'Janja' yamuokoa JK Karatu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'Janja' yamuokoa JK Karatu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Oct 25, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  'Janja' yamuokoa JK Karatu

  • Watu wasombwa majimbo mbalimbali kumnusuru

  na Mwandishi wetu, Karatu,
  TANZANIA DAIMA


  MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete, jana alilazimika kukusanya watu kwa mabasi kutoka Arusha mjini kwenda wilayani Karatu kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wake wa kampeni.

  Habari za kuaminika kutoka Karatu zinasema hali hiyo inatokana na Karatu kuwa ngome ya mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa.

  Dk. Slaa ambaye amekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa kipindi cha miaka 15, anaonekana kuliteka jimbo kwa shughuli mbalimbali za maendeleo ambazo amekuwa akizianzisha.

  “Huwezi kuamini, jana hapa Karatu yaliingia mabasi matano kutoka Arusha yakishusha wafuasi wa CCM kwa ajili ya kuja kujaza watu wa kumsikiliza Kikwete, unajua hapa ni ngome ya CHADEMA ndugu yangu… sasa inawezekana walihofu kukosa watu,” kilisema chanzo chetu cha habari.

  Aidha, chanzo hicho kimesema uongozi wa CCM Mkoa wa Arusha, uliagiza kila mgombea ubunge katika majimbo yote ya mkoa huo kuhakikisha anasafirisha watu kama alivyoagizwa ili waweze kuhudhuria mkutano huo.

  “Huwezi kuamini mpaka jana nyumba za kulala wageni zilikuwa zimefurika ndugu yangu, utadhani kuna ugeni wa kitaifa… hawa jamaa hapa hawakubaliki kabisa,” kilisema chanzo chetu.

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, amekuwa kiongozi kwa kwanza mstaafu kujitokeza hadharani kumnadi Kikwete mbele ya wananchi, tangu kampeni hizo zilipozinduliwa Agosti 21, mwaka huu.

  Sumaye aliwataka wananchi wa Karatu kumchagua tena Kikwete ili aweze kutekeleza ahadi ambazo amezitoa kwa ajili ya faida ya taifa.

  “Mko tayari kumchagua Kikwete Oktoba 31, mwaka huu? Mchagueni ili atimize ahadi alizotoa kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu,” alisema Sumaye kabla hajapanda jukwaani kumuombea kura Kikwete.

  Akizungumza katika mkutano huo uliofanyia wilayani Kiteto, Kikwete aliahidi kuwalipa fidia ya mbegu bora za mbuzi na ng’ombe wafugaji waliopoteza mifugo yao wakati wa ukame.

  Alisema lengo la fidia hiyo ni kuhakikisha shughuli za ufugaji bora zinaendelea ili wananchi waliopoteza mifugo yao wapate kujikimu kimaisha.

  “Tumejiandaa kuwalipa fidia ya mbegu bora za ng’ombe na mbuzi wafugaji wote waliopoteza mifugo yao kipindi cha ukame,” alisema mgombea huyo na kuongeza kuwa fidia hyo itaanza kutolewa mapema mwaka ujao.

  Alisema uhaba mkubwa wa maji unaolikabili jimbo hilo utakuwa historia hasa baada ya mchakato wa uchimbaji visima virefu kwenye vijiji 10 unaoendelea vizuri.

  Alisema mradi huo umefadhiliwa na Benki ya Dunia ambapo kazi hiyo itaanza mapema mwakani, ingawa hakuvitaja vijiji vitakavyopatiwa huduma hiyo muhimu.

  Kwa mujibu wa mgombea huyo, Serikali ya Marekani imekubali kusaidia usambazaji wa umeme kwenye vijiji 10 vya Wilaya ya Kiteto.

  Kikwete alivitaja vijiji vitakavyopata umeme kuwa ni Matui, Kaperesi, Isugumi, Mapango, Chekanao, Chapakazi, Dosidosi, Machunga na Kiteto.

  Awali, aliwaeleza wananchi waliokuwepo kwenye mkutano huo kwamba changamoto zilizopo zinatokana na maendeleo yaliyopatikana katika sekta mbalimbali.

  Leo mgombea huyo yupo mkoani Mwanza akiendelea na mikutano ya mwisho mwisho ya kampeni za kuomba kura na kuwanadi wagombea ubunge na udiwani wa chama hicho.

   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Duh! Hata mimi niliona ktk TV watu ni wachache mno! Nadhani danganya hii ni maandalizi ya kuiba kura!
   
 3. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Wanataka kutumia hadaa ya kujaza mikutano ili wachakachue kura bila wasi..
   
 4. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #4
  Oct 25, 2010
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Kama JK atashughulikia maji Kiteto, Mbunge atakuwa na kazi gani?
   
 5. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #5
  Oct 25, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,629
  Likes Received: 140
  Trophy Points: 160
  Kuna watu wa CCM Arusha wengine walikuwa madiwani wako ktk msafara wa Kikwete karibu 75% ya muda wao. Bila kuchakachua ktk idadi ya watu ingekuwa aibu kabisa. Uchakachuaji huu unaoendelea ni sehemu tu ya UCHAKACHUAJI mkuu utaofanywa ktka matokeo ya Uraisi.
   
 6. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #6
  Oct 25, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Siyo Karatu tu ambapo mchezo huo unafanyika, ni karibia majimbo yote.
   
 7. Gerad2008

  Gerad2008 JF-Expert Member

  #7
  Oct 25, 2010
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 489
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Kama JK ana uwezo wa kuwafanyia watanzania mambo mengi namna hii je miaka mitano iliyopita alikuwa wapi hakuyafanya. Au hakuwa anayajua kwa sababu ya kujihusisha zaidi na safari za kimataifa au maana yake nini. JAMANI KWA MTU MZIMA HUNA HAJA YA KUJIBIWA KWAMBA HII NI JANJA YA KUPATA KURA ILI AANZE TENA SAFARI ZA NJE.

  WATANZANIA ENOUGH IS ENOUGH TUSIDANGANYIKE

  KUZRA ZOOOTE TUMPE DR. WILBROD SLAA
   
 8. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #8
  Oct 25, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  narudia kusema kuwa MWAKA HUU HAKUNA KULALA MPAKA KIELEWEKE.
  KULE HAWEZI KUPATA KITU JK, NA TAYARI AMEHESABU KUSHINDWA.
   
 9. Konakali

  Konakali JF-Expert Member

  #9
  Oct 25, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Hata mimi nashangaa Simanjiro kupata maji kutoka Ruvu....! Hivi kweli Jk anafahamu jiografia ya Tanzania na alichokuwa akiongea?
   
 10. PAS

  PAS JF-Expert Member

  #10
  Oct 25, 2010
  Joined: May 3, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  ukitaka kumwua nyani usimwangalie usoni, we acha ajifanye nyani lakn karatu ni ya chadema tu>>
   
 11. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #11
  Oct 25, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Yaani kama ni kudanganywa jamaa anadanganywa sana, anayoambiwa sijui achanganyi na za kwake!
   
 12. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #12
  Oct 25, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,861
  Trophy Points: 280
  Ukiangalia kwa karibu sura ni zilezile...wanahamishwa toka mkutano mmoja kwenda mwingine
   
 13. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #13
  Oct 25, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Magazeti yao yameandika eti "kafunika Karatu" na eti "wananchi wa Karatu wamewachoka wapinzani"
   
 14. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #14
  Oct 25, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Wamekusanywa viongozi na makada wa mikoa ya Arusha na Manyara na wanachama wao kutoka miji mingine eti ndio wanasema wananchi wa Karatu. Wanajua kujidanganya hawa jamaa!!!!
   
 15. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #15
  Oct 25, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  hizo ndo zinautw PROPAGANDA
   
 16. K

  KASRI Member

  #16
  Oct 25, 2010
  Joined: May 2, 2009
  Messages: 93
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  :thumb:KARATU SAITAAA!!!!!
  HAO JAMAA WALIOBEBWA KUTOKA SEHEMU ZA MTO WA MBU, MONDULI, NGORONGORO, MAKUYUNI, ARUSHA MJINI NAWAONEA HURUMA MAANA WAMEPOTEZEWA MUDA WAO KWENDA KUPIGWA NA VUMBI LA KARATU - WENGI WAO SASA HIVI WANA KOHOA NA MAFUA KWA SANA. POSHO ZENYEWE DUH! KULALA, KULA NA KUNYWA TU.

  WEWE SUMAYE NAFAHAMU NI AIBU TU IMEKUPELEKA KARATU. NAFAHAMU UNAMKUBALI SLAA ILA UNAOGOPA KUWA WAZI - WATAKUELEWAJE WENZAKO WANA MTANDAO. UMEENDA KUUA SOO TU HILO LIPO WAZI.

  WATANZANIA TUNAMKUBALI SLAA KWA SANA.
  NANI ASIYEPENDA KIPYA?
  NANI ASIYEPENDA ELIMU YA NAFUU/BURE?
  NANI ASIYEPENDA RAISI MWENYE UCHUNGU NA NCHI YAKE?
  NANI ASIYEPENDA KUONGOZWA NA MTU MUWAZI KIASI CHA KUWEKA MAMBO YAKE BINAFSI HADHARANI?
  NANI ASIYEPENDA KUONGOZWA NA RAISI ASIYEOGOPA MTU HASA KATIKA HAKI?

  KWA HAYO BAADHI YA MASWALI HAPO JUU JIBU LIPO NA NI "MUOVU/MWONGO/MWIZI/KIBARAKA/ASIYEJIAMINI/FISADI/MDHULUMU/ETC.

  SAA YA MABADILIKO NI SASA.
  WEWE MWANA CCM UNAYESHABIKIA CHONDECHONDE ENDELEA KUMDANGANYA JK LAKINI MWISHO WA SIKU 31 OCTOBER 2010 NENDA KAMCHAGUE DR. WILLIBROAD SLAA ATUONGOZE NA KUBADILISHA TANZANIA IWE NZURI KWA MANUFAA YETU NA WATOTO/WAJUKUU ZETU.

  KIURAHISI TU! JARIBU KUFIKIRIA WANAOMUUNGA MKONO DR. SLAA NI WASOMI NA WENYE NAFASI NA MICHANGO KATIKA JAMII (WANAHARAKATI NK). UNADHANI WAO HAWAIJUI CCM?

  TAREHE 31 OCTOBER 2010 TUMPE DR. SLAA KURA ZA NDIO.

  NAWASILISHA.

   
 17. K

  Kikwebo JF-Expert Member

  #17
  Oct 25, 2010
  Joined: Aug 25, 2006
  Messages: 352
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Huu sasa ni mzaha. Sisi tulisikia kama Arusha yote ni CHADEMA tu na CCM hakuna kiti! sasa hao watu wakujaza mabasi matano wametoka wapi?
  CHADEMA punguzeni hizo. Duuh!
   
 18. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #18
  Oct 25, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,526
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Sumaye anagalia usianze uzushi hapa . JK hafai kuongoza.
   
 19. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #19
  Oct 25, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,589
  Likes Received: 1,675
  Trophy Points: 280
  Kaka kuna RUVU ya Simanjiro ipo mpakani mwa msitu wa tembo karibu na moshi(Same)
   
 20. F

  Froida JF-Expert Member

  #20
  Oct 25, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Haha anajidhalilisha mzee mtu mzima nchi nzima wanajua anahutubia watu walewale kila anapoenda ,duh awe na aibu basi
   
Loading...