January Makamba kiongozi mwenye uzalendo licha ya kuwepo CCM

Kuna watu wanataka tuamini kila jambo la kizalendo linafanywa na cdm. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.

sure,ni ukweli usiojificha kuwa cdm inaongoza kwa viongoz wazalendo lakini ata ccm kuna watu wazalendo.hakika mnyonge mnyongeni haki yake mpeni
 
hiyo kodi anayolilia itazidi kupandisha bei ya pango. kwani ukiweka kodi kwenye bucha au soko la samaki effect yake itakuwa ni nini kama siyo kuongeza ugumu wa maisha
 
asije sababisha bei ya nyumba (pango) zipande zaidi. maana kodi hiyo itahamia kwa mpangaji (na mwisho wa siku bei kwenye soko huria hupangwa na mwenye mali, iwe bei ya nguo, samaki, maziwa, kiberiti, nyumba, nk. ni hivyo hivyo).
 
Issue ya upangaji umeona ni jambo la kitoto?! Basi we utakuwa unakaa kwenye nyumba yenu urithi
Hachana nae mtoto wa mama huyo,hajui watu tunavyosulubishwa na wenye nyumba kwa sababu ya sheria zetu legelege
 
Mh January makamba anahoja nzuri sana hasa kwa watoto wa wakulima wanaotafuta riziki kwa jasho lao.sioni ubaya, namuunga mkono ,anajenga hoja na anasimamia hoja zake vema. Big up never go back
 
Tangu zamani tulikuwa na sheria ya upangaji wa kodi za nyumba lakini baada ya hawa wakubwa kuwa na nyumba nyingi za kupangisha ndipo wakaifuta sheria hiyo

sheria hiyo iliitwa Rent Restriction Act, 1984, kilikuwepo chombo kilichokuwa kinapokea maombi ya mmiliki wa nyumba kuelezea mapendekezo ya kodi atakayotoza katika nyumba yake anayotaka kupangisha. Hivyo kodi ilitegemea na thamani ya nyumba husika; na mwenye nyumba alikuwa hawezi kupandisha kodi bila kibali cha mamlaka hayo. lakini nadhani viongozi wetu walipokuwa na nyumba nyingi za kupangisha waliifuta Sheria hiyo na kuleta Sheria ya mabaraza ya ardhi na nyumba ambayo kwa sehemu kubwa yanasaidia kuwabana wapangaji kulipa kodi au kuwatoa wapangaji katika nyumba n.k.

hivyo sio kwamba makamba hajui bali anajua na anataka kujaribu kutafuta credit kwa serikali iliyopoteza credit kwa wananchi, haya ngoja tusubiri ila nadhani asipoangalia atapoteza ubunge wake kabla au wakati wa uchaguzi wa 2015

yetu macho, kwani wamezoea kutuhadaa ili c-c-m wajue wakati ni ukuta huwezi kushindana nao kwani wakati ukifika wataumia wao
 
Soma hapa uelewe vizuri hoja yake DailyNews Online Edition - Makamba to table motion on Rental Housing Act

ni mjaja! anatumiwa/anajituma kukwepesha hoja za msingi kwa kuibua mambo ambayo si ya haraka, ili macho na masikio yaelekezwe kwenye hoja hii, wasaahu hoja muhimu, kama vile, ongezeko la bei ya umeme kufidia fedha inayochotwa na mafisadi, sheria feki ya katiba mpya, sula la jairo, migogoro ya wafanyakazi, ma-dr, issues mbalimbali za kifisadi n.k

Simuamini sitamuamini hata siku moja... si kwa sababu ni mtoto wa fisadi, bali nashindwsa kumtenganisha na anaofanyakazi, kushinda na kukaanao vikao, atakuwaje mweupe wakati yumo ndani ya waliooza! haiwezekani
 
January Makamba mmoja ya wabunge vijana wanaonivutia sana kwa hoja, binafsi huwa namkubali sana.Hang loose but on focus.
 
Kuna mambo makubwa zaidi yanayohitaji kusimamiwa na mtu akaonekana makini na sio nyumba...ufisadi unaoendelea serikalini ni moja ya maeneo muhimu...kinachoendelea mtaani au kwa wananchi kinahakisi kinachoendelea kwa watawala wetu.

Mkuu Only83,
Umesema point kubwa sana ingawa unarushwa.
Watu wajiulize kwa nini hakujawahi tokea mbunge aka-table private motion kutokomeza ufisadi?
Rushwa serikalini ndio root cause ya all evil.
Fix this and the rest will flow including sheria za kupanga nyumba na kadhalika.
Sababu, hakuna waku implement hata sheria ya kupanga nyumba ikishapitishwa kama mtu anaweza toa rushwa na kuwa juu ya sheria.
 
Hoja na wazo ni zuri lakini je litafanikiwa kama anavyotarajia?

Nyumba nyingi za kupangishwa hapa mijini na pembezoni kwenye Posh areas ni za Wazee ambao ndio wanapelekewa mapendekezo hayo. Hii sheria haitahusu nyumba za vichochoroni pekee kama wengi wanavyofikiria bali zote pamoja na Bungalows za Masaki, Mikocheni,Mbezi Beach, Kigamboni etc.

Kwa upande wangu naona itakuwa ngumu. Makamb na Zitto wamejitahidi kutetea posho kubwa za wakuu siziongezeke klakini jana meona wakizomewa na hao hao watakaojadili hayo mapendekezo. Tuombe heri na amani kwetu na nchi yetu.
 
shauri yenu ambao hamjengi nyumba fedha yote mnayopata mnaweka heshima bar na kutumia ovyo ovyo
 
January Makamba anaakili nzuri na ni msomi hasa lakini si mzalendo ! hajawahi kuwa mzalendo na hatakuja kuwa mzalendo.

Mzalendo hafungamani na wahaini, wezi wa mali ya umma na mafisadi papa. . . muuulizeni nani alidhamini kampeni zake kule Bumbuli na kwanini walimdhamini !!? hana lolote kizazi cha nyoka tu.
 
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni huyu kijana ni kama ile CCM ya kweli inayowapigania wananchi
 
Kuna watu wanataka tuamini kila jambo la kizalendo linafanywa na cdm. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.
Objectivity pays a lot. CDM or non CDM does not matter. An issue here is what can we do about our country that is in the ICU. January and most of CDM are exemplary let us emulate from them.
 
Tuacheni siasa za ushabiki mimi chadema mwenye msimamo mkali nasema january jembe lazima tukubali mwanzo mwisho yuko ccm lakini mpiganaji wa ukweli
 
Tuacheni siasa za ushabiki mimi chadema mwenye msimamo mkali nasema january jembe lazima tukubali mwanzo mwisho yuko ccm lakini mpiganaji wa ukweli

Wewe sio Chadema bali ni shabiki wa Chadema,Chadema ni chama
 
Back
Top Bottom