Japan yaisaidia Tanzania Sh. milioni 640

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
Japan imekubali kutoa Sh. milioni 640 kwa Shirika la Elimu, Sayansi la Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Tanzania kutekeleza mradi wa kuwasaidia wasichana waliolazimika kuacha shule kutokana na kupata mimba za utotoni.

Pande hizo zilitiliana saini jana jijini Dar es Salaam, ambapo Tanzania iliwakilishwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Selestine Gesimba na mwakilishi wa UNESCO, Vibeke Jensen.

Mradi huo wa miaka miwili unalenga kuwasaidia wasichana wenye umri kati ya miaka 13-19 wanaoachishwa masomo kutokana na kupata mimba za utotoni. “Kiasi hicho cha pesa kinalenga kuwasaidia wasichana walioachishwa masomo kwenye shule za Sekondari kwa sababu ya ujauzito kupata fursa mbadala za kusoma na kuwawezesha kiuchumi,” Alisema Jensen.

Alisema mradi huo utalenga zaidi katika wilaya za Shinyanga Vijijini na Kahama kwa sababu Shinyanga ni kati ya mikoa iliyoathirika zaidi na tatizo la wasichana wadogo kuachishwa shule kutokana na mimba za utotoni.
Jensen, aliishukuru Japan kwa msaada huo na pia aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa utayari wao wa kutoa fursa ya kujiendeleza kimasomo na kiuchumi kwa wasichana wanaopata mimba za utotoni.




CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom