James Hadley Chase, Mfu anayeishi

James Hadley Chase, Mfu anayeishi

Nimesoma kimoja tu Cha huyu jamaa
Like a hole in the head
Aisee jamaa alikua anajua Sasa Leo ndio mmenipa hints Ngoja nitafute vingine vyote dadeq imenipa mzuka hii thanks JF members mmenibust Sasa ebooo!
 
Miaka hii ngumu sana kusoma vitabu vta novel hasa upelelezi fashion yake imepita vijana wapo busy na mambo mengine.
Mimi nilisomaga vitabu 15 miaka 25 iliopita. Chamwisho ni wizi wa kwenda kuiba vito vya thamani benki sikumbiki title hata moja kwa sasa.
 
Kuna novel moja theme yake ilikuwa sauzi africa huko ndani ndani
The Vulture is a patient bird ilizungumzia Afrika kusini nawakumbuka Ndege Tai wakimvizia jamaa ajifie wamshambulie
 
Hii ndio babu kubwa mzeee
1.The Vulture is a patient bird

2. One bright summer morning

3. Shock treatment

4. So what happens to me

5. Thats the way the cookie crumbles

6. Knock knock who is there?

Hzi ndio my best
unakikumbuka The Sucker Punch
 
JAMES HADLEY CHASE

AMEKUFA LAKINI ANGALI ANAISHI


NA
NIHZRATH NTANI JNR

Jumatatu ya Mei 6, 1985. Habari kubwa Duniani ilikuwa taarifa ya kifo cha aliyepata kuwa mwandishi nguli Barani Ulaya; aliyejulikana zaidi kwa jina la James Hadley Chase. Kifo cha James Hadley Chase kilileta simanzi kubwa miongoni mwa wasomaji wengi wa vitabu Duniani hasa novel.

Imepita miaka 34 hivi leo. Tangu mwili wake ulale katika ardhi ya mji wa Corseaux-Sur-Vevery nchini Switzerland. Mwanaume huyu ameacha alama kubwa Duniani hata baada ya kifo chake ni kama angali anaishi ndani yetu kupitia mawazo yetu..

JE UNAMFAHAMU RENE LODGE BRABAZON RAYMOND?

Ni jina geni miongoni mwa wasomaji wengi wa riwaya Duniani mara tu unapotajiwa jina hili. Pia, alipata kuitwa kwa majina kadhaa yakiwemo majina ya James. L Docherty, Raymond Marshall, Ambrose Grant, n.k, lakini hakuna unachoweza kukihusisha dhidi yake. Rene L.B Raymond alizaliwa mnamo December 24,1906 uko London nchini England.

Ameishi Duniani kwa miaka 79 tu. Ni miaka 79 yenye kusisimua na miaka hiyo ya kuishi kwake ilileta athari chanya kwa mamilioni ya watu Duniani kote bila kujali imani na utofauti wa rangi kupitia kalamu yake.

Kuna wakati ulijihisi kuwa katika ulimwengu wa peke yako wakati mikononi mwako ukiwa umeshika moja ya kazi ya Rene Raymond.

Ardhi haina huruma. Ardhi imewameza wapendwa na mashujaa wetu na siku moja itakumeza wewe na mimi pia. Hakuna namna!. Rene Raymond ni mmoja wa watu hao.

Historia ya maisha ya utoto wa Rene Raymond imejaa dhihaka , dhihaka nyingi. Akiwa na miaka 18 tu aliondoka nyumbani kwao.

Akiwa mzaliwa kwa familia ya Baba mwanajeshi mwenye asili ya India. Rene Raymond hakupenda kuwa mwanasayansi kama baba yake alivyoazimia. Ilimlazimu kuondoka nyumbani kwao.

Hakuwahi kuwa na ndoto ya kuwa mwandishi maishani. Alipenda sana kuwa mwanamuziki siku moja. Alipenda mno kujifunza muziki aina ya classic na Opera. Ndoto yake haikuwa kweli na haikutimia. Hii hutokea kwa wanadamu wengi Duniani. Kwenda tofauti na ndoto zao.


NDOTO ILIPOFUTIKA NA KUWA MTU MWINGINE
Kuna wakati unachokitamani huwezi kukipata. Unakuja kupata sicho ulichokitamani. Lakini hiki ulichokipata ndicho kinakufanya utambulike kuwa ni mtu wa kipekee.

Rene Raymond alipoondoka nyumbani akaanza kutafuta kazi, akajikuta akihudumu kazi ya kuuza duka kubwa la vitabu. Ni mahala hapo alijifunza pia kupiga picha na kuwapiga watu mbalimbali kwa malipo.

Kati ya miaka ya 1928-1939. Kuliibuka matatizo ya kiuchumi (Great Depression) huko Amerika na Duniani kwa ujumla. Hali hii ilipelekea kuibuka kwa makundi mengi ya kiharamia.

Ni wakati huo akili ya Rene Raymond ikagundua kuna fursa ya kuwa mwandishi wa riwaya. Mamilioni ya watu walikuwa gizani katika habari zinazohusu ujambazi.

Pamoja ya kuwa muuzaji wa vitabu. Akiwa anakaa na vitabu kwa masaa mengi ya siku. Rene Raymond hakuwa mpenzi wa kusoma vitabu. Ni katika hali hiyo ya matatizo ya kiuchumi.

Akajikuta akivutiwa kusoma kitabu cha "The Postman Always Rongs Twice" kilichoandikwa na James M Cain. Kitabu hichi kilichapwa mnamo mwaka 1934.

Rene Raymond hakuishia kusoma kitabu hicho tu. Akapata kusoma simulizi za kundi la kijambazi liliokuwa chini ya mwanamama Ma Barker na watoto wake. Baada ya kumaliza kusoma simulizi hizo. Akajikuta anaandika kitabu chake cha kwanza kilichoitwa "No Orchids For Miss Blandish" safari ya Rene L.B Raymond kuwa mwandishi mahiri ikaanzia hapo.


Katika vita ya pili ya Dunia. Rene Raymond akajikuta akijiunga na Jeshi la Anga la Uingereza. Akiwa ndani ya jeshi aliweza kuandika riwaya kadhaa ikiwemo "A Royal Air Force Anthlology". Mtu huyu Rene Raymond ndiye baadae alikuja kujiita James Hadley Chase.


KWANINI ALIAMUA KUJIITA JAMES HADLEY CHASE?
Wakati alipokuwa akifanya kazi ya kuuza vitabu katika duka la vitabu. Alikuwa angali mvulana mdogo mno. Kutokana na udogo wake alijikuta akipendwa mno na baadhi ya wateja. Mmoja wa wateja hao alikuwapo raia wa Ireland aliyekuwa mfanyakazi wa Bank katika moja ya bank nchini England.

Mteja huyu alijenga urafiki wa karibu mno na Rene Raymond. Kuna wakati kila toleo jipya linapowasili dukani hapo basi Rene Raymond angelimpa taarifa mteja huyo. Mteja huo aliitwa James Hadley Chase.

Rene Raymond na James Hadley Chase wakajikuta wakiwa marafiki wakubwa na kuna wakati James Hadley Chase alipata kumpa mwaliko Rene Raymond kumtembelea nyumbani kwake na Rene akafanya hivyo. Urafiki ukashamiri!

Baada ya kwenda vitani. Mawasiliano kati ya Rene Raymond na James Hadley Chase yalikatika kwa muda mrefu. Vita ilipoishia Rene Raymomd aliamua kwenda kumtembelea James Hadley Chase nyumbani kwake. Huzuni ikatokea!

Badala ya kukutana na James Hadley Chase. Akajikuta anapata simulizi za umauti wa James Hadley Chase na mwishowe kulitazama kaburi lililoficha mwili wa James Hadley Chase akiwa tayari mfu.Huzuni ikatamalaki ndani ya hisia za Rene Raymond.

Kitendo cha kuondokewa na rafiki yake kipenzi, kilimuumiza sana Rene. Ndipo, alipoazimia kumuenzi James Hadley Chase kivitendo.

Akaamuru vitabu vyake vyote vile alivyokwisha kuvichapa na anavyotarajia kuvichapa vitumie jina la JAMES HADLEY CHASE kwa heshima ya hayati James Hadley Chase. Urafiki wenye kumbukizi.


KWANINI TUNAMKUMBUKA JAMES HADLEY CHASE (Rene L. B Raymond)?

Katika maisha yake ya miaka 79 hapa Duniani. Anatajwa kuwa mwandishi bora wa muda wote wa riwaya. Mtu huyu Anatajwa ndio chimbuko la waandishi wengi mahiri wa riwaya Duniani.

Amepata kuandika vitabu 90 huku vitabu vyake 50 vilipata kuchezwa katika filamu. Moja ya kazi zake maarufu ni "What's better than Money", "Well now my Pretty", " The World in My Pocket", I would Rather stay Poor", " My Lough comes Last" na nyinginezo nyingi.

Miongoni mwetu kupitia kazi ya James Hadley chase ilipelekea kuwa na umahiri wa kiwango fulani wa lugha ya kiingereza mbali na kuburudika. Akiwa ameshaondoka Duniani bado kazi zake zimebakia kuwa na thamani kubwa kwa wasomaji wa vitabu.

Huyu ndiye anayetajwa kuwa baba na mfalme wa Riwaya (Novel) Duniani. Bado maandishi yake yanaendelea kuishi vizazi hadi vizazi. Jiulize wewe ukifa leo jamii yako itakukumbuka kwa lipi? Ama utaondoka na jina lako moja kwa moja?

# You're lonel, when you're Dead"

Ref: "The Man with the money generates a feeling of power. He thinks he can do everything. And I don't like the Almighty do not like people who hav a lot of money, because they are starting to put pressure on others"
Namkumbuka sana James Hadley Chase. Miaka ya sabini nikiwa Sekondari nilisoma vitabu vyake na nilifikisha zaidi ya hamsini. Hicho cha "No Orchids for Miss Blandish" kikijulikana kama "the Grimson Gang". Nimepitia pia vile vya mpelelezi Mark Girland na vingine vingi tu. Na niseme ukweli tu hata hiki Kiingereza ambacho najidai nacho leo nimekiibua toka miongoni mwa vitabu vyake. Wakati wetu tulikuwa na uraibu wa kusoma novel kwa wingi kama ilivyo kwa vijana wa kileo na uraibu wa mambo ya mitandaoni.
 
safi saana mwandish.uviv wa kutafuta habari sikujuaga kama hadley chase sio jina lake ingawaje nimesoma stori zake.urithi wa marehem.mzee tena first edition.sijui mzee vile alikua anasafir nje miaka hio so many books za jmes hadley.
mpaka kufikia form 5 nilikua nimesoma almost ving sana
well now my pretty,no orchids for miss blandish, the sucker punch,
nikikaa navirudiaga tena
Pitia pia "Want to stay alive?" na uione formula for fear aliyoitengeneza yule Seminole Indian akijulikana kwa jina la Poke Tohoro. Hakika kinafurahisha sana.
 
Mkubwa p/se naomba unitumie pia hizo soft copy za James hardly chase
 
Namkumbuka sana James Hadley Chase. Miaka ya sabini nikiwa Sekondari nilisoma vitabu vyake na nilifikisha zaidi ya hamsini. Hicho cha "No Orchids for Miss Blandish" kikijulikana kama "the Grimson Gang". Nimepitia pia vile vya mpelelezi Mark Girland na vingine vingi tu. Na niseme ukweli tu hata hiki Kiingereza ambacho najidai nacho leo nimekiibua toka miongoni mwa vitabu vyake. Wakati wetu tulikuwa na uraibu wa kusoma novel kwa wingi kama ilivyo kwa vijana wa kileo na uraibu wa mambo ya mitandaoni.

Mkuu unapomtaja Mark Girland umkumbuke pia na Malik wa the then USSR. Alipoonekana mmoja wapo basi na mwingine hayuko mbali. Walikua ni ma agent wa mataifa mawili mahasimu wakubwa lakini wakati fulani wakiokoana kwenye scenario za kifo

Walikua katika “Have This One On Me, This Is For Real” na kingine nimekisahau kidogo. Kila mmoja aki admire skills za mwenzake japo wakiwindana wauwane
 
Pitia pia "Want to stay alive?" na uione formula for fear aliyoitengeneza yule Seminole Indian akijulikana kwa jina la Poke Tohoro. Hakika kinafurahisha sana.

Umenikumbusha mbali sana chief

Pia kuna ma detectives kama watatu hivi walikua mashuri kidogo. Kuna Patrol Man O’haloran na Detective Second Grade Thom Lepsiky na mwenzao mwingine
 
Back
Top Bottom