Januari aitupia zigo Menejimenti ya zamani ya TANESCO kuchelewa mradi wa JNHPP

saidoo25

JF-Expert Member
Jul 4, 2022
602
1,407
Waziri wa Nishati, Januari Makamba amenukuliwa akiitupia lawama bodi ya wakurugenzi na menejimenti ya TANESCO iliyopita kwamba ndio imehusika kuhujumu mradi wa Bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere na kushindwa kukamilika kwa wakati kwa mujibu wa mkataba.

Kama itawapendeza wajumbe naomba tutajiwe majina ya hao wajumbe wa bodi ya TANESCO iliyopita na Menejimenti ili tuungane na Waziri Makamba kuwalaani kwa kutucheleweshea mradi huu mkubwa.
 
Hii mbona ngumu kumeza, yani wale wajumbe walioteuliwa na waziri aliyekuwa na dhamana hiyo baada ya kupokea maelekezo toka kwa bosi wake Magufuli [RIP], leo wawe sababu ya kukwamisha ujenzi wa hilo bwawa? No.

Mimi naona kinyume chake ndio kweli, hawa wajumbe wa sasa, walioteuliwa na Makamba baada ya kupokea maelekezo toka kwa bosi wake Samia kwamba sasa gas ndio kila kitu, ndio wanaokwamisha ujenzi wa Nyerere Dam.
 
Nadhani shida ilikua kwenye usimamizi sio hujuma za makusudi.
Kushindwa kumsimamia Mwarabu kwenda kulingana na ratiba iliyowekwa.
Ni ukweli usiopingika kazi iko speed sasa.
Ila shaka yangu ambayo sina uhakika nayo je bwawa likiaa tayari na tuna mikataba mirefu ya na makampuni ya gas itakuwaje? Tutavunja mikataba au makampuni ya gasi yataendelea kupata pesa za ununuzi wa gesi yao hata kama hatuihitaji ila tuna mikataba mirefu?
 
Tunajua hawana dhamira ya kumaliza Bwawa la Mwl Nyerere.
Hizi zingine ni POROJO na danganyatoto kwa wingi na kudandia sababu za kitoto ili kutafuta uhalali wa kutomalizia Bwawa la Mwl Nyerere.
 
Back
Top Bottom