James Mbatia: UKAWA ipo imara, haitasambaratika, akerwa na kauli za Magufuli, CCM

Utaombaje mdahalo na viongozi wa vyama badala ya wagombea urais, sijapata kuona. Kwani atayeenda ikulu ni nani. ???
 
UPDATES:

- Mbatia analalamikia vitisho vya Mgombea wa CCM, Magufuli kuwa wakiwachagua wapinzani nchi itaingia kwenye machafuko

- Mbatia: Watu wameanza kupoteza maisha, wana UKAWA wanadhalilishwa na wengine kutekwa

- Mbatia: Hali imeanza kuwa tete, vitisho vya kila aina vimeanza. Tumedhalilishwa sana, tumeitwa matusi ya kila aina.

- Mbatia: Lowassa si mdini, alikuwa anataka watanzania wamwombee. Mhe. Lowassa hajaenda kwenye nguvu za giza. Hajatumia viungo vya albino, ameenda kuomba viongozi wa dini wamwombee; udini wake unatoka wapi?

- Mbatia: Tunawashukuru Lowassa na Sumaye kwa nia zao njema kuja Upinzani kuongeza nguvu ili tuyafanye mabadiliko ya kweli

- Mbatia: Hata CCM wangemweka malaika, si rahisi kupata mabadiliko bila kufanya mabadiliko ya mfumo.

- Mbatia: CCM wanasema usichague chama, chagua mtu. Watanzania wanatakiwa kujua kuwa Magufuli ni CCM, na hawezi kujitenganisha na CCM. Huwezi kulisukuma gari ukiwa ndani yake, lazima utoke ndipo ulisukume. Mabadiliko ndani ya CCM hayawezekani

- Mbatia: Tumefanya utafiti, tuna uhakika wa ushindi mwaka huu

- Mbatia: Hatutawapa CCM nafasi ya kufanya machafuko ndani ya Taifa hili

- Mbatia: CCM hawana hati miliki ya kuitawala Tanzania hii. Watupishe tufanye mabadiliko haya kwa utulivu na amani.

- Mbatia: Sumaye, Lowassa wana uzoefu mkubwa wa kuongoza Serikali, uwezo tunao! Tunao kina Mungai, Msindai, Mgeja n,k na wanao uzoefu wa kuongoza Serikali.

- Mbatia: Limeibuka suala la ukabila. Ni aibu iliyoje? CCM wanahubiri ukabila, ukanda bila aibu yoyote!

- Mbatia: Ilani ya Uchaguzi ni mkataba kati ya mpiga kura na mpigiwa kura; tuwaulize CCM Ilani yao iliyopita imetekelezwa kwa kiasi gani kabla hawajaja na ilani mpya. UKAWA tunayo ilani ya pamoja

- Mbatia: Tunawataka CCM waje tufanye midahalo kwa hoja

- Mbatia: Wenyeviti wa vyama wawekwe kwenye midahalo ili UKAWA tupambane na CCM kwa hoja na watanzania wajue pumba na mchele

- Mbatia: UKAWA ipo imara, haitasambaratika!

- Mbatia anafafanua wapi watapata fedha za kufanikisha yale wanayoahidi kwenye kampeni.

Mdahalo tumekubali ila uwe kati ya Lowasa na Magufuli wengine hatuwataki.
 
huyu mbatia ni hatar, kwanza anaongea kwa kujiamini na anauwezo mkubwa wa kuongea na kupangilia mambo, binafsi nimemkubali
 
Kwanini baadhi ya watu wanapenda kutukana humu JF?Ustaarabu hununuliwi kama unaona alichopost mwenzako huna cha kujibu ni vzr zaidi kutopost
 
Swali toka nipashe... umesema kuna vikao kuhusisha wakuu wa mikoa...weka wazi lengo la vikao
 
mbatia anaongea utumbo tu, watanzania wanaitaji midaharo ya wagombea urais yeye anataka midaharo ya vyama vya siasa, kweli mbatia ni mzigo
Wa fedha na mawazo yaliyotukukaaa!
 
Hii tabia ya kuongea uwongo inabidi idhibitiwe. Ukawa mtaiingiza nchi kwenye machafuko kwa kueneza habari za uzushi.
 
Back
Top Bottom