Mkuu Kelly, heshima yako na tupo pamoja sana,
- Ninamfahamu sana huyu kijana Januari, amesoma Boston na kumaliza Masters kule tena akiwa na grades nzuri sana, ingawa grades au ukali wa shule, au kuandika haujawahi kuwa ni nyenzo ya umahiri katika kupima uwezo wa mtu kuwa kiongozi mzuri wa taifa au wananchi kwa ujumla, Mwalimu alikuwa na kichwa kizuri sana, maneno mazito sana, matendo mazuri sana kama kiongozi, pia aliweza kuandika vizuri sana hoja, lakini to this day bado tunataka kutoana macho kila wakati hapa JF, as of what was his achievements na accomplishments, meaning kwamba haya yote yanayosemwa kama mapungufu ya Januari sio tija kabisa katika kutabiria mwananchi anayeweza kua kiongozi bora kwa standards zetu hapa JF.
- Januari baada ya kumaliza Boston, kwa kifupi ninajua aliomba kazi Foreign ambako alipata kazi hiyo baada ya kupitia a very nasty test ya huko ambayo huwatoa nje watoto wengi wa vigogo wanaotafuta mteremko huko. Januari ameingia huko kipindi ambacho maofisa wengi wa muda mrefu huko walikuwa wanastaafu, kukawa na vacuum kubwa sana iliyompa nafasi kung'ara sana kwa kipindi kifupi sana yeye na kijana mmoja anayeitwa Togolane, mpaka kupata attention ya the then waziri wa nje, rais wa sasa Mh. Kikwete, aliyemchukua na kumfanya muandishi wake, au personal aide to the minister, kazi ambayo in the past imewahi kufanywa na some great Tanzanians kama Sam Mdee RIP, Godfrey Nkulu, Ben Mkapa, Ole Kambaine, Athur Mwakapugi na wengineo, hakuna aliyeweza kutabiri kama hawa niliowataja wanaweza kuishia kuyafanya waliyoyafanya walipopewa uongozi wa juu wa taifa na hawa wote hakuna aliyejua uwezo wao kiuongozi isipokuwa mabosi wao tu, na ndio fate ya Januari kiuongozi ilipo sasa.
- Kazi yake sasa hivi ni msaidizi wa rais, inaitwa msaidizi kwa sababu anatakiwa kufanya mambo mengi sana kila siku ya Mungu, licha tu ya kupangilia uandishi wa hotuba za rais, sasa hivi kwa lugha za kitaalamu ni messenger, kazi yake ni kutumwa shughuli za rais tena mbali mbali, sasa katika state ya kutumwa tena na rais, knowing kwamba msingi wa kazi yake ni uaminifu kwa rais sio rahisi kumuhukumu kwamba anafaa au hafai katika state ya kikazi aliyonayo sasa hivi, kwa sababu ni mara chache sana au almost zero chance kwamba anaweza kufafanya kazi kwa maamuzi yake binafsi kama msaidizi wa rais, kwa hiyo hoja kwamba hafai siioni inatokea wapi hapa!
- Halafu hili la kuandika vizuri au kupangilia hoja vizuri, sijui ni wapi limewahi kuwa proved kama ni important quality kuwa nayo ili uweze kua kiongozi mahiri , ninasema hivi tufike mahali tuwe waangalifu na hizi hizi tathmini zetu na kujali ukweli zaidi kuliko ubinafsi, chuki na wivu, kwa sababu sisi JF ni kioo cha taifa, na ni wengi sana wanaokuja hapa kutafuta ideas na hata elimu kwa ujumla, sasa tukianza kutokuwa makini na tunayoyasema kama hukumu kwa viongozi wetu na hasa watarajiwa, tunaweza kuishia kuonekana kama wananchi tusiokuwa na muelekeo mbele ya jamii ambayo tunajaribu sana kuiamusha kutoka usingizini, maana sio siri kwamba jamii yetu Tanzania imekua kwenye usingizi wa ajabu sana, sasa tusiwaongezee usingizi mzito zaidi na hukumu zisizojali facts.
- Sio rahisi kujua uwezo wa kikazi au uongozi kwa Januari, kwa position aliyonayo sasa hivi, kuongea tu maneno mazuri au hoja is not enough, labda bosi wake ndiye anayeweza kutoa hukumu, ingawa na sisi wananchi tunaweza kuichambua kazi ya uongozi wa bosi wake kwa taifa letu atakapomaliza rasmi kazi yake kwa taifa na kuweza ksuema kama Januari aanao uwezo wa uongozi au hana, maana wanasema show me your friends tu inatosha kujua wewe ni nani, otherwise kwa sasa kuanza kumhukumu kwamba hafai au anafaa kua kiongozi, kwa maoni yangu ninasema hakuna enough facts za kuzitumia kumhukumu.
Ahsante Sana Wakuu.
William.