Jana nimeng'atwa na nyoka mguuni!

Akhsante sana mkuu kwa ushauri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabisa kabisa mkuu, hata kama watakuwa wanakupiga vita namna gani lakini tafuta wa kuelewana nao miongoni mwao iwapo itashindikana kwa wote.

Sent using Jamii Forums mobile app
Miaka mingi ya nyuma nilikuwa ninaishi maeneo ambayo sasa tunayaita 'uswahilini' lakini enzi zile tulikuwa tunasema 'kwa wenyeji' Hapo jirani yetu mzee mmoja wa kihaya alinunua nyumba akawa anaishi pamoja na familia yake.

Tabia zake zilikuwa akitoka kwenye biashara zake basi huenda msikitini na akitoka huko anarudi kwake hivyo hakuwa na maingiliano sana na wenyeji.

Mzee huyu alipewa majina mengi tu ambayo kwa kweli hayakuwa mazuri.
Bahati mbaya alifariki ghafla na baadhi ya jirani walikwenda msibani[ kwani naye alikuwa anafanya hivyo pia]. Ikatokea kuna bibi mmoja jirani ya nyumba ya marehemu alilia kama vile amefiwa na mwanawe na katika udadisi ikagundulika kuwa yule mzee alikuwa ndiye anamsaidia yule bibi pamoja na wajukuu zake ambao wote walifiwa na wazazi wao.

Kumbe marehemu ndiye aliyekuwa msaada wa hali na mali kwa ile familia bila ya wengine kufahamu. Mwisho wa siku wengi tu jirani ilibidi wainamishe vichwa vyao kwa kujuta kumnanga marehemu kuwa anaringa sana.'TENDA WEMA NENDA ZAKO'
 
Waswahili tuna tabu sana, mimi pia yalinikuta kuonekana naringa kisa nikipita nimefunga vioo mitaani! Wanataka usalimie kila nyumba kama unatembea kwa miguu, ila nilipowasoma nikaenda nao sawa ķuwanyenyekea wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waswahili tuna tabu sana, mimi pia yalinikuta kuonekana naringa kisa nikipita nimefunga vioo mitaani! Wanataka usalimie kila nyumba kama unatembea kwa miguu, ila nilipowasoma nikaenda nao sawa ķuwanyenyekea wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
'When in Rome do as the Romans do'
 
Mkuu hongera umezunguka Sana kutunga story tumeshajua kumbe una Gari!!!!!
Nyumbani kwetu sikukuta gari wala pesa ila ndani ya miaka 27 nilishakuwa na gari langu mwenyewe, na hii ilichangiwa sana na kupenda michezo ya magari na marafiki zangu wengi walikuwa na sports car ziwe zao au za nyumbani kwao.
Nilijituma tu na kuwekeza na hapo nilikuwa naishi nyumba ya kupangisha na nilibadili sana magari kwa mtindo wa kuuza na kununua kufuata fashion na ilifika wakati nikawa na matatu uwani na hapo waswahili wakaanza kelele kuwa nina magari naishi nyumba ya kupanga ndipo nikaangusha mjengo, umeelewa?
Magari ni vitu vidogo sana na vinajadilika msiogope kujadili, sasa hivi umri umekwenda nina familia sioni tena gari ni jambo la ajabu kama awali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
katika vitu nilivyojaliwa na mungu ni uwezo wa kuua nyoka,hata awe mkubwa vipi akishaingia kwenye 18 zangu hawezi kuwa salama abadan pole sana.
 
Akhsante sana mkuu kwa ushauri mzuri, siyo saa nne ni saa nane.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akhsante sana mkuu kwa maelezo mazuri, nitafuata njia zako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…