Jambo gani ambalo huwezi kulisahau?

lutemi

JF-Expert Member
Dec 24, 2013
1,743
1,379
Mimi nakumbuka mwaka 2001 nilikuwa mkoani Morogoro kwa biashara ya madini , eneo linaitwa mkuyuni. Nikaugua na kuenda zahanati Fulani hivi .

Na kwasababu ya kutokuwa na vitanda vingi ,tulilazwa kitanda kimoja watu wawili na sote tulitundikiwa drip. Kilichotokea SAA nane usiku nipo macho na tumebakia wawili tu kitanda kimoja huyu mwezangu akafariki huku ninamwona.

Manesi wakaja kumfunika na kuniambia mwezio maeshafariki maiti tutatoa asubuhi na kunitakia usiku mwema. Duh niliondoka usiku huohuo. Sitasahau hii kitu.


Wewe unakumbuka tukio gani maishani mwako?
 
Dah😭 ni kikumbuka mwaka 2014 wakati matokeo ya kidato cha Nne yalipo toka kuna rafiki yangu kabisa, yeye alifauru mimi ni kafeli 😬, basi jamaa akaanza kunicheka kuwa kanizidi hakili mimi sina hakili, Mtaa kwenyewe watu wananicheka kuwa Nimefeli.
Kiukweli maisha yalikuwa magumu sana kipindi hicho cha kuomboleza, mbaya zaidi wale waliofaulu walienda shule na kurudi nyumbani huku mimi nikiwa bado nipo Mtaani sijui niende wapi, niliwaza sana nifanyeje ili hii aibu niifute miongoni mwa watu!
Ndipo mwaka 2017 nilipo amua kwenda Zanzibar huko ndio niliweza kuifuta aibu niliyo kuwa nayo dhidi ya rafiki yangu,

Iko hivi huyu rafiki yangu aliye nicheka yupo yupo tu baada ya kukosa ajira kutoka JK amekuwa kama kachanganyikiwa hivi.
Sasa hivi rafiki yangu anaona aibu sana juu yangu aliona kusoma ndoo kama liza kila kitu kumbe Safari ndio kwanza inaanza,
Aliye ni cheka saivi Nipo Dunia ya kwanza 🤪(Ulaya) yeye bado analamba vumbiiiiii.
 
Back
Top Bottom