January Makamba kiongozi mwenye uzalendo licha ya kuwepo CCM

Anaongea point nzuri. TZ ni moja ya nchi chache sana duniani ambayo haina sheria ya mortgage.Inaleta wizi sana kujenga nyumba kwa pesa taslimu. Pia wananchi wanachukua muda sana kumaliza ujenzi wa makazi yao, wakipata mikopo, riba ni kubwa sana na wanatakiwa kulipa kwa muda mchache sana.Lakini ukimsikiliza kwa makini bado ni walewale CCM kama anavyosemaga MWANAKIJIJI, eti ansema "nasubiri waziri alete muswada bungeni", hajui kazi yake ni nini.
 
Du ila huwa wajinga wengi sana.jamani mpishe watu wenye hoja humu.mbona mnaweza kwenda kwenye kumbi za taarabu mkalumbane huku.nchi haina hata sera ya nyumba.tumekalia ushabiki tu
 
Mh.January Makamba yupo ktk kipindi cha Jahazi-clouds Fm,akizungumzia sheria ya Pango na haki za mpangaji na mwenye nyumba!...zaidi tune Clouds fm upate habari!Jamaa kajipanga sana kwa hoja na haki za wapangaji!


Zitto K, January ni wabunge makini sana their political future looks bright
 
Suala upangaji linaigusa jamii kwa asilimia kubwa sana na kwa kweli huu mjadala kama itakuwa sheria basi itasaidia watu wengi sana. Hachana na hao kula kulala wasio jua maisha nini. Jana nilimsikia mh Zito Kupitia Kipindi hicho hicho akisifia wabunge vijana kuwa wanaopeo wakushughulikia matatizo ya kijamii, sasa huyo BWAKUBWAKU analeta ushabiki wa kisiasa anakusumbua nini?
 
Zitto K, January ni wabunge makini sana their political future looks bright

Jana Pasco alituhabarisha kwamba Zitto alikuwa anaongea Jahazi clouds FM, leo naona ni zamu ya January! Bungeni nako zamu hii both January na Zitto walikuja na hoja binafsi na zote zikapigwa chini! Naona kama wanasoma kwenye ukarasa mmoja hawa vojana na hapo mbeleni watatuambia 'hatukukutana barabarani'.
 
Nakumbuka katika Bunge lililopita Mh.January Makamba kabla ya kuchaguliwa kuwa Naibu waziri aliwahi kusema kuwa atapeleka hoja binafsi kuhusiana na wapangaji wa nyumba kulipa au kulazimishwa kulipa kodi za nyumba kwa miezi sita au mwaka mzima na wenye nyumba.Kitendo hiki kilionekana au kutafsiriwa kuwa ni uonevu kwa wapangaji wa nyumba kwa mujibu wa Mh.January Makamba kutokana na hali ya kiuchumi kwa wananchi.Sasa je, kwa sasa amechaguliwa kuwa Naibu waziri anaweza kuwasilisha hoja hii au ndiyo kafungwa mdomo?
 
Bunge letu tunaliendesha kwa mtindo wa Wenstiminster Style kama bunge la Uingereza ambapo nchi ina mihimili 3 inayojotegemea. The executive, (serikali), the judiciary (mahakama) na the legisleture (bunge). Mihimili hii yote mitatu inaangaliana kwa kufanya checks and balance kuzuia mhimili mmoja usipitilize mipaka katika utaratibu unaojulikana kama " the doctrine of separation of powers".

Mbunge akiwa mbunge yeye ni mtunga sheria kwa niaba ya wananchi, lakini akishachaguliwa kuwa waziri ina maana mbunge huyo sasa ame cross the line kutoka mhimili mmoja wa kutunga sheria na kuingia mhimili mwingine wa kutawala, yaani serikali.

Hivyo sasa Mh. January sasa ni sehemu ya serikali hawezi tena kuwasilisha hoja bungeni kuitaka serikali itunge sheria fulani bali sasa hoja yake ataiwasilisha serikalini moja kwa moja.

Kana umenote utaona mawaziri huwa hawaulizi swali lolote bungeni kutoka kwa wananchi wao, hii haina maana wananchi wa majimbo ya mawaziri, hawana maswali, no, wanayo maswali wanayapeleka direct na yanapatiwa majibu direct kwa utekelezaji ndio maana hutokea kilio cha upendeleo kwa majimbo ya mawaziri!.
 
Huyo si mtoto wa CCm alikuwa magogoni siku nyingi kwa hiyo anajua jinsi ya kupata uwaziri katika serikali( mfano Nape na ccj mpaka ukuu wa wilaya) JM from magogoni- ubunge - kamati ya nishati- naibu waziri''''...... mliotoka kwa kayumba mtabaki kujadili tu.
 
Nakumbuka katika Bunge lililopita Mh.January Makamba kabla ya kuchaguliwa kuwa Naibu waziri aliwahi kusema kuwa atapeleka hoja binafsi kuhusiana na wapangaji wa nyumba kulipa au kulazimishwa kulipa kodi za nyumba kwa miezi sita au mwaka mzima na wenye nyumba.Kitendo hiki kilionekana au kutafsiriwa kuwa ni uonevu kwa wapangaji wa nyumba kwa mujibu wa Mh.January Makamba kutokana na hali ya kiuchumi kwa wananchi.Sasa je, kwa sasa amechaguliwa kuwa Naibu waziri anaweza kuwasilisha hoja hii au ndiyo kafungwa mdomo?
Kama bado anaamini katika hoja hiyo anaweza kuipeleka. kama anaona noma kuwa yeye sasa ni sehemu ya serikali, anaweza kumpatia mbunge mwingine ili aiwasilishe
 
Kutoa hoja si suluhisho, suluhisho ni kupima viwanja vingi kuondoa makazi duni, kuimarisha usafiri kwenye majiji, na kufanya kila mwanachi kumiliki nyumba kwa kutumia pension inayokaa tu kenye pension funds.
 
January Makamba? UCCM? Uzalendo? No, no, no, that's impossible, uzalendo na UCCM ni kama maji na mafuta, hayachanganyiki kirahisi hivyo!

images


You cant eat your cake and still have it!


 
wee basi utakuwa na tatizo unaangalia chama huangalii mazuri ya mtu inamaana hata mafisadi wote walioko ccm wakiamia cdm utaendelea kuipenda cdm kisa unapenda chama huangalii sifa za wanachama
 
Back
Top Bottom