lutemi
JF-Expert Member
- Dec 24, 2013
- 1,743
- 1,379
Mimi nakumbuka mwaka 2001 nilikuwa mkoani Morogoro kwa biashara ya madini , eneo linaitwa mkuyuni. Nikaugua na kuenda zahanati Fulani hivi .
Na kwasababu ya kutokuwa na vitanda vingi ,tulilazwa kitanda kimoja watu wawili na sote tulitundikiwa drip. Kilichotokea SAA nane usiku nipo macho na tumebakia wawili tu kitanda kimoja huyu mwezangu akafariki huku ninamwona.
Manesi wakaja kumfunika na kuniambia mwezio maeshafariki maiti tutatoa asubuhi na kunitakia usiku mwema. Duh niliondoka usiku huohuo. Sitasahau hii kitu.
Wewe unakumbuka tukio gani maishani mwako?