Jamani shemeji/wifi yenu hata sijui ilikuwaje, maana ninavyomfahamu ni mpole sana japokuwa anasumbuliwa mno na wivu.
Jana nimerudi zangu niko 4GB tu, nikaweka simu hapo kwenye chaji nikaenda kuoga, ile narudi akanidaka na kuniuliza huyu ....... (jina la kike) ndo nani maana amepiga hapa nikapokea nimemuuliza yeye ni nani akakata simu, mimi nikababaika tu maana lilikuwa ni swali la ghafla sana na sikutegemea kabisa, wakati natafuta jibu la haraka haraka ghafla nikashtukia kibao kizito sana kimetua shavuni kikifuatiwa na tusi zito mno halafu akasema na kesho utanieleza vizuri huyo malaya ni nani, nilipoangalia vizuri kumbe ni rafiki yangu wa kike (kikazi lakini) ndo alipiga.
Sasa hapa ndo nataka kuelekea home lakini sijajua nini kitatokea na huyo rafiki yangu nimempa picha yote na akasema hata nikimpigia ili anitetee atasema kuwa mimi ni mpenzi wake (maana huwa tunataniana nae sana kuhusu mambo ya malovee).
Nipeni msaada wa hilo wenzangu
[/........MWACHE AJIFURAHISHE TU