SoC03 Janja janja ya China kupata faida maradufu Yani (super profit)

Stories of Change - 2023 Competition

fundi radio

Member
Apr 2, 2023
45
95
Kwa Hapa nchini Tanzania ambayo Ili kuwa na mfumo wa kijamaa, kutoka TANU mpaka CCM.

CCM Bado Ina urafiki na nchini ambazo zilikuwa na mfumo wa kijamaa kama washirika wake wakaribu. Na china (ujamaa) inaitumia fursa hiyo vizuri sana,Kwa kujiweka karibu sana na viongozi waandamizi wa chama tawala (CCM).

Hali ni tofauti Kwa nchi za magharibi (kibepari) wao wakiwa na urafiki wa watu wa Chache kwenye chama tawala na wa vyama vya upinzani,
lakini China ina mafungamano ya karibu sana na chama tawala kiasi Cha kuwa na ushawishi mkubwa.

Kisiasa:
Mafungamano hayo :
I) chama tawala Cha china Kila mara kime kuwa kikitoa misaada ya kifedha na rasilimali mbalimbali Kwa ajili ya Chama Cha CCM.

ii) chama tawala cha china kimekuwa kikitoa mafunzo ya kiutawala na uongozi Kwa viongozi mbalimbali wa chama Cha CCM. (scholarship).

iii). Na Sasa wamejenga chuo Cha uongozi hapa nchini Tanzania, bila shaka kwenye hayo masomo ya uongozi yatakuwa yameandaliwa na Serikali ya China Kwa Falsafa za kijamaa zaidi, ya chama kimoja kutawala pekee.
IMG_20220219_214120_648.jpg

Ni Bora wangeongeza masoma kama ujasiriliamali, uchumi wa kijani,bluu,tehama Katika utumishi, diplomasia, Ili kuleta tija Kwa viongozi wanao tahiniwa.

iv). China kuisadia Tanzania kwenye maswala ya ulinzi na usalama.

Je nchi yetu inahitaji sera za kijamaa ,(chama kimoja), Ili iweze kujiletea maendeleo?

HAPANA, Tanzania inahitaji viongozi watakao fanya kazi Kwa moyo wa dhati kabisa ikiwa pamoja na kusimamia katiba na Sheria za nchi yetu.

a). China kuandaa viongozi watakao kuwa na falsafa za kijamaa zitakazo wasaidia kuwa karibu na viongozi wa chama tawala, kumbuka siku zijazo ,hato chaguliwa kiongozi wa CCM ila awe amepitia kwenye hicho chuo.

Matokeo ya china kujiweka karibu sana na viongozi wa sekretaiti ya Chama tawala (NEC), kama ifuatavyo

Kiuchumi.
Kandarasi za ujenzi wa barabara,madaraja, majengo makubwa, kandarasi za miundombinu ya nishati, ulinzi Kwa asilimia kubwa anachukua china.

Mzunguko wa fedha za kigeni zinaangukia mikononi mwa china.

Fedha za mikopo nafuu Kwa ajili ya Miradi ya maendeleo kutoka IMF, world Bank, UK, AFDB, ufaransa, EU , kandarasi zote anapewa China,
Kumbuka hizi nchi wafadhili wana viwanda vyao na mitaji huko nchini china .

ambapo baadae tunauziwa bidhaa kutoka china, Na Bado Tena china anachukua kandarasi zote za Hawa wafadhili Kwa hiyo mzunguka wa fedha za kigeni unazungukia upande wa china pekee.

Na kupelekea china kupata faida maradufu , Yani (super profit)🤑

Changu changu chako changu (win win)

Ni tofauti na nchi za magharibi mfano USA, UK, EU wanapotoa misaada, wanazipa fedha Serikali kuu au kuanzisha programu za maendeleo ya jamii nchini.ili kuleta uchumi jumuishi kwenye jamii.

Serikali ya China ikitoa misaada ya kifedha Kwa ajili ya maendeleo asilimia zaidi ya 95% ataitekeleza yeye mweyewe, Kwa hiyo mzunguko wa fedha bado unabaki upande wake TU yani.

Mfano mradi wa Bomba la gesi la mtwara mpaka dar es salaam,china alitoa mkopo wa takribani Dola bilioni $ 1.2, na akautekeleza yeye mweyewe na kutuachia deni lenye riba , ambayo sisi raia hatuijua hilo deni Kwa Sasa limefikia kiasi Gani.

Gesi inapita kwenye hiyo Bomba bado haitumiki kikamilifu , kwenye kuzalisha umeme wa kutosheleza nchini, pia gesi ,bado hatujaanza kuunza nje ya nchi , Kwa hiyo bado tuko kwenye hasara kubwa.

Ulanguzi

Kuwekeza kwenye kamari, mpaka vijijini watu wanatapeliwa ,na Serikali inakaa kimya, huu ni uwekezaji Gani wahovyo namna hii, walalahoi na wavuja jasho na wapiga kura wa Chama tawala ,wanakamuliwa mpaka senti zao za mwisho.
images (3).jpeg

Faida inayopatikana mfano ikiwa ni laki mchina anachukua zaidi ya asilimia 90%, fikiria Kwa jiji la dar mchina anakusanya maokoto kiasi gani Kwa mwezi.🤑

Kwanini wasianzishe miradi mbalimbali ya kilimo ambayo yana mahitaji nchini kwao kama, muhugo,mtama, nyama ya nguruwe , na Kila upande uka faidika (win win).💪

Kukamatwa Kwa raia wa China wakijihusisha na uuwaji wa tembo na faru na usafirishwaji wa meno ya tembo, pembe za ndovu, na pembe za faru nje ya nchi,
images (1).jpeg

bila Shaka waliona Tanzania ni shamba la Bibi, je waliwezaje kufanikisha kufanya huu ujambazi Kwa kiasi kikubwa hicho na Kwa muda mrefu,

bila vikosi vya usalama kujua, mpaka zilivyoanza kelele za Taasisi za kimataifa kuhusu ujangili , Ndio Serikali ikaamua kujitutumua kuondoa aibu.

Huku Wenzao USA, UK EU, wakitoa misaada Kwa ajili ya kulinda wanyama pori na hifadhi zake.
Screenshot_20230727-210827.jpg


Je hii ni ( win win) au (janja janja)?

Kutokuwepo Kwa makubaliano ya kibishara ya kimkakati ya maendeleo Kwa muda mrefu.

Mfano wa (win win) (janja janja) hii sio mkataba bali ni makubaliano TU ya kirafiki (mtego) ya kufanya Biashara baina ya nchi mbili Kwa makubaliano Fulani.

Ambapo Kila nchi Inakuwa na uhuru wa kufanya Biashara.

Kwa hiyo mwenye kisu kikali ndio atakaye kula nyama, hii ilipelekea mpaka wachina wakaja kuuza yeboyebo kariakoo,
images.jpeg


Ila Kwa sisi wa Tanzania hatuna uwezo na Bidhaa za kutosha za kuuza China.

Ni tofauti na AGOA wa USA ,ni mkataba wa makubaliano rasmi inaoeleweka kimkakati baiana ya nchi husika,

mfano mkataba wa AGOA , ambapo Tanzania iliridhia kusaini na kupata fursa ya kuuza mazao yake ya chakula na Bidhaa zingine bila ushuru wa forodha kwenda nchini marekani.

Je kwanini mpaka leo Tanzania hatuja Saini mkataba wa EPA?

Je china Yuko nyuma yake kuzuia EPA isisainiwe, maana Yuko karibu na viongozi wa chama tawala.
Maana wanajua Kama Tanzania tukisaini mkataba wa EPA, watanzania watanunua kwa wingi,Bidhaa za ulaya ambazo zinaaminika Kwa ubora duniani, na China kukosa soko la kuuza Bidhaa zake.

Kulingana na repoti ya wizara ya fedha ya mwaka 2022, deni la China nchini Tanzania lilifikia Dola bilioni 11.6,ikijumuisha mikopo ya kibiashara na maendeleo.

Ushauri:
Ndugu zetu washirika wa maendeleo USA, UK, EU, IMF and world Bank, mnapotoa misaada Kwa ajili ya maendeleo nchini Tanzania,itekelezeni wenyewe na Serikali pasipo nchi nyingine, katikati (third party) kuja kuikamilisha hiyo Miradi.

Pia Chama tawala kisiegemee upande mmoja TU, upande ambao anapata kuungwa mkono Kwa chama kimoja kutawala, ukiukwaji wa haki za binadamu na demokrasia , mizania ikae sawa.
 
We need aF air trade ,

kuna mantiki Gani ya kutoa funds za maendeleo , Lakin mtekelezaji wa hiyo Miradi ni Third Party company, kutoka nje ya nchi, si Bora hiyo Miradi itekelezwe na donor's wenyewe.


1. mfano France walivyo toa 300m USD msaada wa solar panels energy , Lakin anayetekeleza huo Miradi kikamilifu Sio France wala tz, ni company ya nchi nyingine kabisa Yan

2. UK wametoa karibia pounds 300ml Kwa Zanzibar,Pemba Kwa ajili ya airport and roads , Lakin anayetekeleza huo Miradi kikamilifu Sio UK wala Zanzibar, ni company ya nchi nyingine kabisa Yan

Sasa sijui hii ni akili Gani
 
Kulingana na repoti ya wizara ya fedha ya mwaka 2022, deni la China nchini Tanzania lilifikia Dola bilioni 11.6,ikijumuisha mikopo ya kibiashara na maendeleo.
Hii ni Kwa tz Pekee, Je + mademu ya Africa + Europe + Asia + south America + North America==🤑🤑🤑
 
Kulingana na repoti ya wizara ya fedha ya mwaka 2022, deni la China nchini Tanzania lilifikia Dola bilioni 11.6,ikijumuisha mikopo ya kibiashara na maendeleo.
Hii ni Kwa tz Pekee, Je + mademu ya Africa + Europe + Asia + south America + North America==🤑🤑🤑
China haikopeshi Europe na North America akama inavoikopesha Tanzania na Afrika. Badala yake China ilinununua Treasury bonds ambazo zinakuwa controlled serikali inayoziuza. Kwenye swala la Treasury bonds, mtu yeyote anaruhusiwa kuzinunua kama investment, siyo mkopo.
 
Nchi yeyote duniani haiwezi kupiga atua kw akutegemea misaada na mikopo tena yenye riba kubwa,
Kuna haja kwa nchi kama Tz kujiimarisha kwanza kisha kufungua mipaka yake, haitoshi kulalamika ukijua mwenzako amekuzid shart umkwepe kwanza ndio ujipange upya, ama utafute baadaye pakutokea
Si Tz pekee imezidiwa hilo hata ulaya kwa sasa moto ni huu huu kutokea china, ajira za watu zinanyang’anywa usiku na mchana.
China ina cheap labor kuliko nchi yyte duniani, na bado wanauwezo mkubwa wa uzalishaji!
Kuwatukana wachina kwamba wanyonyaji ni unawakosea sana, wanapoteza pesa nyingi kwenye uwekezaji wa kimataifa, mfano hayo madeni wanayokopesha ni ngumu kulipika na serikali nyingi za africa zina roop hol pakutokea!
Hata marekani kwenyewe hakuna viwanda vya uzalishaji kwa sasa hutegemea china kuzalisha na kuuza America!

Hakuna nchi inayoshindana na china kwa uzalishaji ulaya! Wametuzidi sharti tujipange wasituumize zaidi,
Huwezi kumkwepa mchina na mikataba ya win win hata marekani anahangaika hilo

Mpaka sasa china inaidai Marekani kiasi cha dolla $859.4 billion ni unkwepable debt

Huku africani zaidi ya dollar 73 billion na $ 9 billion private sectar sasa zinalipikaje?
 
China haikopeshi Europe na North America akama inavoikopesha Tanzania na Afrika. Badala yake China ilinununua Treasury bonds ambazo zinakuwa controlled serikali inayoziuza. Kwenye swala la Treasury bonds, mtu yeyote anaruhusiwa kuzinunua kama investment, siyo mkopo.
China mpaka sasa inaidai zaidi $859.4 billion marekani! Endelea kuwatetea kwamba ni Treasury bond! Kwanza hizo bond ni necesarry sana kulipa kuliko mikopo yenye riba nafuu iko negotiable
 
China mpaka sasa inaidai zaidi $859.4 billion marekani! Endelea kuwatetea kwamba ni Treasury bond! Kwanza hizo bond ni necesarry sana kulipa kuliko mikopo yenye riba nafuu iko negotiable
Swali china ikiamua kuondoa bond zao maana wamenunua hizo bond ili waweze kuwa capable na dollar, yuan iwe na nguvu! Uamuzi huo utaiadhiri kiasi gan serikali ya america ambayi mwezi ulioisha ilikosa fedha kabla ya mswada kupita ili kulipa wafanyakazi?
 
China mpaka sasa inaidai zaidi $859.4 billion marekani! Endelea kuwatetea kwamba ni Treasury bond! Kwanza hizo bond ni necesarry sana kulipa kuliko mikopo yenye riba nafuu iko negotiable
Basi huji biashara ya treasury bonds; ule siyo mkopo mzee wangu. Huwezi kununua treasury bonds halafukesho ukadai upwewe hela yako kwa nguvu kama mkopo.
 
Swali china ikiamua kuondoa bond zao maana wamenunua hizo bond ili waweze kuwa capable na dollar, yuan iwe na nguvu! Uamuzi huo utaiadhiri kiasi gan serikali ya america ambayi mwezi ulioisha ilikosa fedha kabla ya mswada kupita ili kulipa wafanyakazi?
Huu uzi unaitaji watu wanojitambua ndio maana huwezi ona unaenda kwa kasi kama zilivyo nyuzi nyingine
 
Week iliyopita mwakilishi wa world bank aliongea na Waziri wa fedha Dr mwigulu kuhusu mpango wa maendeleo ya kimkakati Katika jiji la Dar..

Ambayo itahusu kuboresha miundo mbuni ya kuhifadhi taka, sewage systems, ujenzi wa mifereji mikubwa , uboreshaji wa eneo la jagwani, uboreshaji wa barabaa Katika jiji la Dar, ikiwemo (mwendo kasi).

Haya niambie watanzania tunashindwa kujenga barabara za Lami, mifereji, tuna miaka Zaidi ya 60 tokea tupate Uhuru.

Kama issues ni vifaa vya technology ya kisasa, hiyo haina shida wapeni fedha kwenye company zao ambazo Wana hisa DSE, Waka aquired Super technology from developed countries. Na Hajifunza technology haichukui Muda mrefu coz tayar Wana elimu ya uhandisi.

Watarudisha mikopo coz tz bado ina miradi mingi ya maendeleo.

Hizo fedha za world bank zinahitajika kwenye company za ndani ili ziongeze mnyororo wa fedha nchi, na Sio kukimbizia kuwapa tender Asian company na sisi kubakiwa na majengo matupu AU miundo mbuni Pekee ,tunahitaji na fedha za kigeni pia tubaki nazo.
 
China inashikilia deni la Marekani kwa njia ya dhamana za Hazina, ambazo ni dhamana zinazotolewa na serikali ya Marekani. Dhamana hizi hutoa kwa wawekezaji ahadi ya kulipa riba ya mara kwa mara na kurudisha thamani halisi katika tarehe ya ukomavu.

China imekuwa ikiongeza uwekezaji wake katika dhamana za Hazina za Marekani katika miaka ya hivi karibuni. Hii ni kwa sababu China inatafuta njia salama na ya uhakika ya kuhifadhi akiba yake ya kigeni.

Deni la China kwa Marekani ni suala la kisiasa na kiuchumi. Baadhi ya watu wana wasiwasi kwamba China inaweza kutumia deni hili kama njia ya kushawishi sera za Marekani. Wengine wanaamini kwamba deni hili ni uwekezaji wa kawaida na kwamba China haitatumika kama njia ya shinikizo.
 
Soko huria Ki muktadha linaoneka ni Zuri, Ila kiutendaji linaegemea upande 1, mwenye kisu kikali ndio anaekula nyama
 
Nchi za Africa na developing countries wameingia kwenye mtego wa kukopa nchini china Kwa ajili ya shughuli za maendeleo .

Mikopo wanayochukua wanafanya Siri, baadaye mnakuja kusikia airport, mara Bandari zimechuliwa na China, sababu serikali imeshindwa Kurudisha deni la watu Kwa wakati.

China hawezi kulaumiwa Kwa hili coz Yuko anafanya biashara, shida ni nchi za third countries hazijielewi
 
Back
Top Bottom