni zaidi ya askari,wanauwezo na nguvu na uharaka wa mawasiliano” alijisemea Honda Makubi.

Safari yao ilikuwa imetawaliwa na ukimya wa kutisha,hakuna aliemsemesha mwenzie na muda wote macho ya askari wale hayakutoka kwa Honda,walikuwa makini na kila mjongeo alioufanya Honda.

Akili ya Honda iliendelea kufanya kazi kwa kasi na hasa hisia zake zilipomwambia hakuwa katika mikono salama,akautazama mkoba mweusi uliokuwa umetulia ubavuni mwake huku mikanda yake ikiwa imepita juu ya bega la kulia na kushuka hadi upande wa kushoto wa mbavu zake.

Akakumbuka alikuwa amepewa mkoba ule na Hayati Ally Sapi na hakuwa amemwambia kuna nini mana hata Sapi mwenyewe alikuwa amepewa na marehemu Bulembo.
Akiwa ndani ya fikira hizo akakumbuka kikaratasi alichotoa kwenye soksi za marehemu Bulembo kabla hajakurupuliwa na yule mtu mbaya wa sura na ulimi wa ajabu hajapata kuona.
Alitamani kukisoma kile kikaratasi,ila akajionya kutokufanya kosa lolote katika wakati kama ule ambao hajui wapi anapelekwa.



Itaendelea
 
Riwaya : Mpango wa Congo

Sehemu ya tatu


Alitamani kukisoma kile kikaratasi,ila akajionya kutokufanya kosa lolote katika wakati kama ule ambao hajui wapi anapelekwa.
*****

Gari ilizidi kuacha mji wa Ivuba na haikufuata barabara kuu ya Julius Nyerere kuelekea katikati ya Mji wa Kinshasa au barabara ya Nailogi kuelekea kituo kikuu cha polisi Ivuba,badala yake ikawa inaelekea katikati ya mji unaokaliwa na waasi wa ADF(Allied Democratic Forces) hiki ni kikosi cha waasi kinachoshambulia mara kwa mara nchi ya Congo japo hujipambanua kama kikosi kinachompinga Rais wa Uganda.

Karandinga lilizidi kuiacha Ivuba na Kinshasa na sasa uelekeo wake ulikuwa ni kaskazini mwa Congo katika Jimbo la Kivu.

Safari ilikuwa ni ya mwendo kasi sana na muda wote watu wale walikuwa kimya kabisa.

Wakiwa wameanza kutoka kwenye makazi ya watu mara gari ikasimama gafla na haraka Sajini Kebu akateremka kisha akaja nyuma ya karandinga lile,hakusema kitu akatoa ishara fulani na mmoja kati ya askari akashuka chini na kwenda kumsikiliza Sajini.

Honda alikuwa akiwatizama kwa makini sana na aliona wakiteta jambo huku wakimtizama kwa macho ya wizi wizi.
Macho yao na maongezi yao yakamtia shaka ila akajipa muda wa maamuzi kwa sababu hadi muda huo hakujua nini alitakiwa afanye na pia hakujua kwa nini mauaji yamewaandama katika ofisi yao,hivyo alihitaji kujua zaidi ila alikwamishwa na aina ya watu waliomzunguka.
Sajini Kebu aliendelea kuteta na yule askari aliemuita huku kila mara wakiendelea kumtazama Honda.
Baada ya mazungumzo yao kuisha ndani ya dakika tano,Sajini Kebu na yule askari wajongea kwenye lile karandinga na walipolifikia,tofauti na matarajio ya Honda kuwa Sajini arudi kuvunja kishoka kule mbele na safari iendelee,ilikuwa tofauti badala yake wote wawili wakaja hadi nyuma ya karandinga na kisha wakapeana ishara na wale waliokuwa ndani ya karandinga lile kisha wakateremka wote wanne waliokuwa wamesalia na hapo ndipo Honda akachezesha akili yake kuona lipi rahisi kulifanya kwa wakati huo na akapata wazo moja tu,kukisoma kikaratasi alichokichukua kwa marehemu Bulembo.
Akakisoma ila hakuelewa kilichoandikwa kwa uharaka ule,akakariri kilichoandikwa mana hakutaka kuamini kilikuwa kimeandikwa bahati mbaya,na kama ni bahati mbaya inamaana gani kufichwa kwenye unyayo wa miguu na kufunikwa na soksi?
Mana ipo!!
Akarudia tena kukisoma.

“142BOULEVARD DU JUIN
B. P. 1612
KINSHASA CONGO (81).”

Alipohakikisha kilichokuwa kimeandikwa kimemkaa kichwani,akakitafuna haraka sana kile kikaratasi na kukimeza.
Kitendo hiki kilifanyika ndani ya nusu dakika tu kiasi kwamba hata wale askari licha ya kuendelea kumtazama hawakufanikiwa kuona uharaka wa kitendo kile.

Wajanja walikutana na mjanja!!.
Dakika mbili badae askari watatu walipanda kwenye karandinga na bila kumsemesha wawili wakamfuata na kunyanyua juu kimabavu,nusura wambwage chini kisha kwa mbwembwe wakamsukuma nje ya karandinga nae akatua chini kwa mbwembwe zile zile bila kuumia na ilikuwa rahisi kwake mana walikuwa hawajafanya jitihada zozote kumfunga.
Kitendo chake cha kutoanguka kikawa kama kimewatia hasira,wale wawili waliokuwa wamebaki chini wakampokea kwa kipigo kizito bila kujali anakwepa au la.
Kipigo alichopewa Honda ndani ya dakika tano kilitosha kumuacha bila nguvu za kusimama na hapo ndipo akagundua alikuwa anapigwa na askari wote watano isipokuwa Sajini Kebu,ambae muda wote alikuwa kimya akishuhudia vijana wake wakimsulubu mfanyakazi yule wa ubalozi wa Tanzania nchini Congo.

Sajini Kebu alipiga hatua moja na kufika pale alipokuwa Honda akitweta kwa maumivu,akamwinamia na kumshika ukosi wa shati lake kisha akamvuta kwa nguvu na kufanya nyuso zao zitazamane kwa karibu zaidi na bila kusema kitu Sajini Kebu akamshushia kichwa kizito Honda na kumuacha akiwa na nundu kwenye paji la uso huku akijibwaga chini kama mzigo ulioozesha matunda.

Honda alipoanguka akafanya jitihada za kunyanyuka na hapo akaona Sajini Kebu anamfuata tena kwa gadhabu na bila kusema kitu akawahi kuushika mkoba uliokuwa ukininginia shingoni Honda.
Honda hakutaka kukubali kizembe,nae akajitutumua kumdhibiti Sajini Kebu asichukue ule mkoba.
Dhamira yake ya kuulinda ule mkoba ukagonga mwamba bada ya mmoja wa askari wale kumchapa teke la kifua na kumyanyua juu kisha kubwagwa chini kwa uzito wa teke lile na hapo askari mwingine akaudaka ule mkoba na kuutoa shingoni kwa Honda.
Honda hakuwa na la kufanya akabaki akitweta kwa maumivu huku akipanga namna ya kuwadhibiti watu wale ambao tayari walionekana si wema kabisa.

Baada ya Sajini Kebu na wenzie kuona wamemdhibiti Honda; akauchukua mkoba ule na kuanza kuukagua kwa umakini sana
 

Similar Discussions

20 Reactions
Reply
Back
Top Bottom