Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 969
- 1,939
Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Arusha, Cecilia Pareso, ambaye pia aligombea Ubunge wa Jimbo la Karatu lakini hakufanikiwa kupata kura za kutosha katika uchaguzi wa ndani uliompa ushindi Daniel Awaki, ameonesha ukomavu wa kisiasa kwa kupanda jukwaani kwa mara ya pili kumuombea Awaki kura kwa wananchi wa Karatu.
Pareso ameeleza kuwa kurejea kwake CCM kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kulitokana na ushawishi wa Awaki. Hivyo, amewataka wananchi wa Karatu kumuunga mkono Awaki ili aendelee kuwa Mbunge wao. Aidha, amesisitiza kuwa ni muhimu wananchi kumpa kura za kutosha Awaki pamoja na Mgombea Urais kupitia CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na wagombea wa nafasi za Udiwani wa CCM.