JamiiForums Usiku wa manane

JamiiForums Usiku wa manane

Mdogo mtu amkaribisha dada yake aijistiri kwa muda ambaye ameachika kwenye ndoa mbili,lakini kama haitoshi akatembea na shemeji yake

Hakika duniani kuna mambo,dunia haipoi huku vita huku mapenzi yana wanyooosha watu,huku wachawi nao wanatusumbua ilimradi tuwe bize

Ni dada ambaye anaishi na mume wake ndani ya chumba kimoja na sitting room,wakiwa wana ndoa ya miaka miwili na dogo wa mwaka mmoja

Kama unavyojua damu ni nzito kuliko maji, mke akaamua kumhifadhi dada yake ambaye ndoa yake imeparaganyika,kwa makubaliano kwamba aje kukaa kwa mwezi mmoja,lakini mpaka hili tukio linatokea tayar da mtu yupo pale ni miezi sita sasa.

Kama kawaida host wa kipindi pamoja na mambo mengine huwapa challenge wanandoa au wapenzi,this time alitoa dau la vocha ya 10,000 ya Kenya kwa ajili ya shopping, kibongo bongo ni hela ndefu kidogo

Simu ya mke ikapekuliwa ipo clean,sasa ilipokuja zamu ya simu ya mwanaume kupekuliwa,mwamba kwanza akajifanya kama anapigiwa simu hivi,watu wakamshtukia,mkewe akamshikia kidedea kwamba leta simu yako ikaguliwe,mwamba akawa hana jinsi

Host kuchek simu hakukuwa na call yoyote iliyopigwa daadeki,mwamba aibu hii hapa

Host kaicheki simu haipo Clean,so kama kawaida akamchukua mke na kwenda nae pembeni kusoma hizo text

Ikasomeka meseji kutoka kwa mume kamtumia dada wa mkewe "leo natoka mapema nije nikukule"

Da mtu naye akajibu "Tena ukuje maana imekaa wik mbili sasa ni muda mrefu inakuwa na kutu" kwa maana ni wiki mbili sasa haujaichapa inaweka kutu

Kuna text nyingine ilisomeka "leo ukija uje ped' jamaa akasema mi sijuiagi hivyo vitu,akaambiwa ukofika dukani niambie niwaeleweshe

Kumbuka mke anasema yeye hutumia vitambaa hajawahi kununuliwa pedi

Baada ya hapo mke na host wakaenda kwa mume kwa ajili ya maswali,ambaye kwa sasa mume huyu tumuite mbwa.

Wakati huo huo mke alimpigia dada aje hapo barabarani maana sio mbali sana na kwao, dada amefika pamoja anaulizwa inakuwaje unatembea na shemeji yako,kama kawaida akakaza kwamba haiwezikani,akataka asomewe meseji,akasomewa pamoja na yule mbwa wa kiume

Mke kacharuka balaa haelewe natamani ungecheki video uone timbwili lake,huku na huku,mume anasema ujue toka awali sikutaka huyu shemeji akae hapa,tulikubaliana mwezi mmoja lakini now ni six months

Mi wala sina amani na nyumba yangu,nashindwa hata kuangalia Tv kwasasa kwakuwa wao wapo Sebuleni,na watoto wa shemeji wamevunja TV pia,mume ambaye ni mbwa pamoja na anayoyasema kwahiyo ndio amelipiza kwa kumkula dada wa mkewe? Au anatafuta sababu tu ya kujisafisha?

Mwisho mume anasema hata yule mtoto aliyezaa na mkewe sio wake,mke akasema host mimi nakaa pale juu twende ukamuone mtoto kama hafanani na baba yake

Mke akamlaumu tena dada yake kwanini umetembea mzee wangu unaona sasa hata anasema mtoto sio wake.

Mwisho wa siku mke kasema hataki kumuona dada yake nyumbani wala mume wake,na alikuwa anaenda home kutoa vitu vya dada yake

Dada mtu ndoa mbili zimemshinda kama haitoshi ameenda kuharibu ya mdogo wake

Hayo ndio mapenzi bwana ni hatari sana,je bado unaamini kuna watu wasafi asilimia 100? Mwenzenu kadri ninavyoangali haya matukio ya wanandoa na wapenzi nakuwa na mtazamo tofauti sana juu ya upendo wa kweli

Kama leo nipo kwenye daladala,kuna jamaa kakaa na mrembo fulani wanaonekana wako happy hivi,ila kimoyo moyo nikasema hapa kuna mtu hayupo clean kabisa,ni vile tu moyo unaficha mengi


View: https://youtu.be/kgnhnzBBh98?si=X1_ATaCkgh458Dy7

Alamsiki!

So
 
Back
Top Bottom