Mgambilwa ni mntu
JF-Expert Member
- May 30, 2017
- 2,869
- 3,188
Wiki hii wakati wa Mjadala wa Bajeti ya Maliasili na Utalii, Mbunge wa Vunjo, mkoani Kilimanjaro, James Mbatia, ambaye ni Waziri Kivuli wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, alimtuhumu Rais John Pombe Magufuli kwa tamko lake kuwa, "Watu wa Kaskazini wasubiri kwanza."
Katika kujenga arguments zake, Mbatia alijaribu kuonyesha jinsi kodi zilivyo nyingi katika sekta ya utalii (57) na kwamba fedha za utalii zinazorudi kwa wananchi wanaoishi maeneo ya kitalii ni ndogo na siyo 7% iliyopo kisheria. Mbatia alisifia juu ya mapato makubwa ya utalii kwenye TANAPA yatokanayo na Hifadhi tano zilizoko Kaskazini - Kilimanjaro, Manyara, Tarangire, Ngorongoro na Serengeti.
Hakutaja maeneo mengine ya kiutalii ndani ya Nchi bali alitetea na kusifia ubora wa Ukanda wa Kaskazini kiutalii. Bahati mbaya hakumpa Rais Magufuli, the benefit of doubt, ukizingatia kuwa, Rais aliyasema hayo akiwa katika Ukanda wa pili kwa Utalii nchini - Iringa.
Kwa kuwa, CHADEMA ndio wamekuwa mstari wa mbele kumuita Rais Magufuli kuwa anapendelea watu wa Kanda ya Ziwa, nimelazimika kufuatilia Wizara Kivuli 18 za Kambi ya Upinzani Bungeni kuona jinsi Wabunge kutoka Kanda zote nchini wamezigawana. Majibu yalikuwa ifuatavyo:

- Kanda ya Kaskazini - 15, ambapo Wenyeviti wa Kamati wana Wizara - 08.
- Kanda ya Ziwa - 07, ambapo Wenyeviti wa Kamati ni - 03.
- Nyanda za Juu Kusini - 05, Wenyeviti wa Kamati ni - 02.
- Kanda ya Mashariki - 04, Wenyeviti wa Kamati - 00.
- Kanda ya Zanzibar - 02, Wenyeviti wa Kamati - 02
- Kanda ya Kati - 01, Wenyeviti wa Kamati - 01.
- Kanda ya Kusini - 01, Wenyeviti wa Kamati - 00.
- Kanda ya Magharibi - 01. Mwenyekiti wa Kamati - 01.