Pole kwa habari ya Wembley. Kupata watu wenye sauti ya kama Jamea Earl Jones (Baba wa Eddie Murphy kwenye Coming to America) na akawa anazungumza Kiingereza kizuri ni kazi kidogo huku kwetu. Yawezekana wapo wanaokaribia kiwango chake. Wadau watasaidia.
Sound Effects (SFX) za 20 gb ni sawa na huna kitu. Namaanisha ni nyingi sana kiasi kwamba kama haujazipanga vizuri huenda usikumbuke ipi iko wapi.
Hiyo clip yenye logo..... uko sharp. Naona fasta umekuja na idea. Kazi nzuri. Ijazie "nyama" sasa. Cha kujazia....... changamsha bongo kwanza, naona kama kichwa yangu haijakaa vizuri kwa sasa. Congrats and all the best. Nikipata muda nitajaribu kurusharusha miguu nije na clip japo ningependa sana kupata rough idea ya requirements toka kwa mods kuliko kuwa general halafu in the end iwe "sivyo tulivyotaka.".