January Makamba ni muongo kuhusu umeme

TikTok2020

JF-Expert Member
Oct 20, 2022
1,817
3,144
January Makamba anasumbuliwa na tatizo kubwa sana la kutojua hesabu na kusema uongo. Anataabishwa sana na kufanya mambo ili kuonekana anafanya makubwa wakati ukweli ni kuwa mbali na maonyesho ya kusaini mikataba kila siku na kuleta porojo za miradi ya umeme bado taifa hili lina matatizo makubwa sana ya umeme

CAG alituambia jinsi alivyodangaya kwenye idadi ya vijiji vyenye umeme wa REA na hilo tunasubiri muda ufike tutakijadili kwa sababu halitapita kimya.

Leo amenukuliwa akisema kuwa ni vijiji 2000 tu havina umeme Tanzania na vitapata umeme Juni 2024.

Waziri huyu asiyejua hesabu jana alisema ni asilimia 94% ya vijiji vyote imefikiwa na umeme na vyombo vya habari vikamnukuu.

Tanzania ina vijiji 12,319 kwa mujibu wa sensa ya makazi na watu ya hivi karibuni.

94% ya vijiji 12,319 ni vijiji 11,580 na hivyo asilimia 6% iliyobaki ni 12,319-11,580 ambapo ni vijiji 739 tu.

Kwa mahesabu haya maana yake vijiji visivyo na umeme ni 739 tu kwa Tanzania nzima ambavyo kimahesabu ni 6% tu ya vijiji vyote nchi nzima.

Sasa leo anaposema vijiji 2000 tu havina umeme anatoa wapi haya mahesabu? Maana vijiji 2000 ni 16% ikiwa na maana vijiji vyenye umeme ni 84%. Yeye anapata wapi 94%? Waziri hajui hesabu? Waziri ni muongo? Waziri anadanganya taifa? Yote haya ni majibu sahihi kwa kuwa hivyo ndivyo hesabu zinavyosema kwa maneno yake mwenyewe.

CAG alituambia juu ya udhaifu wa kupikwa kwa hizi taarifa za vijiji vilivyowekewa umeme na REA na hili linafanywa na hii wizara ili kuonyesha wanafanya mambo makubwa sana wakati kiuhakisia hakuna kitu wanafanya kama wanavyojinasibu.

January Makamba ni waziri muongo na hana akili za kufanya mahesabu hivyo anaishia kupika takwimu ambazo kimahesabu zinakuja kumuumbua na kudhalilisha hii serikali.

Taifa hili lina mainjinia wengi wanaoweza kuwa mawaziri kwenye hii wizara, wapewe hii kazi kuliko kuendelea na huu ujinga tukidhani tunalisaidia hili taifa.

Waziri huyu ni mzuri kwenye kuandaa matamasha na mikutano kwa kuwa ndiyo mambo kasomea basi kama mnamhitaji serikali basi mpelekeni wizara ya michezo akawe anashirikiana na TFF na BASATA kuandaa matamasha au wizara ya wanawake na watoto kule kuna matukio mengi yanayotaka matamasha ambayo ni sekta anayoiweza sana.

Kumuacha hapa ni kupata aibu za hivi anashindwa kufanya mahesabu mepesi kwa sababu ni muongo na mbadhilifu na kakosa maarifa ya kufanya hesabu kwa utulivu.
 
2da929da-cc70-45f4-af40-94c37e35a5b3.jpg
 
Dah jamaa anaandamwa mpaka kabla ya budget kaamua kugawa mitungi ya gesi
 
Mpeni muda j Makamba anayo nia ya dhati kusimamia kuungwa Kwa umeme vijiji vyote nchini hilo suala la hesabu kumpiga chenga isiwe sababu ya kuonekana muongo. Hivi hawa maadui j Makamba aliwatengeneza yeye au matokeo ya njia alizopitia!
 
Unajua hizi takwimu huwa zinaandaliwa na 'wataalamu' huko chini, kama zinamapungufu makubwa namna hii ni wazi kuwa 'wataalamu' wa hiyo wizara wanashida. Wao ndio wapika takwimu na mwisho wa siku wanamtesa waziri wao kwa uongo wao.

Kalemani alikuwa anajua sana upuuzi wa 'wataalamu' wetu, bila mshikeshike na purukushani mambo hayaendi. Kuna siku 'wataalamu' wa TANESCO waliamua kufanya scheduled maintenance ya power plants kadhaa kwa mpigo! Nchi ikajikuta ipo kwenye mgao wa umeme. Kalemani aliweza kung'amua kuwa walifanya maamuzi ya kipumbavu, akawashukia kama mwewe na adhabu zikatolewa kwa wazembe.

Swali ni je, Januari Makamba anao uwezo wa kung'amua uongo na takwimu za kupikwa kutoka kwa 'wataalamu' wake akina Maharage na wenzao?? Au ndio analazimika kukubaliana nao tu?
 
Nawaza ela ya kununua mitungi when was it budgeted maana si chini ya bilion kwa wabunge zaidi ya 300
Hapa kuna mashaka na ndio mana wanasema kuna walakini,atueleze hizo pesa zimetoka wapi unajua mtu akiwa mpigaji upigaji unakuwa kwenye damu
 
Mpeni muda j Makamba anayo nia ya dhati kusimamia kuungwa Kwa umeme vijiji vyote nchini hilo suala la hesabu kumpiga chenga isiwe sababu ya kuonekana muongo. Hivi hawa maadui j Makamba aliwatengeneza yeye au matokeo ya njia alizopitia!
Hiyo taarifa kabla haijasomwa bungeni huwa anakua kishaipitia, Kama ameshindwa kuona hizo dosari vipi kwenye mikataba mikubwa?
 
Hii Nchi ni ya wajinga sana, kuna Makamba, Nape na Mwigulu, wamepewa wizara ambazo wao wenyewe hawajui wafanye nini, yaani wanaongea na kuwakilisha vitu ambavyo wao wenyewe hawa vijui, wamelishwa ujinga wa kuwa wao ni ceremonial tu katika wizara zao, kuchukua karatasi na kusoma basi.
 
Back
Top Bottom