January Makamba na Byabato wametuingiza chaka umeme ni mwendo wa ratiba sio mgao

ichumu lya

JF-Expert Member
Aug 11, 2016
2,605
2,729
Awa ni watu waliokataa mapendekezo ya wananchi juu ya utunzaji wa mazingira nchini katika kipindi chao tumeshuhudia matumizi ya kuni na mkaa yakiongezeka kwa kasi uku matumizi ya umeme asa majumbani yakipungua kutokana na bei ya umeme (bill) kuwa juu na umeme kubaki kuwasha taa na kunyoosha nguo.

Kama wadau wa mazingira tulishauri bei za kununulia umeme zipungue watumiaji wa chini kabisa wapate unit 250 kwa bei ya 9, 500+1, 500 za majengo jumla T.sh, 11, 000/kwa mwezi hii ingewalazimu wananchi kutumia umeme kupikia majumbani, mama rishe, na maeneo mengi wangeokoa mazingira kwa kuachana na mkaa na kuni ambavyo ndio chanzo kikuu cha uharibifu wa mazingira lakini walikataa licha ya mapendekezo kupelekwa Wizarani sijui wao walinufaikaje na ukatwaji miti kwaajili ya mkaa na kuni ivyo watu awa wamekuwa maadui wakubwa wa mazingira katika kipindi chao chote walipokuwa wameshikilia Wizara ya Nishati.
Hawakujiuliza iwapo watu wengi wangetumia umeme serikali ingepata kodi kiasi gani hawakujiuliza kwanini Magufuli alita kila nyumba iwe na umeme nadhani uko mbele kama angekuwepo bei ya kuunganisha Tsh. 27, 000/ angeziondoa na mwisho angelazimisha kila nyumba kufungwa umeme mpaka waishio maporini lengo lilikua kodi lakini pia utunzaji wa mazingira eneo hili alikua sahihi kabisa.

Swali wameacha alama gani katika nchi yetu? Watakumbukwa kwa lipi?
Tukimuweka pembeni aliyekuwa Naibu Waziri Adv.S.Byabato tumjadili January Makamba kwanza historia inaonyesha kuanzia baba yake mzee Yusufu Makamba ni watu wasiojari kabisa nakumbuka uyu mzee akiwa mkuu wa mkoa apa mjini alitupelekesha alidhani jiji nila ukoo wake nayeye ndiye mwenyekiti wa ukoo.
Nigeukie timu VETTING kwanini hammshauri Rais juu ya wateule? Haiwezekani Rais anaingia chaka na nyie mpo tu matokeo yake nchi inayumba kutokana na ninyi kushindwa kumsaidia Rais kwenye kupata watu wa sahihi wa kufanya nao kazi.
Leo mtu aliyeshindwa kutatua kero ya umeme anapelekwa Mambo ya nje kakosa mtu sahihi wa kupeleka nje? Mnampelekaje mtu aliyeshindwa ndani? Yaani mtu ashindwe kuongiza familia yake akaongoze nchi? Apo kuna tatizo kubwa sana muda naona Wizara ya mambo ya nje ikiyumba naona mahusiano na nchi marafiki ukiyumba kama umeme ulivyoyumba nchini na kupelekea uharibifu mkubwa wa mazingira.
Nchi imeingia kwenye ukosefu wa umeme nakulazimishana migao inayoitwa ratiba na kuvuruga uchumi wa nchi. Kumbuka wafanyabiashara wanaingia hasara ambayo TRA haitaki kusikia wao wanataka kizima uku mfanyabiashara akigumia kwa maumivu yaliyotokana na ukosefu wa umeme uliopelekea bidhaa kuharibika.
Mpaka apo hamjaona madhala ya January?

Tunahitaji watu wenye akili wanaotanguliza uzalendo wenye fikra tunduizi (critical thinking) katika nchi yetu ili tuondoke kwenye mkwamo mkubwa wa utawala wa mazoea na kuleta ustawi wa uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Aya hayatokuja kwa miujiza lazima tuungane kwanza tupate Katiba bora inatakayoondoa madalaka ya Rais kuteua mtu yeyote anayemtaka ata kama hana sifa mradi awe kada na chawa wake. Katiba itakayo rudisha madaraka kwa wananchi na kuwaadhibu wezi na wabadhilifu wa fedha zetu na mali ya Umma kwa ujumla.
Tunataka katiba mpya sio kwaajili ya vyama bali kwaslahi makubwa ya nchi yetu.



View attachment 2777354View attachment 2777356
Screenshot_20231010-055716.jpg
 
Back
Top Bottom