January Makamba kiongozi mwenye uzalendo licha ya kuwepo CCM

hizo nyumba zenyewe mnajua zilipo?mngesimamia kwanza mpango miji nyumba zipangwe vizuri na viwanja vipangwwe ndio muanzi=e kula kodi ila mmelala sasa kwenye slums utamdai nani kodi ya nyumba?
 
Binafsi sio mungaji mkono wa *******,lakini pia ni mpinzani mkubwa sana wa siasa za kishabiki!Napenda sana kwa moyo mweupe kabisa nimpongeze January Makamba mbunge wa bumbuli kwa hoja yakebinafsi ya kuitaka serikari itunge sheria ya kuwadhibiti wenye nyumba ili wasiwe wanapandisha bei za kupanga kiholela na pia kuwadhibiti wenye nyumba hao kuwalazimisha wapangaji kulipa kodi za muda mrefu.

Kiukweli hili ni eneo muhimu sana kwa sababu linahusisha watanzania wengi na linahusisha makazi kitu ambacho ni muhimu sana na cha msingi sana kwa Watanzania, nawapongeza pia kambi ya upinzani kwa kuunga mkono hoja hiyo kwani wamedhirisha kuwa hawapo kichama bali kimaslahi ya Watanzania walio wengi,hawakuangalia ni chama gani kimetoa hoja bali hoja yenyewe,Hongereni sana!

Jukumu ni la serikali kuharakisha kuandaa sera itakayo wezesha sheria kutungwa!BRAVO JANUARY!

Makamba ni mnafki mbona haongelei NHC kuwadhalilisha wapangaji? Issue ya upangaji iahitaji mjadala na si ushabiki kwani ni sawa na serikali kuwapangia shule na vyuo vya binafsi ada wakati haiwasaidii kwa lolote. Mfano ukiingiza kodi kwenye upanga ndio gharama zitapanda kwani mwenye nyumba anahitaji faida. Hebu angalia kwenye Petroli serikali imeongeza kodi na kupaisha bei ya mafuta.
 
Nami nampongeza makamba kwa hoja yake nzuri. Lakini kama prof Tiba alivyoeleza haya mambo sio ya kukurupuka. Kutunga sheria ni rahisi . hata leo tunaweza kuitunga na kuipitisha kama tunataka. Ila sasa tukikurupa tutakwisha. Kuna mambo mengi inabidi yawekwe sawa ndio sheria ije . Kwa mfano nyumba za kupanga ni chache ukija na sheria yako yenye ufinyu ya kuwabana wenye nyumba haitafanya kazi. kwa mfano, Sheria itakayowabana wenye nyumba inaweza kupelekea wakabadili matumizi ya nyumba zao na kuzifanya gesti hata mabanda ya kufugia kuku? . Ikitokea hivi wapangaji watakimbilia wapi? wakati nyumba zenyewe ni chache. nami pia ni mpangaji lakini tabia ya wapangaji wengi wanajefeel" inferior" kwa kujiona wananyanyaswa. Wengi wanalia lia . Nyumba za bina binafsi sio NHC. Huwezi kulilia kwa nyumba private. Hujui mwekezaji amewekeza kiasi.gani. Sio charity hiyo. Nampongeza professor kwa kuliona ilo. Professor ana mtizamo mpana. Wazungu wanauita " holistic view" Narudia tena tukikurupa kwenye hili watakaomia ni hao hao wanaolilia kwamba wananyanyaswa na wenye nyumba. Biashara ya nyumba iachwe indelee kua soko huria. NHC wawekeze ili kuleta ushindani kwa private. HAta NHC ikiwekeza bado mtizamo ni wa kibiashara kwani NHC inawekeza kwa kushirikiana na wabia. Tujitahidi kufanya kazi kwa bidii. Na haina haja mshahara wako ni laki kwa mwezi wewe unataka kuishi oystabay kodi mili moja na unataka ulipe kwa mkopo. Nani atakubali ****** huo. Kuna sehemu nyingine bei za pango nzuri.

NAWAKILISHA
 
Ingekuja ni hoja ya kuitaka serikali ijengee raia wake nyumba kama serikali zingine huko duniani zinavyofanya ningemuona wa maana. Haya tusubiri tuone kama ataibuka na hoja ya bei ya mchicha na nyama ...
 
Hoja ya Mh. January Makamba kuhusu serikali kuthibiti wenye nyumba kukusanya kodi ya pango ya mwaka mzima ni ya kuunga mkono kama ukiliangalia suala lenyewe katika mtazamo finyu (narrow-perception). Tatizo hapa si wenye nyumba! Nafafanua! Kwa miaka mingi hapa nchini suala la nyumba limekuwa halipewi kipaumbele na wachumi wetu wanapopanga au kuandaa sera za maendeleo za taifa! Ndio maana Prof. Tibaijuka (Mchumi) ameamua kuandika kitabu cha HOUSING in ECONOMICS, akiamini kwamba wachumi hawalichukulii suala la housing kama linachangia maendeleo ya taifa!

"
This book is a much-needed account, with numerous detailed examples, of the role of housing in economic growth and development by an author in a unique position to understand its importance and the practical measures for delivering that growth. While the linkages between housing and the macroeconomic environment in developed countries has been studied, the case of developing and transitional countries has been mostly overlooked. The author establishes these linkages with great clarity, supported by detailed case studies chosen to reflect regional diversity as well as differences in socio-economic development and political systems. On the basis of this analysis, the author goes on to develop specific policies and practices to enable governments to enhance the contribution of housing in economic growth."


Ni katika hili ndio maana sheria za mortgage haziko friendly kwa mkopaji, viwango vya riba ni vikubwa sana kwa mkopaji kuweza naye kununua na kumiliki nyumba! Benk nyingi zinafanya biashara na serikali na kupata riba nono (risk free), na ndio maana zinakuwa na kiburi kufanya biashara na Hii inafanya wanaomiliki nyumba wawe wachache, na wapangaji kuwa wengi!

Karibu zaidi ya 70% kwa DSM ni unplanned, na hivyo maeneo machache yaliyopimwa na kupewa hati, bei za viwanja ama nyumba ziko juu! Hili nalo linafanya wamiliki (Landlords & Landladies) kuwa wachache na wapangaji(Tenants) kuwa wengi!

Tukirudi kwenye hoja ya Mh. Makamba, ni dhahiri kwamba demand ya housing DSM na mikoa mingine ni kubwa kuliko supply ya nyumba! Utakuta zaidi ya watu watano wanagombania kupanga nyumba moja, na mwingine yuko tayari kulipa hata kodi ya miaka miwili, nini kodi ya mwaka?

Tuelewe kwamba hakuna sheria inayowapa nguvu wenye nyumba walipwe kodi ya mwaka, hapa ni suala la soko, MARKET FORCES OPERATION! Serikali inabidi kujipanga zaidi katika hili kwani hata ikipitisha sheria bado utekelezaji wake utakuwa hafifu just like EWURA, waulize mkoani bei ya lita moja ya petrol au diesel, ni bei elekezi? Nawasilisha!
 
kwa namna anavyoendesha siasa nadhani sio mtoto wa makamba. Makamba kasingiziwa tu
 
dogo yuko vizuri tatizo ni chama alichonacho,hata aseme kitu kizuri vipi anaonekana mzushi tu vijana wengi tuna alleg na chama chake.
 
Mh.January Makamba yupo ktk kipindi cha Jahazi-clouds Fm,akizungumzia sheria ya Pango na haki za mpangaji na mwenye nyumba!...zaidi tune Clouds fm upate habari!Jamaa kajipanga sana kwa hoja na haki za wapangaji!
 
Mh.January Makamba yupo ktk kipindi cha Jahazi-clouds Fm,akizungumzia sheria ya Pango na haki za mpangaji na mwenye nyumba!...zaidi tune Clouds fm upate habari!Jamaa kajipanga sana kwa hoja na haki za wapangaji!

Kama ukifanikiwa kupiga simu muulize kama Posho atachukua au lah!
 
JAna nilikipenda sana kipindi cha Jahazi wakati wakijadiliana na Zitoo bila shaka na kijana Makamba naye atafunika. All the best Makamba.
 
***** MTUPU,redio hiyo ***** na mtoa maada mwenyewe (J. Makamba) naye ni ***** maana kaidandia hoja asiyoilewa vyema. Hiyo hoja ya nyumba na makazi ni hoja ya CHADEMA,ipo kwenye ilani za Uchaguzi za Chadema za miaka ya 2005 na 2010. Bwanamdogo huyu anadandia gari kwa mbele!!
 
Tunashukuru kwa taarifa nimeketi namsikiliza issue za makazi ni nyeti kama tutaweka ushabiki wetu wa kisiasa pembeni!

 
hawooooooo mawingu ni waseeeeeee.................. sana peleka hiiiiiii topic FB na ucludie tena etii jivanaaaaaaa wa luuuuuuuugeeeee............. kama wana ubavu wamwite jembe sugu na vinega:embarassed2::embarassed2::embarassed2::embarassed2::embarassed2::embarassed2::embarassed2::embarassed2:
 
Back
Top Bottom