Jana nimeng'atwa na nyoka mguuni!

Antivenom ni ghali kiasi kwa huko bongo bei yake yafika 200k pia kuwa na Antivenom hakukupi uhalali wa kupona baada ya Shambulio sababu kuna yapaswa ujue umeshambuliwa na specie gani ya nyoka pia unapochoma yapaswa uwe na Adrenaline Pembeni kuzuia Anaphylatic reaction nikimaanisha hutoweza kujichoma pia kama watu wajichomavyo Insulin! Mwisho nikutaarifu tu sio kila nyoka anayo Anti-venom ila kwa sababu ya ukanda uliopo yaweza kuwa rahisi kujua walau ni jamii gani hupatikana ukanda fulani na ukanda fulani kama ambavyo ipo kwa wanyama wa kawaida tu
 
Thnx mukenya,ujuee hapa bongo jua vile ni kali kuna yapaswa kujua pesa mfukoni nakauka kabisa!!!!!
 
Kipindi Niko shule msingi nilishawa kung'atwa na green mamba! Nilipooza mwili mzima macho tu ndiyo yalikua yanaona ila kwenye dark mode!

Thanks to my teacher mallya alihakikisha napata tiba haraka
 
Mama alipo sema nipelekwe hospital
Nikasikia Watu wanasema hospital Hakuna dawaa ya nyoka....
Hapo
Ndipo hofu na woga ulipo zidi sikutamani kuiaga dunia huku najiona live......
Inaonekana ilikuwa miaka mingi nyuma, sasa hivi dawa za kuzuia sumu ya Nyoka kusambaa mwilini zipo hospital.
 
kuna elimu niliwahi kupataa kuhusu nyokoka ni kwambaa!!

1: kuna nyoka aina mbili kuna wale wenye kichwa cha pembe tatu- hawa nyoka wana sumu sana , ikitokea umeumwaa na huyu nyoka basi wahi hospitalini sana na uwaeleze ni aina gan ya nyoka.
2: pia kuna wale wenye kichwa mduara hawa hawana sumu kivile, ilq ikitokea umeng'atwa na hawa pia nenda hospitalini na pia uwaambie aina ya nyokaa.
 
Vipi maumivu yake?na kwanin ulimuacha aende ulitakiwa umuue
 

Weka picha[emoji849]
 

Usingetoa pesa ungekuwa na tatizo? Yaan mpaka pesa ndio uonekane mzuri
 
Ondoa Nge hapo. Nge akikugonga maumivu yake hata usipoweka dawa yadumu 24 "hours" halafu yanaaondoka yenyewe ghafla. Ila huyo mwingine naogopa hata kumtaja maana wanasema ukimtaja taja sana huchelewi kumukuta mguuni kwako.

Hahahaha
 

Tukiumwa na nyoka tujitibu na nini?
 
Vipi maumivu yake?na kwanin ulimuacha aende ulitakiwa umuue
Hamaki ilikuwa kubwa sana na huku nikifikiria hatma yangu hasa nikizingatia ni usiku wa maanane.
Maumivu yake hapo kwa hapo si makali ila kadri sumu inavyopanda ndiyo kimbembe.
 
Usingetoa pesa ungekuwa na tatizo? Yaan mpaka pesa ndio uonekane mzuri
Yapo mambo automatically yanahitaji pesa na wenzako wote wanatoa, sasa wewe usipotoa na ni mgeni hii inamaanisha umekataa taratibu ulizozikuta na ni sawa na kukataa ushirikiano hivyo huleta hali ya kuonekana mbaya. Unanielewa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…