Jamii imempora mwanamke nafasi yake


Kumbe kuiongelea sana jinsia fulani ni viashiria vya chuki/maumivu fulani dhidi ya jinsia hiyo?

Fikra zingine hizi
 
Here is another fact for you: Enzi za kumnyima mwanamke elimu na mali ili mwanaume amtawale zimeisha
 
Mimi sio muandishi mzuri lakini napenda nichangie kwa kusema miongoni mwa mada ambazo zimenigusa ni hii, na mimi ni muhanga wa mfumo huu ulioasisiwa huko Beijing nchini China wakiwiita haki sawa kati ya mwanamke na mwanume, nimesoma wachangiaji wengi kiukweli ninawaunga mkono. Jamii yetu imeingia kwenye shida kubwa ikiamini kumuelimisha mtoto wa kike ndio suluhisho la kuondokana na kunyanyaswa, kudhurumiwa, kuonewa na mengine yanayofanana na hayo.
Lakini matokeo yake Jamii imejaza wanawake wenye kiburi na jeuri kwa sababu tu wanaamini kupitia elimu (kazi) zao wanaweza kufanya wanachokitaka wao hivyo ile heshima ya mwanamke kwa mwanume haipo tena.
Pia mmomonyoko wa maadili kwa watoto umekuwa mkubwa kwani malezi ya wazazi hayapo tena zaidi ya kutegemea wasichana wa kazi kwa wale walioko majumbani lakini pia kutegemea walimu na walezi walioko mashuleni hususani kwenye shule za boarding.
Hii inaendelea kutengeneza wanawake ambao sio wife materials kwani unaweza kuta mtoto wa kike mpaka anafika form4 hajui hata kupika wala kufua nguo zake kwakuwa tayari ameshajengewa mfumo wa kuwa yeye ni mtafutaji na sio mtu wa kufanya kazi fulani, kwakuwa muda wote huo majukumu ama kazi alizopaswa kufanya km mtoto wa kike zinafaywa na walezi a wapo shuleni ama mdada wa kazi a wapo nyumbani.
Inasikitisha sana kuona Jamii yetu inapotea huku tukiendelea kupiga makofi kwa kuimba wimbo wa haki sawa, tuombe neema ya Mungu watu wapate ufunuo kufunuliwa juu ya angamizo hili. Mwenye masikio na asikie.
 
Mkuu umeongea ukweli mtupu hawa viumbe likija suala la pesa kwao ni km hakuna mwisho wa dunia wala hawatakuja kuiacha hii dunia.
Maandiko yanasema nchi na vyote viijazavyo ni Mali ya Mungu dunia na wote wakaao ndani yake.
So wanawake wanapaswa kufahamu kuwa pesa na mali ni vitu vya kupita na mwisho wa siku tutaviacha hapahapa duniani lkn je heshima ya mwanamke katika family na jamii kwa ujumla iko wapi.
Utafutaji huu wa mwanamke umempa kiburi kiasi kwamba yeye haoni umuhimu wa kuwa na mume isipokuwa tu pale ambapo anaweza kutumia nguvu yake ya kiuchumi kummiliki mtu anayemtaka. Inasikitisha sana.
 
Madam katika jamii yetu hii ni ukweli ulio wazi wanawake wanaoishi maisha ya furaha na uhuru wa nafsi ni wanawake wa aina yako ambao wanakubali kukaa kwenye nafasi yao ya uanamke na sio hawa ambao wako bize kutunishiana misuli na wanaume.

Hawa wanawake wenzio wanaojifanya ni ma Alpha females wengi wao wamejaa visirani, uchungu rohoni na chuki kali sanan dhidi ya watu wengine hususani wanaume. Kwa sababu muda wote wako kwenye battle of Supremacy na pale inapotokea jamii kuwachukulia hawana kitu chochote special kulinganisha na wanawake wengine hali hiyo uwajaza hasira sana, maana akilini mwao wanajiona sio wanawake wa kawaida tena.

Mwenyezi Mungu hakuwa mjinga kutuumba tukiwa na hizi tofauti tulizonazo, kuna mambo ambayo yapo kwa ajili ya kufanywa na mwanamke tu, pia kuna mambo ambayo yapo kwa ajili ya mwanaume tu na kwenda kinyume na hapo ni kuishi kinyume na makusudi yake.
 
Asante mkuu kwa kulitambua hilo.

Hawa wanaamini pesa na mali ndio kusudio la wanawake wengi kuolewa, kwa hiyo akiwa navyo hivyo basi hata mwanaume/kuolewa kwake sio suala muhimu tena.

Yaani iko hivi pesa/mali=mwanaume

Ukiwa navyo hivyo basi tayari una mwanaume ndani. Inafurahisha na inasikitisha.

Si umeona kuna mmoja kule mwanzo kasema ukishakuwa na uhuru wa kiuchumi tu(pesa) unaweza hata kumnunua mwanaume, haya ndio mawazo ya wanawake wa kileo kwamba tafuta pesa mambo mengine yatakuwa ni ya ziada tu.

Cha kushangaza pamoja na pesa zao lakini kuna mambo mbali mbali ya Kijamii kama malezi wamefeli vibaya mno.
 
Umeongea vitu vizito sana bro!! Yaani vizito mno ni maneno machache tu lakini yamekusanya scenarios kibao zenye ukweli mtupu.
 
Madam kama Mungu angekuwa anataka tuwe sawa basi hakuwa na haja ya kutuumba na hizi tofauti zetu tulizonazo ambazo ndio zimekuwa msingi wa mgawanyo wa kimajukumu.

Kama angetaka tuwe sawa hakuwa na haja ya kumfanya mmoja awe dhaifu kimwili kuliko mwingine.

Kama angetaka tuwe sawa basi wote angetupa adhabu zinazofanana.

Leo hii tunalazimisha usawa lakini nature inatuhukumu. Na uzuri wa nature inatuumbua bila kificho.

Sasa hivi yale masuala ya kupewa vipaumbele kwa kuangalia jinsia hayapo tena kwenye matukio mbali mbali. Na hata kama yapo basi ni kidogo na yanaenda yanaisha.

Kadri siku zinavyozidi kwenda wanaume nao wanajifunza kwenda sawa na huu mfumo mpya.

Wanawachukulia wanawake kama wanaume tu. Mimi mwenyewe ni mmoja wapo ambaye tayari nimeanza kuwachukulia wanawake kama ninavyowachukulia wanaume tu.

Leo hii ikitokea vita ya tatu ya dunia nakuhakikishia kila mtu anapigania kuokoa maisha yake tu.

Na wala hakuna mwanaume atakaye sacrifice maisha yake kwa ajili ya wanawake na watoto kama ilivyokuwa imezoeleka miaka ya nyuma.

Huu mfumo umekuja kutusaulisha kabisa kama kuna dini na kuna wengine umewaondolea dini kabisa, wanaona dini ni nyenzo ya ukandamizaji, utakuta wanakwambia vitabu vya dini vimeandikwa na mwanaume kwa maslahi yake binafsi halafu cha ajabu hawawezi hata kuthibitisha haya madai yao.
 
Umeongea point aisee....umetema madini
 
Mkuu umeongea mambo halisia yanaendelea kwenye baadhi ya familia zetu. Binafsi sometimes huwa na-regret kuoa mke msomi, maana sioni faida yake kiukweli masaa mengi yuko bize na mambo yake hana muda hata na watoto. Lakini pia mwisho wa siku faida ya kazi zake hizo kwa familia ni very negligible.

Yaani kwa uzembe wake kwa watoto ilifika pahala nikahamua kuwa narudi nyumbani mwenyewe mapema ili nikague school works na kuwasimamia watoto wafanye homeworks.

Nilifikia uhamuzi huu baada ya kumsihi afanye hivyo yeye bila mafanikio, wakati huo mimi navipenda kweli vitoto vyangu hivi vi3 na pia ninavilipia hela yangu nyingi ninayopata kwa shida ili visome!

Nikaona bora nijitoe tu muhanga nivisaidie maana kwa upande wangu kama ni kukosea/kupatia maisha kidogo kuna muelekeo ila kwa hawa watoto bado sana kulijua hilo hivyo inabidi kuwasaidia kadri iwezekanavyo hata kama ushirikiano wa bibie ni mdogo.
 
bora huja over react.. 😅 😅 😅


Mimi sitaki uchokozi na mtu siku hizi.
Mnanichokoza lakini hamnipati ng'oo!

Wewe Rebeca 83 na wenzako mnachokitafuta kwangu mtakipata.

Khantwe
Karma ambaye ndiye Marianah
Lady Red
Hamnipati ng'ooo.

Kwanza Rebeca Njoo Pm
 
Mimi sitaki uchokozi na mtu siku hizi.
Mnanichokoza lakini hamnipati ng'oo!

Wewe Rebeca 83 na wenzako mnachokitafuta kwangu mtakipata.

Khantwe
Karma ambaye ndiye Marianah
Lady Red
Hamnipati ng'ooo.

Kwanza Rebeca Njoo Pm
Aah na mimi tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…