Jarida la Sani limerudi sokoni

Jarida la Sani limerudi sokoni

Haliwezi kuwa kama lile la enzi hizo
Kwa ushauri tu wangefanya muendelezo wa stori, na hili la sasa likawa ni season nyingine kabisa wakijaribu kuiga ya wakati ule halitakuwa na ubora ladha nyingi zitapotea, kipanya ahusike kwenye michoro
 
Nimefurahi kurejea kwa sani ila sina uhakika na ubora ule wa miaka ya 80 na 90
 
wale mapacha mmoja aliitwa sunche na mwingine kapeto.bila kumsahau ndumilakuwili,bob makani,pampula,etc
Lodi lofa, Dr Love Pimbi, Bila kusahau ile UEFA ya Bush stars na Born town
 
Ha ha ha harakati za pimbi, jamaa hajawahi kabisa kufanikiwa, nampendaga comred kipepe na rungu lake ni kuwinda vitoweo tu afu nae hatari hawapati lol
Kule kwenye mpira ndo bas kabisa
Mpira balaa..Yale maneno yao ya shombo uwa yananikosha sana....Dr love safari hii wamfanikishe hata mara moja bana...japo aonje utamu wa papuchi
 
Mpira balaa..Yale maneno yao ya shombo uwa yananikosha sana....Dr love safari hii wamfanikishe hata mara moja bana...japo aonje utamu wa papuchi
Ha ha ha akifanikiwa harakati zitakosa mvuto aendelee hivo hivo
 
Kwa ushauri tu wangefanya muendelezo wa stori, na hili la sasa likawa ni season nyingine kabisa wakijaribu kuiga ya wakati ule halitakuwa na ubora ladha nyingi zitapotea, kipanya ahusike kwenye michoro
Hilo la kipanya hata mm nilifikiri hivyo, ladha ya sani ni katuni bhana, katuni inamvuta mtu kusoma maneno. Lodi lofa. Kipepe, kijana wa totooz pimbi, mtoto wa elimu bureee madenge, hebu tuleteeni huo uhondo
 
Lodi lofa, Dr Love Pimbi, Bila kusahau ile UEFA ya Bush stars na Born town

Mimi nilikuwa nachanganyikiwa kuona Madenge eti ni golikipa wa timu ya wakubwa wakati anasoma primary tena kama darasa la tatu tu.

Nilikuwa nachukulia kama issue ni za kweli yaani.
 
Bush Stars walikuwa na Mzee Meko, nadhani timu nzima ndo alikuwa anavaa shati, kuna kipindi alipataga timu South Afrika, sina uhakika kama aling'ara kama huku Bongo. Jamaa alikuwa mkali balaa.

Kulikuwa na jamaa mmoja mbabe Bush Stars anaitwa Hui Hui, sijui yuko wapi siku hizi.

Umemsahau na kabelo
 
Umemsahau na kabelo

Ha ha ha, timu ilikuwa imesheheni.

Huku Born Town matozi kibao, kipa wao Rasta, kuna kina Ndumilakuwili, Lodi Lofa, Pimbi.

Hivi Sokomoko alikuwa Town au Bush?
 
Ha ha ha, timu ilikuwa imesheheni.

Huku Born Town matozi kibao, kipa wao Rasta, kuna kina Ndumilakuwili, Lodi Lofa, Pimbi.

Hivi Sokomoko alikuwa Town au Bush?
Golden boy mapung'o wa bush stars
 
Back
Top Bottom