Eng. Mitambo: Fedha za umma zinapotea kwa ucheleweshwaji wa miradi ya Ujenzi

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
602
1,526
MTAMBO KUHUSU HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23.

Utangulizi
Katika mwendelezo wa uwasilishaji, mijadala na upitishwaji wa bajeti Bungeni, jana tarehe 23 Mei 2022, Prof. Makame Mnyaa Mbarawa (Mb), aliwasilisha hotuba ya utekelezaji wa bajeti kwa mwaka uliopita na mpango na makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2022/23. Katika mwaka wa fedha 2022/23, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi imeomba kuidhinishiwa jumla ya Shilingi trilioni 3.86 (3,866,616,675,800.00) kati ya fedha hizo, Shilingi trilioni 1.465 (1,465,835,235,800.00) ni kwa ajili ya Sekta ya Ujenzi na Shilingi Trilioni 2.4 (2,400,781,440,000.00) ni kwa ajili ya Sekta ya Uchukuzi.

Kutokana na majukumu ya Wizara katika kusimamia masuala ya ujenzi, utengenezaji na ukarabati wa miundombinu ya reli, barabara, bahari, maziwa na anga. Aidha wajibu wa kusimamia na kudhibiti huduma za uchukuzi na usafirishaji nchini na kusimamia taasisi zenye lengo kuhakikisha sekta ya Ujenzi na uchukuzi inachangia katika kusukuma maendeleo ya wanajamii na nchi kwa ujumla, hivyo mara zote tumeshuhudia wananchi na wadau wengine wakifuatilia kwa karibu sana bajeti ya wizara hii ili kuona kama inaweza kwenda kujibu vilio vyao vya muda mrefu.

Hivyo basi, katika kuchangia mjadala wa bajeti hii muhimu na kutimiza wajibu wa kuisimamia na kuiwajibisha Serikali, Sisi ACT Wazalendo kupitia Msemaji wa Sekta ya Miundombinu ya Ujenzi, Reli na Barabara Eng. Mohammed Mtambo tumefuatilia hotuba na kuichambua ili kuona kwa kiasi gani imeweza kubeba matarajio na matamanio ya wadau na wananchi kwa ujumla wake. Katika hotuba hii, tumeonyesha hoja saba (7) kuhusu vipaumbele, utekelezaji wa bajeti na mpango wa makadirio ya mapato na matumizi kutoka kwenye hotuba ya bajeti ya wizara kwa mwaka wa fedha 2022/23.

Hoja saba (7) za ACT Wazalendo kuhusu Hotuba ya Bajeti ya Wizara Ujenzi na Uchukuzi.

1. Uchakavu wa miundombinu ya barabara na reli:

Uchakavu, ubovu na uharibifu wa miundombinu ya reli na barabara imekuwa ni changamoto kubwa sana hata kutishia usalama wa matumizi ya miundombinu hiyo. Mifano inayotolewa na wizara juu ya uchakavu wa miundombinu ya njia ya reli iliyopo katika vipande vya Isaka- Mwanza, Tabora Kigoma, Kaliua - Mpanda na Ruvu Junction - Mruazi, Tanga - Arusha; kutokana na miundombinu hii kujengwa muda mrefu ni jambo linapaswa kuishtua Serikali na kuwekeza fedha za kutosha ili kufanya matengenezo, ukarabati na uboreshaji.

Mtandao wa barabara zinazosimamiwa na Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) una urefu wa kilometa 89,204. Mtandao huo unajumuisha, kilometa 12,176 za barabara kuu zinazounganisha mikoa na nchi jirani, kilometa 24,082 barabara za mikoa zinazounganisha wilaya na miji mikuu na kilometa 52,946 barabara za wilaya zinazounganisha wilaya, kata na vijiji.

Katika bajeti ya mwaka huu Serikali imetenga fedha kiasi cha Shilingi Bilioni 523.4 kwa ajili ya matengenezo na madeni ya wakandarasi, kiasi hiki ni hakiwezi kutosheleza hata kulipa tu madeni ya wadai ambao ni wastani wa kiasi cha Shilingi bilioni 651.9. Aidha, kwa upande wa Barabara, Serikali inakiri kuwa uwezo wa Serikali kupitia Mfuko wa Barabara, una uwezo mdogo wa kukidhi mahitaji ya matengenezo ya barabara. Kwa sasa mfuko una uwezo wa kugharamia asilimia 42 tu ya mahitaji halisi ya matengenezo ya barabara Tanzania Bara.

ACT Wazalendo tunaitaka Serikali kuja na vyanzo endelevu na vya uhakika kwa ajili Mfuko wa Barabara kuliko kutengemea mafungu ya kawaida ya bajeti.

2. Madeni na utendaji mbovu wa Wakala wa Ujenzi (TBA):

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ni wakala wa Serikali chini ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Ujenzi). Lengo kuu la TBA ni kutoa makazi bora kwa Serikali na watumishi pamoja na kutoa ushauri katika masuala ya Ujenzi kwa Serikali. Wakala wa Ujenzi wa nyumba za watumishi wa umma na majengo ya ofisi za Serikali umekabiliwa na changamoto zisizopatiwa ufumbuzi wa kudumu kila uchao. Wakala inakabiliwa na malimbikizo ya madai/madeni zinazoidai Serikali kupitia idara, taasisi na watumishi wa serikali kutokana na huduma walizopokea kutokana na ushauri, Ujenzi, kupangisha nyumba na mauzo.

Kwa mujibu wa ripoti ya CAG 2020/21, Wakala iliingia mikataba 199 na Taasisi mbalimbali za Serikali ili kutoa makazi kwa watumishi wa umma wa Taasisi husika ambapo Taasisi zinatakiwa kuilipa TBA kodi ya kila mwezi kama ilivyoainishwa kwenye mkataba wa upangaji Serikali inadaiwa na wakala kiasi cha Shilingi Bilioni 4.76, kutolipwa kwa madeni haya, kunaipunguzia uwezo TBA na hatimaye kuwa na ufanisi mdogo.

Aidha, kasi ndogo ya ujenzi wa nyumba kwa miaka, miwili mfululizo imeweza kujenga nyumba chache tofauti na malengo pamoja na kasi ya mahitaji. Hii inathibishwa, kwa mujibu wa ripoti ya CAG, anasema “nilibaini kuwa kati ya mpango wa uwekezaji wa ujenzi wa nyumba 851, TBA iliweza kujenga nyumba 219 tu (awamu ya kwanza na ya pili), na kuacha nyumba 632 hazijajengwa hadi muda wa ukaguzi, Januari 2022. Pia, nilibaini kuwa TBA tayari imetumia Sh. 18,835,068,187.69 (asilimia 82) .kutoka katika fedha zilizokopwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba.”

Kukosekana kwa uwezo wa kifedha, kumepunguza ufanisi wa wakala kiasi cha kusitishiwa mikataba na mwajiri. Kitendo cha kusitishiwa mikataba kimepelekea Serikali kupata hasara ya Shilingi. Bilioni 6.30 ziliosaniwa kati wakala na Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo (mwajiri) kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo tangu mwaka 2018.

ACT Wazalendo tunaitaka Serikali, na kwa kuwa jambo hili limelalamikiwa kwa muda mrefu ni wakati sasa wa kufanya tathmini ya utendaji wa Wakala wa majengo ili iweze kudai madeni yake yote.

3. Utekelezaji wa miradi ya Barabara kwenye maeneo ya pembezoni, unasuasua:

Utekelezaji wa miradi ya Barabara imekuwa ikichukuwa muda mrefu kwa ujumla wake. Lakini kwa upande wa Barabara zinazoonekana na pembezoni ni changamoto zaidi. Katika miradi ambayo imetengewa fungu dogo zaidi ni kama miradi ifuatayo:

Barabara ya Soni - Bumbuli - Dindira – Korogwe (km 74)- umetengewa bilioni 1.0, kiwango kilichotengwa kwa ajili ya kulipia madeni ya makandarasi, hata hivyo kwa wastani wa kawaida kiasi hiki kitaweza kujenga kilomita zisizozidi mbili.

 Barabara ya Mtwara – Newala - Masasi (km 210)- umetengewa bilioni 11.01

 Barabara ya Likuyufusi – Mkenda (km 122.50) bilioni 7.5

 Barabara ya Nachingwea – Liwale (km 130) milioni 500
 Nanguruku- Liwale (km 210) milioni 500
Licha ya kuwa na umuhimu wa barabara hizi, kasi upangaji, ugawaji na uidhinishwaji wa fedha kuelekea kwenye miradi hii hairidhishi .

ACT Wazalendo inaitaka Serikali iongeze umakini na kujali mahitaji ya wananchi wa maeneo haya ambao hawana usafiri wa uhakika kwa muda mrefu tangu nchi hii imepata uhuru.

4. Fedha za umma zinapotea kwa ucheleweshwaji wa miradi ya Ujenzi:

Hali ya utekelezaji wa miradi mbalimbali inayoanzishwa na Serikali mara nyingi huchukua muda mrefu kukamilika kinyume na mikataba iliyoingiwa na wakandarasi. Moja ya sababu za ucheleweshwaji ni Serikali kutenga fedha kiduchu kwa ajili ya miradi tofauti na mahitaji halisi; na pili, wizara kutopewa au kutotoa fedha zilizoidhinishwa kwa wakati kwa ajili miradi mbalimbali. Fedha za umma zinatekezwa kwa ajili ya kulipia fidia (riba) kwa wakandarasi kutokana na ucheleweshwaji huo. Kutokana na Mwenendo huu Serikali kwa mwaka wa fedha 2020/21 na 202122 imesababisha hasara ya Shilingi bilioni 4.79 kwa ajili ya kuwalipa wakandarasi kwenye miradi sita (6).

Kwa mujibu wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) mwaka 2020/21 kuna Malimbikizo ya riba kutokana na ucheleweshaji wa kuwalipa Wakandarasi katika Miradi ya Ujenzi wa Barabara Sh. Bilioni 4.79. Miradi iliyobainishwa na CAG ni;

 Programu ya Usaidizi wa Sekta ya Uchukuzi (TSSP) yenye tozo za riba kiasi cha Sh. Bilioni 1.39
 Mradi wa Uwezeshaji Biashara na Uchukuzi Kusini mwa Afrika (SATTFP), Sh. Milioni 511.71
 Arusha Holili, Sh. Bilioni 2.21
 Programu ya Uboreshaji wa Miundombinu ya Usafirishaji Jijini Dar es Salaam (DUTP), Sh. Milioni 349.87
 Mradi wa Multinational Rumonge-Gitaza-Kibondo-Kasulu-Manyovu, Sh. Milioni 329,082,934.76
Aidha, kuna ucheleweshwaji katika Mradi wa mkakati wa Ujenzi wa reli ya kisasa, Ujenzi wa awamu ya kwanza kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro kilitakiwa kukamilika tangu mwezi Novemba 2019 lakini hadi sasa umefikia asilimia 96.5 kwa mujibu hotuba ya wizara. Wakati kipande cha Morogoro hadi Dodoma (Makutupora) kilipaswa kukamilika mnamo February 2022, kwani hadi sasa umefikia asilimia 85.

Vilevile, kuongezeka kwa gharama za miradi Kwa sababu ya kuchelewa kulipwa kwa fidia. CAG katika ripoti ya mwaka 2020/21 anabainisha kuwa kuna ongezeko la gharama za mradi kwa Kiasi cha Sh. Bilioni 22.35 kutokana na Kaya 1,125 zilizoathiriwa na Mradi kutolipwa fidia kwa zaidi ya Miaka 23 kwenye kiwanja cha ndege cha Mwalimu Julius Kmabarage Nyerere (JNIA).

ACT Wazalendo tunaitaka Serikali kutenga bajeti inayotosha ili kuepusha malimbikizo ya madeni kutoka kwa wazabuni na wakandarasi.

5. Msongamano katika Bandari ya Dar es Salaam:

Kwa muda mrefu pamekuwa na malalamiko yasiyoisha ya kuwepo kwa msongamano wa magari unaopelekea kuwepo kwa muda mrefu wa kusubiri kupakia au kupakua mizigo. Ucheleweshwaji unaosababisha haya na uwezo wa bandari kumudu mahitaji hayo, unapaswa kufanyiwa kazi kwa haraka. Hususan katika kipindi hiki ambapo gharama za vitu vimekuwa juu.

Gharama zinazoweza kuokolewa kwa kuboresha utendaji na uwezo wa bandari zitaenda kuwasaidia wananchi kupata huduma kwa bei ya chini kuliko hivi sasa. Katika hotuba ya mwaka jana Waziri wa Ujenzi na uchukuzi Prof. Makame Mbarawa alitaja kufanya maboresho ya GAT na. 7 & 8 kulijenga, Lakini katika hali ya utekelezaji bado halikamilika, ahadi imejirudia tena kwa mwaka na kutegewa fedha kiasi cha shilingi Bilioni 7.

Sisi, ACT Wazalendo tuna mapendekezo yafutayo ili kukabiliana na changamoto za msongamano katika Bandari ya Dar es Salaam:

I. Wadau wote wa bandari waunganishwe kwenye mfumo wa kielektroniki unaotumiwa na bandari ili kuweza kuharakisha uondoshwaji wa mizigo bandarini kwani wakati mwingine mizigo inachelewa kutokana na wadau wengine kama Mkemia mkuu, Shirika la Viwango Tanzania-(TBS), Wizara ya Nishati na Wizara ya Madini na wengine wengi kutokuwemo kwenye mfumo huo;

II. Mchakato wa kuwa na eneo Kurasini-Shimo la Udongo ambalo litatumika kuegesha magari yanayoingiza na kutoa mizigo bandarini sasa ufanyike kwa haraka ili eneo hilo lipatikane kwani mojawapo ya kero za wafanyabishara wanaotumia Bandari ya Dar es Salaam ni kutokuwa na maegesho jambo ambalo husababisha usumbufu na gharama zisizotabirika;

III. Serikali kuharakisha ujenzi wa bandari za nchi kavu ili kupunguza gharama kwa wateja kusafiri mpaka Dar se salaam kwa ajili ya kutoa mizigo. Ni muda sasa tangu Serikali imeanza mipango ya kujenga bandari kavu katika maeneo ya Kwala -Pwani, Ihumwa -Dodoma, Katosho-Kigoma na Misungwi –Mwanza;

IV. Kuimarisha na kuboresha bandari ya Tanga, Lindi na Mtwara ili kupunguza msongamano.

6. Kupanda kwa gharama za nauli na usafirishaji wa bidhaa/mizigo:

Wiki kadhaa zilizopita Mamlaka ya udhibiti wa usafiri Ardhini (Latra) ilitangaza nauli mpya za mabasi ya masafa marefu (yaendayo mikoani) na daladala (mabasi ya mijini) ambazo zimeonyesha kupanda kwa ongezeko la asilimia 11 kutoka sh. 36 kwa kilomita moja hadi sh. 41 kwa daraja la kawaida na daraja la kati limepanda kwa asilimia 6 kutoka kilomita 53 hadi 56. Hali iliyofanya kupanda kwa gharama za usafiri na usafirishaji kwa ujumla wake. Upandishwaji wa gharama za nauli umefanywa bila kuzingatia kuwa kwa sehemu kubwa, gharama za ukomo wa nauli zilizowekwa awali kabla ya Ongezeko la bei za mafuta kwa maeneo mengi haikuweza kufikiwa na watoa huduma.

Kwa hiyo, kukubali kwa shinikizo hilo kuna waumiza zaidi wananchi.

Aidha, kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta, imeongeza gharama za usafirishaji wa vifurushi na mizigo. Katika hotuba ya mipango na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka huu haijazingatia kabisa hali hii na kuona namna bora ya kukabiliana na changamoto zote.

7. Kuongezeka kwa ajali za barabarani:

Kwa kuwa Wizara inaratibu shughuli za usalama barabarani, mazingira na kudhibiti uzito wa magari yanayotumia Barabara zetu, viwango na ubora wa magari.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, taarifa zinaonesha jumla ya matukio makubwa na madogo ya jinai 583,245 yaliyoripotiwa katika kipindi cha Januari hadi Desemba, 2020.

Katika kipindi cha Januari hadi Desemba, 2020, matukio makubwa ya jinai yalikuwa 50,689 na matukio madogo ya jinai yalikuwa 532,556 katika kipindi cha Januari hadi Desemba, 2020. Matukio makubwa yanajumuisha ajali zinazopelekea vifo na majeruhi (mahututi).

Kuongezeka kwa matukio haya, kuishtue Serikali kuona namna bora ya kukabiliana nayo ili tusiendelee kupoteza nguvu kazi wakati upo uwezekano wa kupunguzwa kwabisa.

Pia, tunaishauri Serikali kupunguza ukubwa na idadi ya matuta katika Barabara kuu hadi kwa kiwango kinachoweza kukubalika kitaalamu.

Hitimisho.
Sekta ya miundombinu kwa kiwango kikubwa imekuwa ikichukua fedha nyingi kwenye bajeti ya Serikali kuu na hata mgao wa pato la taifa. Na ukitazamwa mnyororo wa thamani wa sekta hii ni sehemu kubwa ya fedha hizo zinachukuliwa na makampuni makubwa kutoka nje ni kwa kuwa makampuni mengi yanayojihusisha na uwekezaji wa miundombinu hiyo ni kutoka nje, sehemu kubwa ya fedha za umma zinasafirishwa nje.

Aidha, ufinyu wa bajeti katika wizara hii unapelekea ucheleweshaji wa utekelezaji wa bajeti na kuzalisha malimbikizo ya madini yanayongeza gharama za miradi.

Imetolewa na:
Eng. Mohammed Mtambo,
Msemaji wa Sekta ya Miundombinu ya Ujenzi, Barabara na Reli,
ACT Wazalendo.

24 Mei, 2022.
 
Huwa hamueleweki mnasimamia nn nyinyi wafuasi wa hayatolah

USSR
 
NGOGWE nazo zinalalamika, wakati nazo ni sehemu ya Serikali!
 
Waulize ile bandari kavu ya Kigoma, itaisha lini ili ianze kutumika?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom