Jana shemeji yenu kanipiga kibao

Jana shemeji yenu kanipiga kibao

Galadudu

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2014
Posts
2,304
Reaction score
780
Jamani shemeji/wifi yenu hata sijui ilikuwaje, maana ninavyomfahamu ni mpole sana japokuwa anasumbuliwa mno na wivu.

Jana nimerudi zangu niko 4GB tu, nikaweka simu hapo kwenye chaji nikaenda kuoga, ile narudi akanidaka na kuniuliza huyu ....... (jina la kike) ndo nani maana amepiga hapa nikapokea nimemuuliza yeye ni nani akakata simu, mimi nikababaika tu maana lilikuwa ni swali la ghafla sana na sikutegemea kabisa, wakati natafuta jibu la haraka haraka ghafla nikashtukia kibao kizito sana kimetua shavuni kikifuatiwa na tusi zito mno halafu akasema na kesho utanieleza vizuri huyo malaya ni nani, nilipoangalia vizuri kumbe ni rafiki yangu wa kike (kikazi lakini) ndo alipiga.

Sasa hapa ndo nataka kuelekea home lakini sijajua nini kitatokea na huyo rafiki yangu nimempa picha yote na akasema hata nikimpigia ili anitetee atasema kuwa mimi ni mpenzi wake (maana huwa tunataniana nae sana kuhusu mambo ya malovee).

Nipeni msaada wa hilo wenzangu
 
Eti nini!!!mwanamke akakuzaba kibao!!!He he he,Mungu wangu are you a man enough?naomba kwa heshima ondoa hii thread yako,umetudhalilisha wanaume,eti nini???nizabwa kibao Hahahahahah makubwa.

Hadi sasa hata mi bado nashangaa sana kwa kilichotokea maana ckutarajia na wala haijawahi kutokea hii kitu
 
Hadi sasa hata mi bado nashangaa sana kwa kilichotokea maana ckutarajia na wala haijawahi kutokea hii kitu

Sasa nikwambie usipokua makini atazoea huyo,kuna siku atakuchapa hadharani,chukua hatua.
 
mkikua mtaacha sim...msg ya mwanamke

watu tunafumania tuna mute
huyo mpenzio mkidumu sana kwenye ndoa maana najua hamjaoana itakua ni miez kadhaa tu
kama asipobadilika
 
Eti nini!!!mwanamke akakuzaba kibao!!!He he he,Mungu wangu are you a man enough?naomba kwa heshima ondoa hii thread yako,umetudhalilisha wanaume,eti nini???nizabwa kibao Hahahahahah makubwa.

Mbona unanaswa tu kiulanii wanaume siku hizi kududwa kawaida kuna mmoja anapigwa hadi majirani wanamuombea msamaha
 
mkikua mtaacha sim...msg ya mwanamke

watu tunafumania tuna mute
huyo mpenzio mkidumu sana kwenye ndoa maana najua hamjaoana itakua ni miez kadhaa tu
kama asipobadilika

Miaka 7 jamani mnasema bado tu hajazowea
 
Eti nini!!!mwanamke akakuzaba kibao!!!He he he,Mungu wangu are you a man enough?naomba kwa heshima ondoa hii thread yako,umetudhalilisha wanaume,eti nini???nizabwa kibao Hahahahahah makubwa.

kamanda jamaa bado anaomba na ushauri wa leo anaingiaje ndani, sio kuzabwa kibao tu adhabu bado inaendelea na yawezekana leo akachezea mikanda ya hatari sana..."AYEEE MAMA WEE INGEKUWA WE UNGEFANYAJEEEEE"
 
Ha ha ha ha mbona amekupapasa tu angekushushia mingumi ka ya Big show ndo ungetia akili

Maana nahic leo atakuwa amejiandaa sana ndo maana nimeomba ushauri kwenu ili mcje kuckia kesho unaimbwa wimbo wa parapanda
 
kamanda jamaa bado anaomba na ushauri wa leo anaingiaje ndani, sio kuzabwa kibao tu adhabu bado inaendelea na yawezekana leo akachezea mikanda ya hatari sana..."AYEEE MAMA WEE INGEKUWA WE UNGEFANYAJEEEEE"

Jana nilikuwa mpole lakin leo hata cjui kitakachotokea
 
kamanda jamaa bado anaomba na ushauri wa leo anaingiaje ndani, sio kuzabwa kibao tu adhabu bado inaendelea na yawezekana leo akachezea mikanda ya hatari sana..."AYEEE MAMA WEE INGEKUWA WE UNGEFANYAJEEEEE"

Mie wala hiyo kesi isingekuwepo,jana hiyo palepale kwenye tukio angeomba po,ila sababu alishamistake anahitaji ushauri sorry huwa sijui kushauri kesi ya mwanamke kumpiga mumewe nitakua na kesi ya kujibu,coz jana alikubali akachapwa kimoja leo awe mpole tu.
 
Back
Top Bottom