Jasusi Honda ndani ya mpango wa Congo

Riwaya :Mpango wa Congo

Sehemu ya nne


Baada ya Sajini Kebu na wenzie kuona wamemdhibiti Honda; akauchukua mkoba ule na kuanza kuukagua kwa umakini sana.
Kitu cha kwanza kukutana nacho ni karatasi mbili nyeupe za ukubwa A4,sura ikambadilika Sajini Kebu, akafanya papara kuanza kupekuwa mkoba ule, na hapo akavuta hisia za wengine nao wakapoteza umakini wa kumlinda Honda, wakabaki wanashangaa zile karatasi nyeupe mbili zilizokutwa ndani ya mkoba walioagizwa kuukagua.
Kama Sajini Kebu alidhani mshangao huo ulikuwa kwake tu,alikuwa anajidanganya.
Mshangao mkubwa yaezekana kuliko wote waliokuwa eneo lile alikuwa ni Honda Makubi.
Licha ya wepesi wa wa mkoba ule, lakini hakudhani kutakuwa na karatasi mbili pekee tena moja ikiwa haijaandikwa kitu kabisa na nyingine ikiwa na namba tu tena namba zilikuwa nne tu huku mbili kati yazo zikiwa zimezungushiwa duara huku hizo mbili zingine zikiwa zimepigiwa msitari mfupi kwa chini kila moja.
Ina maana gani hii!!!!

Wakati Honda akiendelea kujiuliza; wakati huo Sajini Kebu nae alikuwa anapata mshangao mwingine zaidi.
Ndani ya mkoba alikuta kidole cha shahada cha binadamu, na kilionekana bado kina damu kabisa na ilionekana haina siku nyingi damu ile.
Aliogopa kukishika kidole kile na hata yeye hakujua kwa nini alijikuta anaogopa gafla namna ile.
“inamaana,… aha..” Sajini Kebu akili ilishindwa kupambanua na akajikuta anaishia kutabasamu tu huku akipitisha macho kushoto na kulia kuhakikisha wengine nao wanauona mshangao wake.
Sajini Kebu macho yake yakatua kwa Honda aliekuwa bado amekaa chini nae mshangao ukiwa juu yake. Sajini akamkazia macho Honda.

“Nini hii!?” aliuliza Sajini Kebu huku akiwa bado ameushikilia mkoba ule mweusi na kuulaza upande ili zipu ya katikati iliokuwa wazi imsaidie Honda kujua yaliomo ndani ya mkoba na kubwa zaidi wapate kujua Honda anataarifa na yaliomo?

“Na mimi kama wewe komredi!” alijibu Honda huku dhahiri mshangao ukiwa bado u machoni pake na masuali kadhaa yakiwa yanatiririka kichwani kwake.
“Kile kidole cha nani, na kwanini karatasi hazijaandikwa kitu” Maswali hayo yalipita bila kupata majibu.
Honda hakupata jibu la hayo maswali ila aliamini majibu yapo kwenye hizo karatasi,lakini sasa hiko kidole kimefuata nini tena humo kwenye mkoba!
“ina maana hata balozi alijua kuhusu hiko kidole? Mbona hakunambia?” Maswali kama mvua yalizidi kutiririka kichwani mwa Honda.

Sajini Kebu akiwa bado haamini alichokiona,mara hii akaamua kung’uta kabisa mkoba ule.
Hali ile ile!
Hakuna jipya lilopatikana zaidi ya karatasi zile mbili na kile kidole.

“sasa utatuonesha ilipo maiti ya hiki kidole Honda!” Sajini Kebu aliongea huku akiutupa ule mkoba mweusi chini na kupiga hatua ndogo ndogo zilizoonesha gadhabu ya hali ya juu kwa mtembeaji yule, ofisa wa jeshi la polisi Congo.
Hatua za Sajini Kebu zilihesabiwa vizuri na Honda akiwa pale chini, kisha akaacha masikio yaendelee kuusikia mshindo wa miguu ya Sajini Kebu na macho yakawatazama askari wengine watano na bunduki zao mikononi.
Alihitaji kufanya jambo.
Muda haukuwa rafiki wakati huo na alihitaji majibu kuhusu mauaji ya Bulembo na Balozi Sapi, hivyo kusubiri kipigo kutoka kwa watu wasio wema, ilikuwa ni kuzidi kujiweka mbali na ukweli.

Kebu alizidi kumsogelea Honda huku mkono wake ukiwa unatoa bastola iliokuwa ameisunda kiuononi kwake,hata wenzie hawakujua alitaka kuifanyia nini ikiwa walimhitaji Honda katika harakati za kuzima jambo wasilotaka lijulikane.

E bana eh!

Honda alisimama kwa mtindo wa ajabu haijapata shuhudiwa na askari wale na mkononi mwake alikuwa na kisu.
Alipokipata hawakujua!
Ila Honda alikichukua kwa mmoja ya askari wale wakati wakimshambulia kwa kipigo.
Wakati wakishangaa kasi ya usimamaji wa Honda, tayari Honda yeye alikuwa uso kwa uso na Sajini Kebu na bila kuchelewa akamnasa kofi kali la uso, wakati Sajini akifumba macho kusikilizia maumivu, tayari kasi ya Honda ilikuwa imemfikisha nyuma ya mwili wa Sajini.
Kebu bila kupenda akajikuta amejaa kwenye kabari matata ya Honda huku kwa mbali akizisikia pumzi za Honda nyuma yake.
Akawa mbuzi wa kafara!!
Askari wengine wakabaki kuzikoki silaha zao bila kuwa na maamuzi sahihi ya kufanya kumuokoa kibaraka mwenzao.

Honda nae akazidi kupiga hatua za kuwatoka, lakini anawatokaje wakati karatasi na kidole vimesambaratika chini?.

Pagumu!!

*****

NCHINI TANZANIA.


..JIJINI MWANZA….

“Hata!! Hii imekaaje tena sasa!!” alijiwazia wakati akiwa ameshika kiuononi na mkono mwingine akivua kofia iliokuwa imemziba uso wake, hakuwa anaamini anachokiona.Hii ilikuwa ni nyumba ya pili alioikusudia na hali aliikuta sawa na alikotoka.
Chumba alimokuwamo kulikuwa kumeparanganyika hovyo hovyo kuonesha kwamba kulifanyika varangati na upekuzi wa hovyo kabisa.

“na wao walikuwa wanatafuta nini sasa!” alijiuliza tena bila wa kumpa jibu kuonekana.

Hata!

Aliendelea kutalii kwa macho kile chumba ili walau apate pa kuanzia kujua maswahibu yaliomkuta mtu aliemkusudia.
Hakuona kitu zaidi ya maiti ya mwanaume iliokuwa ikimtizama kwa huruma ya kukutana na kiama.

“Hii ni kazi maalumu sasa nani kaaingilia gafla hivi mmh” alijiuliza tena bwana yule huku akitoa simu mfukoni mwake na kupiga pahali.

“Nambie Mtegaji !” ilisema sauti upande wa pili.

“Aisee hali ile ile kama kule nilikotoka” alisema Mtegaji na huku akisikilizia mguno wa mshangao upande wa pili.

“Sasa Mtegaji ; huoni wanakuchokonoa afu wanarudi pangoni?”ilisema sauti upande wa pili.

Kama kuna mtu alijua kucheza na akili za Mtegaji ni huyu aliekuwa anaongea nae na hapo alikuwa amegusa penyewe
Kajazwa kichwa ebo!!
Mzee Kinyonga alikuwa amempa ruhusa kijana wake wa kazi maalumu ya kuwasaka wanaotaka kutibua mipango yao waliopewa kuikamilisha.

“Mtega Nyoka, hao Nyoka wananitega mi Kinyonga, hebu wapekenyue komredi!” ilisema sauti ya Mzee Kinyonga na kukata simu.

“wao Nyoka mi mtegaji, ama zao ama zangu” alijiwazia

“Mimi ndie MTEGA NYOKA bana waga hawanishindi hawa Nyoka” alifunga mlango na kutokomea kama alivyokuja.

Mtega Nyoka!!
Ndio alikuwa ni Mtega Nyoka, Nyoka wanaomwinda Mzee Kinyonga!!

Ila kama alijua ni kazi rahisi kumlinda Kinyonga mbele ya nyoka wakaao pangoni, yaezekana alikosea kufikiri vema.


Itaendelea
 

Similar Discussions

20 Reactions
Reply
Back
Top Bottom