James Hadley Chase, Mfu anayeishi

James Hadley Chase, Mfu anayeishi

Coffin from Hong kong
Eve
No orchids for miss blandish
Like a hole in the head
I'll get you for this
The double shuffle
Just a matter of time
I will bury my dead
Tiger by the tail
You never know with women
12 Chinamen and a woman
There's always a price tag
My laugh comes last
Strictly for cash
You must be kidding.
 
Nimebakiza novels chache za huyu jamaa ambazo sijazisoma lakini naendelea kwa sababu ninazo zote kwenye soft copy, Salute kwake. Ni miongoni mwa waandishi bora wa novels.
"One bright summer morning "
"The vulture is a patient bird"
 
Nimesoma sana hivi vitabu nilivyokuwa Sekondari O Level.
Mimi nilichelewa kidogo, nilianza kuzisoma nikiwa University, mwaka wa 4 baada ya shule kuwa imepungua kidogo makali na digrii kuwa inaanza kunukia. Nina soft kopy za ufupisho wa novel zote za Chase (nadhani kwa kiingereza wanaita excerpts), nikipata muda nitaziweka humu kwenye uzi huu
 
Coffin from Hong kong
Eve
No orchids for miss blandish
Like a hole in the head
I'll get you for this
The double shuffle
Just a matter of time
I will bury my dead
Tiger by the tail
You never know with women
12 Chinamen and a woman
There's always a price tag
My laugh comes last
Strictly for cash
You must be kidding.
uchung sana baadh mchwa wameniharibia.ila almost vyote vipo hard copy first edition mzee enzi hizo karud navyo nje.1990
 
Kaka ilo jina lako limenikumbusha kuna kamalzaman,kitabu cha Alif leila ulela,na safari saba za Sindbad baharia.
sio alif.alfu layl wa layl.usiku elfu moja na moja.visa vyakale uajem kuhusu sultan aliyekua anaua wake zake kila usiku akioa asubh anaua.akatokea huyu mmoja aliyekua anatoa hadith for one thousand nights ikawa kila ikifika asubh anamwambia mumewe sultan,bwana wangu ikiwa utasikia kisa cha flan na flan nimkizur kushinda hki bas mfalme anamwachia hamuuw ikaenda sana hii.ndio zikapokelewa na kuwekwa katika lugha za mataifa mbalimbal.kwa mara ya kwanza kutiwa kiswahil yapata 1930
 
JAMES HADLEY CHASE

AMEKUFA LAKINI ANGALI ANAISHI

NA
NIHZRATH NTANI JNR

Jumatatu ya Mei 6, 1985. Habari kubwa Duniani ilikuwa taarifa ya kifo cha aliyepata kuwa mwandishi nguli Barani Ulaya; aliyejulikana zaidi kwa jina la James Hadley Chase. Kifo cha James Hadley Chase kilileta simanzi kubwa miongoni mwa wasomaji wengi wa vitabu Duniani hasa novel.

Imepita miaka 34 hivi leo. Tangu mwili wake ulale katika ardhi ya mji wa Corseaux-Sur-Vevery nchini Switzerland. Mwanaume huyu ameacha alama kubwa Duniani hata baada ya kifo chake ni kama angali anaishi ndani yetu kupitia mawazo yetu..

JE UNAMFAHAMU RENE LODGE BRABAZON RAYMOND?

Ni jina geni miongoni mwa wasomaji wengi wa riwaya Duniani mara tu unapotajiwa jina hili. Pia, alipata kuitwa kwa majina kadhaa yakiwemo majina ya James. L Docherty, Raymond Marshall, Ambrose Grant, n.k, lakini hakuna unachoweza kukihusisha dhidi yake. Rene L.B Raymond alizaliwa mnamo December 24,1906 uko London nchini England.

Ameishi Duniani kwa miaka 79 tu. Ni miaka 79 yenye kusisimua na miaka hiyo ya kuishi kwake ilileta athari chanya kwa mamilioni ya watu Duniani kote bila kujali imani na utofauti wa rangi kupitia kalamu yake.

Kuna wakati ulijihisi kuwa katika ulimwengu wa peke yako wakati mikononi mwako ukiwa umeshika moja ya kazi ya Rene Raymond.

Ardhi haina huruma. Ardhi imewameza wapendwa na mashujaa wetu na siku moja itakumeza wewe na mimi pia. Hakuna namna!. Rene Raymond ni mmoja wa watu hao.

Historia ya maisha ya utoto wa Rene Raymond imejaa dhihaka , dhihaka nyingi. Akiwa na miaka 18 tu aliondoka nyumbani kwao.

Akiwa mzaliwa kwa familia ya Baba mwanajeshi mwenye asili ya India. Rene Raymond hakupenda kuwa mwanasayansi kama baba yake alivyoazimia. Ilimlazimu kuondoka nyumbani kwao.

Hakuwahi kuwa na ndoto ya kuwa mwandishi maishani. Alipenda sana kuwa mwanamuziki siku moja. Alipenda mno kujifunza muziki aina ya classic na Opera. Ndoto yake haikuwa kweli na haikutimia. Hii hutokea kwa wanadamu wengi Duniani. Kwenda tofauti na ndoto zao.

NDOTO ILIPOFUTIKA NA KUWA MTU MWINGINE
Kuna wakati unachokitamani huwezi kukipata. Unakuja kupata sicho ulichokitamani. Lakini hiki ulichokipata ndicho kinakufanya utambulike kuwa ni mtu wa kipekee.

Rene Raymond alipoondoka nyumbani akaanza kutafuta kazi, akajikuta akihudumu kazi ya kuuza duka kubwa la vitabu. Ni mahala hapo alijifunza pia kupiga picha na kuwapiga watu mbalimbali kwa malipo.

Kati ya miaka ya 1928-1939. Kuliibuka matatizo ya kiuchumi (Great Depression) huko Amerika na Duniani kwa ujumla. Hali hii ilipelekea kuibuka kwa makundi mengi ya kiharamia.

Ni wakati huo akili ya Rene Raymond ikagundua kuna fursa ya kuwa mwandishi wa riwaya. Mamilioni ya watu walikuwa gizani katika habari zinazohusu ujambazi.

Pamoja ya kuwa muuzaji wa vitabu. Akiwa anakaa na vitabu kwa masaa mengi ya siku. Rene Raymond hakuwa mpenzi wa kusoma vitabu. Ni katika hali hiyo ya matatizo ya kiuchumi.

Akajikuta akivutiwa kusoma kitabu cha "The Postman Always Rongs Twice" kilichoandikwa na James M Cain. Kitabu hichi kilichapwa mnamo mwaka 1934.

Rene Raymond hakuishia kusoma kitabu hicho tu. Akapata kusoma simulizi za kundi la kijambazi liliokuwa chini ya mwanamama Ma Barker na watoto wake. Baada ya kumaliza kusoma simulizi hizo. Akajikuta anaandika kitabu chake cha kwanza kilichoitwa "No Orchids For Miss Blandish" safari ya Rene L.B Raymond kuwa mwandishi mahiri ikaanzia hapo.

Katika vita ya pili ya Dunia. Rene Raymond akajikuta akijiunga na Jeshi la Anga la Uingereza. Akiwa ndani ya jeshi aliweza kuandika riwaya kadhaa ikiwemo "A Royal Air Force Anthlology". Mtu huyu Rene Raymond ndiye baadae alikuja kujiita James Hadley Chase.

KWANINI ALIAMUA KUJIITA JAMES HADLEY CHASE?
Wakati alipokuwa akifanya kazi ya kuuza vitabu katika duka la vitabu. Alikuwa angali mvulana mdogo mno. Kutokana na udogo wake alijikuta akipendwa mno na baadhi ya wateja. Mmoja wa wateja hao alikuwapo raia wa Ireland aliyekuwa mfanyakazi wa Bank katika moja ya bank nchini England.

Mteja huyu alijenga urafiki wa karibu mno na Rene Raymond. Kuna wakati kila toleo jipya linapowasili dukani hapo basi Rene Raymond angelimpa taarifa mteja huyo. Mteja huo aliitwa James Hadley Chase.

Rene Raymond na James Hadley Chase wakajikuta wakiwa marafiki wakubwa na kuna wakati James Hadley Chase alipata kumpa mwaliko Rene Raymond kumtembelea nyumbani kwake na Rene akafanya hivyo. Urafiki ukashamiri!

Baada ya kwenda vitani. Mawasiliano kati ya Rene Raymond na James Hadley Chase yalikatika kwa muda mrefu. Vita ilipoishia Rene Raymomd aliamua kwenda kumtembelea James Hadley Chase nyumbani kwake. Huzuni ikatokea!

Badala ya kukutana na James Hadley Chase. Akajikuta anapata simulizi za umauti wa James Hadley Chase na mwishowe kulitazama kaburi lililoficha mwili wa James Hadley Chase akiwa tayari mfu.Huzuni ikatamalaki ndani ya hisia za Rene Raymond.

Kitendo cha kuondokewa na rafiki yake kipenzi, kilimuumiza sana Rene. Ndipo, alipoazimia kumuenzi James Hadley Chase kivitendo.

Akaamuru vitabu vyake vyote vile alivyokwisha kuvichapa na anavyotarajia kuvichapa vitumie jina la JAMES HADLEY CHASE kwa heshima ya hayati James Hadley Chase. Urafiki wenye kumbukizi.

KWANINI TUNAMKUMBUKA JAMES HADLEY CHASE (Rene L. B Raymond)?

Katika maisha yake ya miaka 79 hapa Duniani. Anatajwa kuwa mwandishi bora wa muda wote wa riwaya. Mtu huyu Anatajwa ndio chimbuko la waandishi wengi mahiri wa riwaya Duniani.

Amepata kuandika vitabu 90 huku vitabu vyake 50 vilipata kuchezwa katika filamu. Moja ya kazi zake maarufu ni "What's better than Money", "Well now my Pretty", " The World in My Pocket", I would Rather stay Poor", " My Lough comes Last" na nyinginezo nyingi.

Miongoni mwetu kupitia kazi ya James Hadley chase ilipelekea kuwa na umahiri wa kiwango fulani wa lugha ya kiingereza mbali na kuburudika. Akiwa ameshaondoka Duniani bado kazi zake zimebakia kuwa na thamani kubwa kwa wasomaji wa vitabu.

Huyu ndiye anayetajwa kuwa baba na mfalme wa Riwaya (Novel) Duniani. Bado maandishi yake yanaendelea kuishi vizazi hadi vizazi. Jiulize wewe ukifa leo jamii yako itakukumbuka kwa lipi? Ama utaondoka na jina lako moja kwa moja?

# You're lonel, when you're Dead"

Ref: "The Man with the money generates a feeling of power. He thinks he can do everything. And I don't like the Almighty do not like people who hav a lot of money, because they are starting to put pressure on others"
Ungefanyia kazi kiingereza chako..maana vitabu vyake vingi umevikosea title mpaka nikaanza kuwaza kuwa hivyo ni vya wapi. Historia nzuri. Next time kwenye kiingereza mpe mtu ahakiki.
 
Nimesoma hicho "you are lonely when you're dead "
 
sio alif.alfu layl wa layl.usiku elfu moja na moja.visa vyakale uajem kuhusu sultan aliyekua anaua wake zake kila usiku akioa asubh anaua.akatokea huyu mmoja aliyekua anatoa hadith for one thousand nights ikawa kila ikifika asubh anamwambia mumewe sultan,bwana wangu ikiwa utasikia kisa cha flan na flan nimkizur kushinda hki bas mfalme anamwachia hamuuw ikaenda sana hii.ndio zikapokelewa na kuwekwa katika lugha za mataifa mbalimbal.kwa mara ya kwanza kutiwa kiswahil yapata 1930
Duh,kweli we unakumbukumbu.unacho hiki kitabu.
 
Ungefanyia kazi kiingereza chako..maana vitabu vyake vingi umevikosea title mpaka nikaanza kuwaza kuwa hivyo ni vya wapi. Historia nzuri. Next time kwenye kiingereza mpe mtu ahakiki.
Jamii forums kuna grammar tena? Mbona tumemuelewa km ametumia Google translator kwa copy & paste tunashukuru pia
 
Back
Top Bottom