Janja mpya itakayotumiwa na wauza mafuta

Kwanini ungoje wahindi na waarabu waagize, kwa nini usiagize wewe mwenyewe? Unanshangaza!

Faiza Foxy kweli una mafilifili kichwani. Yaani kabisa unaongea maneno haya?
Da ...... Kweli sisiemu mnarudi kwenye unyani taratiiiibu.

Kaka mnasema serikali legelege, inaonekana watanzania ni wepesi mno wa kusahau na pengine ata mh JK akitoka madarakani mtakuja kumuelewa baadae na kumuona alikuwa sahihi. Mnayosema serikali strong ndio iliyouza mashirika yote hayo kama unajua kulikuwa TPDC na TIPPER hebu jisumbue kidogo ni awamu ipi ya uongozi iliyoiondoa TPDC kwenye biashara ya uagizaji wa mafuta? kaulize kiwanda cha tipper kiko wapi na kiliondoka kwenye awamu ipi? kwa ujumla awamu ya tatu ndio moja ya serikali iliyoharibu miundo mbinu ya kiuchumi kuliko serikali ingine yoyote mnaposema uchumi ulikuwa imara kwa vigezo vp? kama mnaangalia thamani ya sh dhidi ya usd mwaka 1995 usd 1 ilikuwa sawa na TSH 510 mpaka dec 2005 usd1 ilikuwa sawa na Tsh 1115, ongezeko la TSH605 kwa miaka 10, mwaka 2006 hadi ss usd1 ni Tsh 1530 ongezeko la 405, ili sarafu iimarike ni lazima tuwe tunauza vitu nje na kuounguza manunuzi kutoka nje, ni awamu hiyo tulioshuhudia mpaka samani za maofisi zinaagizwa kutoka nje huku uchumi wetu ukimilikiwa na wageni, watanzania tuache siasa na kufanya kazi ili tuboreshe maisha yetu, maendeleo ya kiuchumi hayawezi kupatikana kwa kutokuwa na political stability, badala ya kukaa na kulaumu kwenye magazeti, forum mbalimbali na blogs tuamke sasa na kujivunia utanzania wetu bado hatujachelewa tusilaumu haya mnayoyasikia ya ufisadi ni ujasiri wa mh JK na demokrasia aliyokuwa nayo unazani kwenye tawala za huko nyuma hayakuwepo? hakukuwa na demokrasia ya kuweza kuzungumza kama mnavyofanya ss hv, sio vijana wa zamani tunaelewa hilo
, tafakari, chukua hatua tubadilike 1
Tumeyataka sie wenyewe hawo Wahindi au Waarabu si makosa yao ni mimi na wewe ndio wenye makosa kwa nini usijiulize TPDC na TIPPER ziko wapi?

Hawo waliopewa kazi za kuendeleza mashirika ya umma hayo wamefanya nini? zaidi ya kuyauwa?
....tusiwe na nidhamu tu ya kulaumu watu na kutafuta wanyonge wakati makosa ni yetu kuweka serikali LEGELEGE madarakani.

Serikali imelikoroga, meli zenye shehena ya mafuta zimeondoka bandarini na shehena ya mafuta na kuelekea nchi nyingine. Kuanzia leo kama ulipanga kusafiri, bora uhairishe safari yako, wakazi wa jiji jitayarisheni kwa gwaride mitaani mkienda makazini. Hali ni mbaya sana.

Meli zimeondoka baada ya Serikali kuwadanganya waagizaji mafuta kua Imepunguza Gharama wa kuingiza mizigo Bandarini (wharf-age) kutoka 1.6% ya CIF value na kua 1.47% wakati inaendela kutoza 1.6%

Pili katika current exchange ya EWURA, wanatumia rate ya Tshs 1,570/1US$ wakati kununua dola kwa kwa sasa kunafikia mpaka Tshs 1,590/1US$.

Kifupi mchanganuo wa Bei ya Petrol uko hivi,
Bei ya Nje 1,210.94
Usafiri wa Meli 34.00
Bima baharini 16.21
EWURA, Sumatra, Vipimo, TBS, Wakaguzi, TIPER, nk 63.39
TRA 539.00
Faida ya Waagizaji Mafuta 108.69
Usafiri, Depot kwenda Kituo cha mafuta 10.00
Faida ya mwenye Petrol Station 57.50
JUMLA 2,039.73

Nchi iko kwenye auto pilot tusubiri tu labda hali itatulia yenyewe maana hakuna mtawala mwenye uwezo kurekebisha,kukemea wala kuamua...ndio kosa la kuwekwa madarakani na pesa za matajiri hao huwezi kuwakoromoe hata wakitishia usalama wa nchi!!kweli mgeni anatoa masaa 24 kwa serikali??badala ya kushauri na kuiomba serikali iangalie upya akitoa na sababu yeye anawapa masaa 24 kweli??nchi haina mwenyewe!!

Tunayataka wenyewe tunalalamika sana kwenye keybords zetu na hakuna cha maana atunchofanya utadhani tumelishwa limbwata ya kisiasa!! Kwanza natamani waendelee na mgomo kabisa na umeme uishe kabisa na wasafirishaji wote nao wagome na vyakula vipande bei ndipo tutapata akili ya kujua,
maana ya kudai haki

Point!

Kwanini ungoje wahindi na waarabu waagize, kwa nini usiagize wewe mwenyewe? Unanshangaza!

Ukweli ff. I really hate the way u support ccm deeds at the expense of poor citizens. yaani wewe ni muuwaji. huna huruma, una roho mbaya sana. nahisi wewe sio binadamu wa kawaida, huna tofauti na wale wanaojitoa mhanga kule afghanistan. ff unatia kinyaa

wauza mafuta wamepanga yafuatayo:
1. Stock yao ya kituoni ikiisha, hatanunua tena mafuta kutoka depot.
2. Depot wakimaliza stock hawata IMPORT hadi serikali ikubali kupandisha bei ya mafuta kwani wao wanadai running cost zimekuwa juu kutokana na wao kutumia umeme wa jenereta kipindi hiki cha mgao.
MY TAKE:
kwa namna yoyote hakikisha una mafuta mengi sana, kwani hawa wahindi na waarabu nia yao ni kutuangamiza.
Mkuu, kwani hamna waswahili wa kuuza mafuta au nani kawakataza kuuza mafuta!
Kama Waarabu na Wahindi unasema nia yao ni kutuangamiza

Tunayataka wenyewe tunalalamika sana kwenye keybords zetu na hakuna cha maana tunchofanya utadhani tumelishwa limbwata ya kisiasa!! Kwanza natamani waendelee na mgomo kabisa na umeme uishe kabisa na wasafirishaji wote nao wagome na vyakula vipande bei ndipo tutapata akili ya kujua maana ya kudai haki

kweli mkuu hawa CCM wanatupanda kichwani sasa,tunahitajika kufanya kitu tena mapema mno kabla mambo hayajatuharibikia sana.

Nani wa kulaumiwa ni serikali au wahindi/waarabu,mi naona hapo jibu ni wote kwani kila mtu anamatatizo yake.......serikali inategemea mapato zaidi kwenye mafuta kupitia agency zake walizozianzisha kutoza tozo kwenye mafuta kuna kipindi nilisikia kwenye vyombo vya habari Mchambuzi mmoja anasema tozo inafikia hadi Tsh 900/lt,namna iyo kweli tunategemea maisha bora kwa kila mtanzania kweli.
Kwa upande wa wahindi/waarabu nao waache visingizio vya kuwa na stock ambayo imenunuliwa kwa bei ya zamani kabla ya serikali kupunguza tozo kwenye mafuta,kwani serikali toka watangaze kushusha bei ni kipindi kisichopungua mwezi sasa tunaimani tayari stock imeshaisha kwani kila cku mafuta yanaingia bandarini na kusafirishwa nchi za nje.

Nani wa kulaumiwa ni serikali au wahindi/waarabu,mi naona hapo jibu ni wote kwani kila mtu anamatatizo yake.......serikali inategemea mapato zaidi kwenye mafuta kupitia agency zake walizozianzisha kutoza tozo kwenye mafuta kuna kipindi nilisikia kwenye vyombo vya habari Mchambuzi mmoja anasema tozo inafikia hadi Tsh 900/lt,namna iyo kweli tunategemea maisha bora kwa kila mtanzania kweli. Kwa upande wa wahindi/waarabu nao waache visingizio vya kuwa na stock ambayo imenunuliwa kwa bei ya zamani kabla ya serikali kupunguza tozo kwenye mafuta,kwani serikali toka watangaze kushusha bei ni kipindi kisichopungua mwezi sasa tunaimani tayari stock imeshaisha kwani kila cku mafuta yanaingia bandarini na kusafirishwa nchi za nje.

Tutaipima serikali kwa maamuzi magumu hapo mafuta yatakapoisha!!Siyo kudai maamuzi nikumfukuza waziri mkuu!

wauza mafuta wamepanga yafuatayo:
1. Stock yao ya kituoni ikiisha, hatanunua tena mafuta kutoka depot.
2. Depot wakimaliza stock hawata IMPORT hadi serikali ikubali kupandisha bei ya mafuta kwani wao wanadai running cost zimekuwa juu kutokana na wao kutumia umeme wa jenereta kipindi hiki cha mgao.
MY TAKE:
kwa namna yoyote hakikisha una mafuta mengi sana, kwani hawa wahindi na waarabu nia yao ni kutuangamiza.

Wahindi na Waarabu ni wafanya biashara. Hawakuja kucheza zeze. Pengine wewe ndio ungetuangamiza kama tunavyoshuhudia Mashirika ya umma yalivyoliwa na WEUSI wenzetu kama wewe na mimi eenhh!!!!!!

Wakuu, kuna ukweli katika habari hii, nimeangalia kwa muda wa kutosha jioni hii 'flow' ya magari kutoka mjini kwenda mikoani kwa kutumia barabara ya Morogoro, sijaona gari lolote (fuel tanker) linalopita kupeleka mafuta mikoani. So the issue is serious!
upatikanaji wa nishati ya mafuta kuanzia kesho J

Wakuu, kuna ukweli katika habari hii, nimeangalia kwa muda wa kutosha jioni hii 'flow' ya magari kutoka mjini kwenda mikoani kwa kutumia barabara ya Morogoro, sijaona gari lolote (fuel tanker) linalopita kupeleka mafuta mikoani. So the issue is serious!
upatikanaji wa nishati ya mafuta kuanzia kesho J
Uchunguzi wako umezingatia ukweli kwamba leo ni public holiday?
Pili siku mbili ziluzopita zilikua ni wikiend?

Hata kama Tanzania ingekuwa inazalisha mafuta leo, na kuyauza, ndani na nje ya nchi, UHABA UNGETOKEA TU!

Tatizo ni kwamba MAFISADI wameikamata hii nchi, na kimsingi, hakuna wa kuwaambia HAPANA!

Tukitisha maandamano, kuna wengi, wanga, wanoko, wanafiki, humu ndani wataruka na kudai, ni njama za kisiasa, yaani mafisadi kutaka kujisafisha, Wengine watasema aliyeitisha maandamano katumwa. Ili mradi kila mwenye kupinga atapinga, halafu baadaye analaumu.

Unalaumi kitu gani wakati wenzako wanapotaka maendeleo yao na ya taifa lao wewe unapinga? Unasema kuna mafisadi, haya, umefanya nini kuwaondoka hao mafisadi?

Uwoga wenu, Watanzania, ndio utawafanya muendelee kutawaliwa kila siku. Kila siku. Miaka nenda rudi! Hamna ubavu wa kufanya mabadiliko. Hata ziwepo CHADEMA mia tatu, hamtaweza kuwaondoa mafisadi madarakani, kwa kuwa NINYI NI WAOGA! Nawaambieni ukweli, siwaogopi.

Mtaikalia politiki, wenzenu wanachakachua, kilaini. Wanajilia vyenu na vyao, kilaiini. Kodi zenu zasomesha watoto wao, nje ya nchi, watoto wanaenda kutanua ulaya, wanafanya starehe. Wake zao wakipata ujauzito, kujifungua ni ulaya, UK na USA. Mnabisha? Endeleeni tu. Kwani si mmepewa midomo ya kuongea na mikono na vidole vya kutype post zisizo na kichwa wala mguu? Safi sana! Endeleeni!

Kweli mimi sioni sababu ya kulalamika, ati hakuna mafuta, wakati ninyi MMEWAPA hao mafisadi ruksa ya kufikiria kwa niaba yenu. Mtu akishapokea chake, unadhani atafanya nini? Akuangalie, we nani? Hahahahaah!

Sijatumwa, ila ukweli ndio huo! HAMNA UBAVU wa kufanya mabadiliko. Kwa hiyo kelele zenu hizo za chura hazitamzuia tembo kunywa maji! Nimemaliza!

Leo sitasaini!

Back
Top Bottom