January Makamba adai kuna mtikisiko wa uchumi nchini

Ni kweli lazima tupitie kwenye wakati mgumu sana kipindi hiki cha mwaka mzima au hata miwili! Suala la Zbar na mizigo kupungua, mzunguko wa pesa umepotea mijini nchi inakuwa kwenye mkwamo wa kudodorola kwa uchumi! Kosa letu hatukubali kuwa tuna koloni letu ambalo ndio limetufikisha hapa tulipo! Tunaogopa kivuli chetu na kubakia kukimbilia kwenye kufunga mikanda!
Mzunguko wa pesa umepotea kwa mafisadi..

Kama ukosefu wa pesa kwa mafisadi ndio kutikisika kwa uchumi basi na utikisike hata dunia...lakini mwisho wa siku tutaheshimiana hapa mjini...
 
Tatizo la 'Ngosha' yeye ni mfanyakazi zaidi kuliko kiongozi/mtawala.
Asipoangalia hili linchi linakwenda kumuangukia!!
Watanzania tuko matesoni sasa....
Maamuzi yake saa zingine vichekesho, anaahirisha shereh mbal mbal, anasema pesa peleka sehemu fulani sasa ma 'Financial advisors' wanafanya kazi gan!!
Ameingia na moto kwa kwel...Mungu amsaidie tu ila anakoelekea na mdororo huu wa kiuchumi sio kabisa asipotia jitihada haraka baadaye inaweza kuwa sio rahis tena.
 
Of course, baada ya kurudisha $300,000 za Mwitaliano unategemea mambo yawe shwarii???????!!!
 
Huyu ni ADUI namba moja wa serikali ya Magufuli. Magufuli asipomwangalia January na genge fulani ndani ya CCM kwa umakini, watamuangusha.

Kwanza wasijidanganye kwamba January ni mwenzao. Huyu ni fisi katikati ya Kondoo. Ana vijana mia kidogo aliowaajiri kumchafua Magu mitandaoni. Habari ndio hiyo
 
Kuyumba kwa uchumi mara kabla na baada ya uchaguzi kwa nchi za Afrika ni jambo la kawaida na kwa Tz miaka yote imekuwa ikitokea hivyo sasa unashangaa nini? Au uwezaliwa awamu ya JK?
 
....ujuha huu/..
HV VIONGOZI WANAPOSEMA TUFUNGE MIKANDA, UNADHANI NAO HUFUNGA MIKANDA?..
kalagha bao.....
 
Hakuna mtikosiko wa uchumi katika nchi yetu, kuna malalamiko kutoka kwa wakwepa kodi......
 
Hapo bado vikwazo havijaanza kufanya kazi.ifikie mahala viongozi wetu wawe wakweli.
 
Alichosema ni sawa kwa maana mfumo wa uchumi wetu unapitia mabadiliko makubwa kama vile serikali kubana matumizi, na mashirika yake kufunga account katika benki za kibiashara, kuzuia kuchapisha kalenda, kadi pia vikao nje ya majengo ya serikali marufuku. Vilevile banas zimefyekwa.
Huu ni mtikisiko uliotegewewa na nidhahiri. Sasa cha ajabu ni nini hapo
 
Back
Top Bottom