Jamii yetu inakubali hili?

Kweli

JF-Expert Member
Jul 14, 2007
1,152
302
Hii nimeikuta kwenye Blog ya faza Kidevu na kwa kweli nimekasirika na kusikitika sana kuona kweli Tanzania Mama anaweza kumpa mtoto kileo katikati ya watoto wanaosherehekea sikukuu na ionekane ni kiburudisho?
Tena huyu Mama anajisifia hili!! Jee hakuna sheria ya kumuadhibu Mama kama huyu? Anasema Mtoto anaondoka na safari 2 bila kulewa?
Ni tuseme haelewi kuwa anachokifanya ni kuvunja sheria?

Mama.jpg

Laga.jpg
 
Good Lord! What is this world coming to? I wonder what whoever took the photo did after witnessing this outrageous act, and were there no other sober adults around?
 
sheria ya kileo nadhani inakataza kuonja kama sio kunjwa kilevi kama una umri chini ya miaka 18.Kwa hiyo huyu mama anatenda kosa na anapaswa kushitakiwa kwa kuvunja sher/amri hii kwa kumpatia mtoto aliye chini ya umri unaoruhusuwa.
 
Hii nimeikuta kwenye Blog ya faza Kidevu na kwa kweli nimekasirika na kusikitika sana kuona kweli Tanzania Mama anaweza kumpa mtoto kileo katikati ya watoto wanaosherehekea sikukuu na ionekane ni kiburudisho?
Tena huyu Mama anajisifia hili!! Jee hakuna sheria ya kumuadhibu Mama kama huyu? Anasema Mtoto anaondoka na safari 2 bila kulewa?
Ni tuseme haelewi kuwa anachokifanya ni kuvunja sheria?

Mama.jpg

Laga.jpg

Tuwacheni uchochezi usiokuwa na faida wala manaa inawezekana huyo mamam alimpa mtoto aonje hiyo beer na sio kwaleo la kumlewesha ukiangalia hata hao wazungu tunaowaiga jinsi ya kuishi na starehe wamekuwa wakiwapa watoto zao kwenye vigilasi kiasi kidogo kama ni beer au wine waulizeni kama watakataa hilo kwakua nchi sasa inafuata mila ya uhaibuni ndio tukubali mabadilisho ya tamaduni yanakuja hayo
 
Kumuonjesha mtoto kilevi ni kosa. Kwa kuwa watu wengi na wazungu pia wanawapa wana wao pombe basi nasi tuwape ? Je sio wazungu hawa hawa wanaotaka wana wao wafike 18 yo ndio waanze kunywa pombe na kufanya starehe nyingine kama kwenda disco na pengine kuvuta sigara ?
 
Tuwacheni uchochezi usiokuwa na faida wala manaa inawezekana huyo mamam alimpa mtoto aonje hiyo beer na sio kwaleo la kumlewesha ukiangalia hata hao wazungu tunaowaiga jinsi ya kuishi na starehe wamekuwa wakiwapa watoto zao kwenye vigilasi kiasi kidogo kama ni beer au wine waulizeni kama watakataa hilo kwakua nchi sasa inafuata mila ya uhaibuni ndio tukubali mabadilisho ya tamaduni yanakuja hayo
Kule kwenye source ya hii habari kwa Father Kidevu wamesema Mama ndie aliyethibitisha kwamba huyo dogo anapiga tarumbeta chupa 2 za safari, hii sio kuonja na kutamsababishia madhara huyu mtoto kama ataendelea.

Laga-1.jpg
 
Tuwacheni uchochezi usiokuwa na faida wala manaa inawezekana huyo mamam alimpa mtoto aonje hiyo beer na sio kwaleo la kumlewesha ukiangalia hata hao wazungu tunaowaiga jinsi ya kuishi na starehe wamekuwa wakiwapa watoto zao kwenye vigilasi kiasi kidogo kama ni beer au wine waulizeni kama watakataa hilo kwakua nchi sasa inafuata mila ya uhaibuni ndio tukubali mabadilisho ya tamaduni yanakuja hayo

Sipendi kukandia watu. Lakini watu wenye mawazo kama haya ndiyo waliotufikisha hapa tulipo! Huyu mtoto anaonja pombe ili iwaje? Halafu kwa kupiga tarumbeta! Mkuu, unasikitisha na kutia aibu.
 
Huko ughaibuni, huyu mama angemsikia mtoto wake kwenye redio tu maana hastahili sifa ya umama. Ati anaona sifa mtoto wake kuweza kunywa chupa mbili za safari! Na si ajabu umekuwa mradi. Watu watoa dau ili mtoto afanye kweli! Halafu bila aibu tunalalamikia watoto wetu wakivaa tunachoita vichupi! Hiyo tunaona ni uovu kuliko kumnyeshwa mtoto mchanga Safari!
 
Sisi kule kwetu tunazoka ulanzi tangu tukiwa hatuna fahamu vizuri.
Ulanzi kwetu si pombe kwa sababu ni ulanzi.
Pombe kwetu ni ile ya kupika kwa kutumia kimea.
Huko ni kwetu.

Tanzania tuna desturi ya kuto wapa pombe watoto, lakini sidhani kama kuna sheria ya kumbana mtu mahakamani kuhusu kumpa mtoto ulabu au pombe.
Mara nyingi mtu huzuiwa kunywa pombe akiwa shule,wale wenye umri sawa na yeye lakini hawako shule ni pombe mtindo mmoja, akihitimu hakuna anaye mruhusu wala anaye mkataza.
Kuna unafiki mkubwa sana kwenye suala la pombe.

Pili pombe ni nini?
Ulanzi,lubisi na mbege nazo ni pombe!!?

Sasa hiyo ni Bia, kuna wanao wapa watoto wao Konyagi mwitu ( Gongo).
Kuwapa pombe watoto hatuwaigi wazungu kwa sababu pombe hawakutufundisha wao kutengeneza wala kunywa .

Mila yetu kitaifa juu ya pombe haiko wazi, inautegemezi kwamba mzazi au mlezi anajisikiaje akiona mtoto wake ana kata kiu kwa ulabu.
Kazi ipo.
 
Mara nyingi watoto walikuwa wanapewa kinywaji ambacho hakija-ferment. Pamoja na hayo, si mila zetu zote zinastahili kuenziwa. Mara nyingi tunapenda kuwasingizia wageni kuwa wao ndiyo wametufundisha maovu wakati si kweli. Jamii zote duniani zilikuwa na mila ambazo hazikubaliki katika dunia ya leo. Hii ya kuwapa ulevi watoto ni mojawapo zisizo kubalika hata kwa mtazamo gani!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom