Pole sana.. Umenikumbusha miaka michache nyuma workmates wangu walikuwa Wana kawaida ya kuja kwangu mara kwa mara hasa weekends.....siku moja tukawa twala zenu nyama tumechoma wenyewe tupo kama wa nne hivi..then secretary wetu akaibuka moja kwa moja akaja mezani na kuanza kula nyama...asha bugia kadhaa akisifia nyama ndio nikakumbuka kwake ile ni haramu, nilishindwa mzuia nikakaa kimya maana sikuwa na jinsi. Baada ya siku tatu akauliza lini tena Kuna nyama aje? Jamaa mngine akaropoka mara nyingi kitimoto twala weekends tu....Daaah dada akabadilika sura na kukuuliza ina maana nilikula kitimoto? Basi alitapika sana tu that day. Tukanuniana wiki nzima but baada ya hapo...... Kama kawa tu.