Kumbe madereva wa maschool bus nao wameechangamka!!!
Habar za usiku huu lafamilia,kama kawa mtaa ni mmoja tu ndani ya jf,Usiku wa Manane yes the place to be
Kumbe bwana hawa madriver wa hizi bus nao wana ulimwengu wao linapokuja swala la mapenzi, nao wana mambo ambayo yapo underground lakini sio poa kabisa
Ni mwanaume ambaye bado kijana,alikutana na mkewe ambaye ni nesi , kwa mujibu wa mke wa huyu driver anasema alikutana na huyu jamaa akiwa kama chokoraa,hana maisha hana direction
Hata vaa yake ilikuwa shida,lakini mwanadada aliamua kuwa na jamaa,akamtakatisha akamleta nyumbani kwake na mwisho wa siku akamtafutia sehemu ya kutafutia ridhiki,ni hapo shuleni
Wana watoto wawili,mke anasema amekuwa akitongozwa sana huko nje na wanaume lakini alikuwa anawaambia ana mume wake hivyo wamuache,yes ndoa iheshimiwe
Lakini guess what? Huyo mume mwenyewe sasa hafai hata kula nae chips kavu, yes ameshindikana
Mchongo uliwekwa ubaoni kupitia meseji ambazo zilikutwa kwenye simu ya school bus driver,hakika mke hakuamini kwamba ndio huyu jamaa niliyekutana nae kama chokoraa au huyu ni mwingine
Zimekutwa meseji za walimu kadhaa ambao ametembea nao,akiwemo naibu mwalimu mkuu
Halafu karibia walimu kama watano au sita kawatia mimba,halafu kisha anawa block,lakini kiujumla kalala na walimu kama 10 flani hivi
Mwalimu mmoja meseji yake ilisomeka "najua mimi ni mgeni hapa,umenidanganya kuwa upo single kumbe umetembea na fulani na fulani,ila mimi sitasema kitu"
Mwengine alisomeka akisema 'nilikwambia usimwage ndani ona sasa Asante kwa kunipa mimba,ila sitatoa kama wengine walivyofanya"
Hizo ni meseji chache tu nimekudokolea, daaah kuna watu wanauza mechi kama kawaida tu wala hawajali kabisa
Kibaya zaidi wakati wanatoka lunch, mke alikuwa na best yake ambaye mara nyingi huja home kwao,na ni mtu wa karibu sana,ingawa nae ana mume wake, lakini katembea na huyo school bus driver ambaye ni mume wa rafiki yake,dah mke anabaki kulalamika tu "yani wewe ni best yangu hata hapa tumetoka kula lunch pamoja na mume wangu,kumbe unatembea nae"
View: https://youtu.be/tTX-9PhQGzA?si=s-KoSgbFoEd6Pvzi
Mwisho wa siku mke kasema huyo rafiki yake wasijuane tena,na mume kaambiwa atoke nyumbani kwa mke,akaanze maisha yake huko kwingine maadamu ana kazi sasa, ingawa mume alikaza kwamba wataenda home wakayajenge
Alamsiki