James Mbatia: UKAWA ipo imara, haitasambaratika, akerwa na kauli za Magufuli, CCM

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,202
5,012
attachment.php


UPDATES:

Mbatia analalamikia vitisho vya Mgombea wa CCM, Magufuli kuwa wakiwachagua wapinzani nchi itaingia kwenye machafuko

Mbatia: Watu wameanza kupoteza maisha, wana UKAWA wanadhalilishwa na wengine kutekwa

Mbatia: Hali imeanza kuwa tete, vitisho vya kila aina vimeanza. Tumedhalilishwa sana, tumeitwa matusi ya kila aina.

Mbatia: Lowassa si mdini, alikuwa anataka watanzania wamwombee. Mhe. Lowassa hajaenda kwenye nguvu za giza. Hajatumia viungo vya albino, ameenda kuomba viongozi wa dini wamwombee; udini wake unatoka wapi?

Mbatia: Tunawashukuru Lowassa na Sumaye kwa nia zao njema kuja Upinzani kuongeza nguvu ili tuyafanye mabadiliko ya kweli

Mbatia: Hata CCM wangemweka malaika, si rahisi kupata mabadiliko bila kufanya mabadiliko ya mfumo.

Mbatia: CCM wanasema usichague chama, chagua mtu. Watanzania wanatakiwa kujua kuwa Magufuli ni CCM, na hawezi kujitenganisha na CCM. Huwezi kulisukuma gari ukiwa ndani yake, lazima utoke ndipo ulisukume. Mabadiliko ndani ya CCM hayawezekani

Mbatia: Tumefanya utafiti, tuna uhakika wa ushindi mwaka huu

Mbatia: Hatutawapa CCM nafasi ya kufanya machafuko ndani ya Taifa hili

Mbatia: CCM hawana hati miliki ya kuitawala Tanzania hii. Watupishe tufanye mabadiliko haya kwa utulivu na amani.

Mbatia: Sumaye, Lowassa wana uzoefu mkubwa wa kuongoza Serikali, uwezo tunao! Tunao kina Mungai, Msindai, Mgeja n,k na wanao uzoefu wa kuongoza Serikali.

Mbatia: Limeibuka suala la ukabila. Ni aibu iliyoje? CCM wanahubiri ukabila, ukanda bila aibu yoyote!

Mbatia: Ilani ya Uchaguzi ni mkataba kati ya mpiga kura na mpigiwa kura; tuwaulize CCM Ilani yao iliyopita imetekelezwa kwa kiasi gani kabla hawajaja na ilani mpya. UKAWA tunayo ilani ya pamoja

Mbatia: Tunawataka CCM waje tufanye midahalo kwa hoja

Mbatia: Wenyeviti wa vyama wawekwe kwenye midahalo ili UKAWA tupambane na CCM kwa hoja na watanzania wajue pumba na mchele

Mbatia: UKAWA ipo imara, haitasambaratika!

Mbatia anafafanua wapi watapata fedha za kufanikisha yale wanayoahidi kwenye kampeni.

Mbatia anadai Safari za Rais hazikuwa na tija kwa Taifa.

Mbatia: Lowassa na Serikali yake wakiingia madarakani wanao uwezo wa kupunguza kodi kwa wafanyakazi

Mbatia: Tukinyimwa haki yetu kwa mbinu chafu… Hatutaki kuona yaliyotokea Kenya yakitokea Tanzania

Prof. Baregu ametoa ufafanuzi juu ya gharama za safari za JK na athari zake kwa Taifa (pamoja na gharama za kuingilia shughuli za watendaji walio chini yake na kutokuwepo kwake nchini)

Shaweji Mketo (CUF) pia ameendelea kuongelea safari za JK na athari zake kwa Taifa; amegusia pia teuzi zilizofanywa jana na vikao vingine vya kiutendaji vinavyofanywa na Rais Kikwete nyakati hizi.

Mbatia kahitimisha kwa kusema "Tanzania bila CCM Inawezekana"

Asanteni
 

Attachments

  • 20150915_224934-1.jpg
    20150915_224934-1.jpg
    29.1 KB · Views: 57,485
Mwenyekiti mwenza wa UKAWA mh.Mbatia anatarajia kuongea na wanahabari saa nne usiku leo.

mkutano huo utarushwa moja kwa moja na ITV.

siasa za mwaka huu ukisikia kiongozi anaita press presha inakua juu kweli kweli....

sosi ITV.
 
Kuna tetesi zimezagaa kwenye social networks Mbatia ataongea na taifa ifikapo saa nne usiku kupitia ITV mwenye taarifa sahihi atuweke sawa tujiandae kiakili.Na kiumeme"Jenereta tujaze mafuta.
 
Kuna tetesi zimezagaa kwenye social networks Mbatia ataongea na taifa ifikapo saa nne usiku kupitia ITV mwenye taarifa sahihi atuweke sawa tujiandae kiakili.
ITV wmatangaza anataka kuzungumzia mwenendo wa kampeni
 
Mbatia gusia kidogo kuhusu NEC, kwa nini kuna utezi wakati huu? hapa goal la mkono limeanza kuandaliwa live live.
 
Kuna tetesi zimezagaa kwenye social networks Mbatia ataongea na taifa ifikapo saa nne usiku kupitia ITV mwenye taarifa sahihi atuweke sawa tujiandae kiakili.Na kiumeme"Jenereta tujaze mafuta.

Suala la majenereta si walisema watatumia siku saba kuingiza gesi kwenye mitambo sasa vipi tena wakate umeme aaaaagh!
 
kuna tetesi zimezagaa kwenye social networks mbatia ataongea na taifa ifikapo saa nne usiku kupitia itv mwenye taarifa sahihi atuweke sawa tujiandae kiakili.na kiumeme"jenereta tujaze mafuta.
anataka kujitoa ukawa
 
Wakuu wote wa Jamiiforums napenda kuwajulisha kuwa Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA anategemewa kuhutubia taifa leo saa 4 usiku kupitia ITV.Mh.Mbatia anakwenda kuueleza umma mwenendo wa kampeni za UKAWA.Itarushwa Live...Msanue na Mwenzio atulie kumsikia na kumuona Mbatia
 
Cku nzma nihustle na kla mahali in siasa, akahutubie ukawa sio nchi nzma..
Hub mda wa UeFa champions league...
 
Tena nilikuwa nataka nikalale sasa nimegeuzia mlangoni angekua magufuli nisingewasha Tv tena.ila jwa Ukawa hahaaaaa sikosi
 
Hizo ni za ukweli zimeshabitishwa na Tumaini Makene Mbatia atakuwa live kupia ITV,Azamu 2 tv na vyombo vingine vya habari kuanzia saa nne leo .lengo la mkutano huu
Tunataka kuendelea kuwasaidia watanzania waendelee.kutembea kwenye mstari sahihi,kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu ili wafanye maamuzi sahihi hapo oktoba 25,2015.
Pia kutoa shukrani kwa watanzania ambayo wamekubali na wanaimba mabadiliko nje ya CCM kupitia Mgombea uraisi wa CHADEMA anayeungwa mkono na vyama washirika vinavyounda UKAWA,na wagombea ubunge na udiwani wanaotokana na vyama vinavyounda UKAWA yaani NCCR -MAGEUZI,CUF,CHADEMA NA NLD.
Mkutano huu utaoneshwa live.
 
Back
Top Bottom