mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,663
- 18,037
Haya makubaliano ya kuoleana baina ya jamii mbili bila kutozana mahari tuyamulike! Jamii moja mabinti zake wengi walishaolewa tayari! Ndiyo inakuwa ya kwanza kupendekeza mambo ya kuoleana bila kulipishana mahari! Jamii nyingine bado ina mabinti wengi ambao hawajaolewa.
Japo kila jamii inapewa kibali kwenda kuoa bure jamii ya jirani lakini upande mmoja hauna mabinti wa kutosha! Utaenda kule na kutafuta binti wa kuoa na hutampata! Wao wakija kwako wataoa maana una mabinti wengi! Vijana wako utakuwa umewaongezea ushindani bila sababu ya msingi.
Hali kadhalika kwa Kenya kusema watanzania tuende huko kufanya kazi na biashara bila vibali. Huko kumebana!! Kwetu bado ni bwerere!! Hivi inahitaji mtu kuwa na PhD kuliona hilo. Ukinaswa kwenye mtego ulio wazi hivyo watu hawataamini kuwa umenaswa kwa bahati mbaya, bali ulikuwa na jambo lako.
Sisi Tanzania bado tunaongea habari ya kutoa ardhi kwa wawekezaji huko kwa wenzetu hakuna hiyo ardhi ya kumpa mwekezaji haipo!! Wao unyang'au uko kwenye damu na wanauonea fahari wakati sisi tumejaa "undugu"!! huwezi kutoboa!! Wanaoweza ni wafanyabiashara wakubwa tu kama kina Bakhresa.