Jarida la Sani limerudi sokoni

Jarida la Sani limerudi sokoni

Jarida lako pendwa la SANI lipo mtaani sasa, kila Alhamis.
Unazikumbuka Story za Madenge, Kifimbo cheza, Mzee Fukunuku, Zena na Betina. Lodi Lofa, Sokomoko, Pimbi n.K.

Usiwakose leo kwenye Jarida la SANI kwa Tsh.1000 tu.
 

Attachments

  • 1453268388939.jpg
    1453268388939.jpg
    74.2 KB · Views: 184
Ladha huenda ikabadilika kidogo kutokana na mazingira ya wasomaji ila wajitahidi burudani ibaki ileloe au wakiweza izidi ile ya mwanzo.
 
Aisee kitambo sana,mishe mishe za ndumilakuwili balaa
 
Okay mzee wa kurekebisha wachafuzi wa lugha,pia mzee wa misemo.
 
Nadhani limerudi jina ila Ladha sio ile kabisa, kumbuka watunzi wengi wa Vichekesho vya Sani walikwisha tangulia...
1453268942503.jpg
1453268954522.jpg
 
watatukumbusha tulikotoka, enzi za vikaragosi vya marehemu ndunguru na wenzake,
jambo limezua jambo...
 
Kwenye sani Original kwa wale wapenzi wasoka jamaa walikuwa wanachora mechi mpaka watu wanahisi wako pitch kabisa....Wengi wetu humu ndani tumesoma Mabaki ya sani yaani yale yaliyonunuliwa na wazee wetu alafu wakayatunza..
 
Asikwambie ile game ya town stars na bush stars mapung'o na Chepe..! Wapi baba ubaya na mzee wa busara.
 
Wimbi la Kitintale litakuwepo? Akina Obi, Linda na Mayuku

Mzee Tupatupa
 
Nitafurahi sana kumwona madenge, kipepe, lodi lofa, prof ndumilakuwili, zena na betina, mzee kifimbo cheza, bila kusahau stori kali siikumbuki jina ila kulikua na mhalifu anajiita Mark Steven Chenje.
 
Back
Top Bottom