James Mbatia: UKAWA ipo imara, haitasambaratika, akerwa na kauli za Magufuli, CCM

Nilikua namuheshimu baregu hivi unawezwaje kuandaa tathmimi mbovu hivi au ndiyo kukalia au kuzikodisha alkali kwa jambazi lowassa huku.
Safari za jk wakati wa kampeni inasaidia nini, kupoteza muda kumuongelea jk mtu ambaye tayari wananchi na chama chake chenyewe kimemtenga na kumchoka ni kupoteza muda tu na cheap propaganda za kuhadaa watu . Wangeongelea ilani yao lowassa aliyosema ipo kwa tovuti, wangeongelea na ahadi zao na summary ya kampeni mikoa yote waliyopita hadi sasa na watu wa ngapi, viongozi wa ngapi Mae neo hayo wamehamia ukawa, specifics za kampeni siyo upuuzi wa mtu anayeondoka na ambaye hata ikimuattack tayari watu wanamchukia na hupati extra points..

Mdahalo tu nahitaji lowassa awepo na magufuli siku ya mwisho Kabla ya kupiga kura.
CCM OUT.Hakuna porojo hapa....
 
Hakuna ubaya kuchagua pasipo kuona lakini usizuie wengine kufahamu hoja za wagombea!hatuengi kuchagua chama ndio maana kuna wagombea wa ubunge na udiwani vinginevyo tungechagua chama then kiteue madiwani na wabunge!Kwa hiyo hakuna budi kuwaleta wagombea tuwasikilize kama mtu hawezi kusimama apewe kiti akae lakini aje ajibu hoja za watu!

Zilongwa mbali zitendwa mbali.
 
Hvi una cheo gani hapo lumumba? Naona kina Uwoya Wema sepetu wanapewa kipaumbele wakati mkongwe umetelekezwa au huoni kwamba hata kwa hao CCM HUAMINIKI?
Yawezekana ndio W. Sepeta mwenyewe mana jamaa walimng'ata sikio ili asiache baada ya kutoswa. ajing'ang'anize hiv hiv mzee wa kilaji kama akitinga
ikulu atapewa kapost. akaongeze chachandu Dom
 
Mbatia asubiri ubunge wa kuteuliwa na Magufuli kwani Vunjo hawezi shinda kamwe!

Hongereni Chadema kusaidia kuua upinzani nchini na ️️hapo mmefanikiwa sana! Songela zigizigi

babaoko kikwete kapata utapiamlo wa ghafla kachoka mbaya anasumbuliwa na woga kwani akiingia magufuli ni mbaya kwake akiingia Lowasa ndo mbaya pia nimesikia wameanza kuuza majumba yao
 
Mwenyekiti Mwenza Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), James Mbatia, ameibuka na kudai kuwa Rais Jakaya Kikwete amekuwa akisafiri zaidi na kutumia muda mwingi akiwa nje ya nchi kuliko nchini katika kipindi chake cha takriban miaka 10.

Vyama vinavyounda Ukawa ni NCCR-Mageuzi, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), NLD na Chama cha Wananchi (CUF).

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi, Mbatia alidai kuwa katika kipindi hicho cha miaka 10 chenye wastani wa siku 3,650, Rais Kikwete amesafiri mara 409 na alikuwa akikaa nje ya Tanzania kwa wastani wa siku tano katika kila safari, hivyo jumla kuwa siku 2,045. Alisema siku hizo ni sawa na asilimia 56 ya muda wake wote akiwa madarakani hadi kufikia sasa.

Akifafanua zaidi, Mbatia alisema wastani wa gharama ambazo taifa imezibeba kutokana na safari hizo ni Sh. trilioni 4.5.

Alisema kiasi hicho cha fedha alichotumia Rais katika safari zake kingetosha kutoa elimu bure kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, kujenga hospitali na pia vyuo vya ufundi.

Alitaja idadi ya vyuo vya ufundi vinavyoweza kujengwa kuwa ni 200, vyuo vikuu 80 na pia kiasi kingine kingeweza kujenga hospitali za rufaa.

Kwa mujibu wa kitabu cha makadirio ya idadi ya watu na wapigakura kilichotolewa Machi, 2015 kwa ushirikiano wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Zanzibar, Tanzania itakuwa na watu 48,522,228 kufikia mwezi ujao.

Hivyo, kwa kiasi alichokitaja Mbatia kuwa kimetumika kwa safari za nje za Rais Kikwete, maana yake ni kuwa kila Mtanzania angeweza kupata wastani wa Sh. 92,741 ikiwa zingegawiwa kwa kila mmoja. Kadhalika, kwa mujibu wa ripoti ya NBS ya Machi mwaka huu, wastani wa pato la kila Mtanzania kwa siku ni Sh. 4,724.

Alipoulizwa jana kwa njia ya simu kuhusu madai hayo ya Mbatia, Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue, hakupokea na badala yake akajibu kwa njia ya ujumbe mfupi (sms) 'I'm busy and i can't take your phone'. Ujumbe mwingine aliojibu kupitia simu yake ulisema 'siwezi kujibu naendesha kikao'.

Unaweza pia kupitia hapa zaidi.

Chanzo: Nipashe

mwenyekiti mwenza umoja wa katiba ya wananchi (ukawa), james mbatia, ameibuka na kudai kuwa rais jakaya kikwete amekuwa akisafiri zaidi na kutumia muda mwingi akiwa nje ya nchi kuliko nchini katika kipindi chake cha takriban miaka 10.

Vyama vinavyounda ukawa ni nccr-mageuzi, chama cha demokrasia na maendeleo (chadema), nld na chama cha wananchi (cuf).

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini dar es salaam juzi, mbatia alidai kuwa katika kipindi hicho cha miaka 10 chenye wastani wa siku 3,650, rais kikwete amesafiri mara 409 na alikuwa akikaa nje ya tanzania kwa wastani wa siku tano katika kila safari, hivyo jumla kuwa siku 2,045. Alisema siku hizo ni sawa na asilimia 56 ya muda wake wote akiwa madarakani hadi kufikia sasa.

Akifafanua zaidi, mbatia alisema wastani wa gharama ambazo taifa imezibeba kutokana na safari hizo ni sh. Trilioni 4.5.

Alisema kiasi hicho cha fedha alichotumia rais katika safari zake kingetosha kutoa elimu bure kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, kujenga hospitali na pia vyuo vya ufundi.

Alitaja idadi ya vyuo vya ufundi vinavyoweza kujengwa kuwa ni 200, vyuo vikuu 80 na pia kiasi kingine kingeweza kujenga hospitali za rufaa.

Kwa mujibu wa kitabu cha makadirio ya idadi ya watu na wapigakura kilichotolewa machi, 2015 kwa ushirikiano wa ofisi ya taifa ya takwimu (nbs) na ofisi ya mtakwimu mkuu wa zanzibar, tanzania itakuwa na watu 48,522,228 kufikia mwezi ujao.

Hivyo, kwa kiasi alichokitaja mbatia kuwa kimetumika kwa safari za nje za rais kikwete, maana yake ni kuwa kila mtanzania angeweza kupata wastani wa sh. 92,741 ikiwa zingegawiwa kwa kila mmoja. Kadhalika, kwa mujibu wa ripoti ya nbs ya machi mwaka huu, wastani wa pato la kila mtanzania kwa siku ni sh. 4,724.

Alipoulizwa jana kwa njia ya simu kuhusu madai hayo ya mbatia, katibu mkuu kiongozi, ombeni sefue, hakupokea na badala yake akajibu kwa njia ya ujumbe mfupi (sms) 'i'm busy and i can't take your phone'. Ujumbe mwingine aliojibu kupitia simu yake ulisema 'siwezi kujibu naendesha kikao'.

Unaweza pia kupitia hapa zaidi.

chanzo: nipashe

hakuna tofauti kati ya magufuli na ccm
 
Mwenyekiti Mwenza Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), James Mbatia, ameibuka na kudai kuwa Rais Jakaya Kikwete amekuwa akisafiri zaidi na kutumia muda mwingi akiwa nje ya nchi kuliko nchini katika kipindi chake cha takriban miaka 10.

Vyama vinavyounda Ukawa ni NCCR-Mageuzi, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), NLD na Chama cha Wananchi (CUF).

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi, Mbatia alidai kuwa katika kipindi hicho cha miaka 10 chenye wastani wa siku 3,650, Rais Kikwete amesafiri mara 409 na alikuwa akikaa nje ya Tanzania kwa wastani wa siku tano katika kila safari, hivyo jumla kuwa siku 2,045. Alisema siku hizo ni sawa na asilimia 56 ya muda wake wote akiwa madarakani hadi kufikia sasa.

Akifafanua zaidi, Mbatia alisema wastani wa gharama ambazo taifa imezibeba kutokana na safari hizo ni Sh. trilioni 4.5.

Alisema kiasi hicho cha fedha alichotumia Rais katika safari zake kingetosha kutoa elimu bure kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, kujenga hospitali na pia vyuo vya ufundi.

Alitaja idadi ya vyuo vya ufundi vinavyoweza kujengwa kuwa ni 200, vyuo vikuu 80 na pia kiasi kingine kingeweza kujenga hospitali za rufaa.

Kwa mujibu wa kitabu cha makadirio ya idadi ya watu na wapigakura kilichotolewa Machi, 2015 kwa ushirikiano wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Zanzibar, Tanzania itakuwa na watu 48,522,228 kufikia mwezi ujao.

Hivyo, kwa kiasi alichokitaja Mbatia kuwa kimetumika kwa safari za nje za Rais Kikwete, maana yake ni kuwa kila Mtanzania angeweza kupata wastani wa Sh. 92,741 ikiwa zingegawiwa kwa kila mmoja. Kadhalika, kwa mujibu wa ripoti ya NBS ya Machi mwaka huu, wastani wa pato la kila Mtanzania kwa siku ni Sh. 4,724.

Alipoulizwa jana kwa njia ya simu kuhusu madai hayo ya Mbatia, Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue, hakupokea na badala yake akajibu kwa njia ya ujumbe mfupi (sms) 'I'm busy and i can't take your phone'. Ujumbe mwingine aliojibu kupitia simu yake ulisema 'siwezi kujibu naendesha kikao'.

Unaweza pia kupitia hapa zaidi.

Chanzo: Nipashe

Hata kama wakianika kwani zinamnufaisha nani? ni wao ukiwemo na wewe na mimi, unadhani anaenda kutalii kule nje? acheni wivu, ila mkae mkijua kwamba IKULU mtaishia kuiona kwenye Runinga tuuu hampati nafasi ya kuingia ng'ooooo
 
Kwa hiyo Baba naniliu ameishi nje takribani miaka mitano katika kipindi chote alichowahi kuwa Rais wa nchi hii?
 
Kama hizi safari zina malengo ya kutembeza bakuli kwa wahisani, kwa nini Tz bado ni maskini?
Ina maana bakuli halijajaa?
 
Wataalamu wameshajumlisha safari zote za Rais wetu za kusafiri nje ya nchi tangu aingie madarakani na kupata JUMLA ya miaka 6 kati ya 10, inamaana Rais amekaa ndani ya nchi miaka 4.
Kama hili Lina ukweli nimeshangaa sana tena sana! Nimejiuliza aliyajuaje matatizo ya nchi yake?
 
Back
Top Bottom