Jamani waungwana wa jf kwanini inakuwa hivi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani waungwana wa jf kwanini inakuwa hivi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by WomanOfSubstance, Mar 18, 2011.

 1. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #1
  Mar 18, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Kabla sijasema ninachokikusudia, naomba niwatakeni radhi kwa vile inaweza kuwagusa baadhi ya wana JF moja kwa moja.Siyo kusudio langu kumuudhi mtu lakini kiungwana unapoona jambo na likakusumbua basi ni vema ukaliweka wazi.

  Baada ya kuwatakeni radhi naomba niseme: Kwanini mara kwa mara tunaona wana jamvi wakiteka nyara thread na kuanza kuchomekea hoja ambazo hazina uhusiano? Mfano watu wanazungumzia jambo zito jukwaa la siasa au jamii intelligence, unashtukia hoja imeshapotoshwa na kuanza kuonekana ina ladha au harufu ya udini au mapenzi!
  • Kwanini wahusika wasiache tu kuchangia badala ya kupotosha mtiririko wa mada?
  • Kwanini wahusika wasihamie jukwaa la dini kulumbana kuhusu dini zao?
  • Kwanini wahusika hawahamii MMU pale wanapojisikia wanataka kuambizana mambo matamu matamu?
  • Au basi kwanini tusiwashukuru Mods kwa kuanzisha jukwa la chit chat na tukalitumia vilivyo pale tunapokutana na wapendwa wetu ndani ya majukwaa mengine tukaambizana tutoke chemba tukutana CHIT CHAT ili tuendeleze gumzo la nini kilijiri baaya ya kuachana jana yake kwenye viti virefu au kwenye nyama-choma?
  Binafsi sina tatizo na mtu yeyote ila ninatatizika kidogo kuona tunapoteza ladha ya majadiliano kwa kutokutumia majukwaa husika vizuri.

  Asanteni kwa kunisoma na samahani kwa nitakayemkwaza kwa namna yoyote ile.Ukiona nimekukera basi badala ya kunizodoa hapa, tukutane kwenye jukwaa la chit chat tupige gumzo vizuri.

  WAKATABAHU!
  WoS
   
 2. L

  Leornado JF-Expert Member

  #2
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ndio watu walivyo, manake katika msafara wa mamba kenge nao wao.


  Hamna button ambayo mwenye thread anaweza kudelete michango ambayo iapotosha mada husika?

  Mfano michango kama vipi mpenzi, nimekumiss si mahala pake kama si jukwaa la mapenzi.
   
 3. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #3
  Mar 18, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Hili kila mtu anayeanzisha mada linamkera, mimi nadhani kungekuwa na button ambayo inaweza kumuwezesha mtoa mada kufuta michango yote yenye lengo la kuvuruga mada, tutaripoti michango mingapi maana topiki zingine zinavamiwa hadi lengo lote linapotea na yanajadiliwa mambo yasiyohusika mpaka thread inapotea hamna la maana lililochangiwa.
   
 4. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #4
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,572
  Likes Received: 5,759
  Trophy Points: 280

  ukitaka jibu lako uwe na amani zaidi tafuta thread jf imevamiwa wala hutohangaika nao mtumishi
  ahsante
  Appostle Pdidy
   
 5. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #5
  Mar 18, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Inakera mno aisee.Unakuta mtu unafuatilia mada na kujifunza mambo mazuri mara ghafla inachakachulia. Unajikuta unahama moja kwa moja.
  Mods wanaweza kuweka kitufe cha kufutilia mbali michango isiyohusu.Lakini wana JF pia tunaweza kutoa mawazo ya nini kifanyike kupunguza adha hii.

  Nadhani ku delete inawezafanywa na moderators peke yao.Au nakosea?
   
 6. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #6
  Mar 18, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mi naona ni sababu wengi wa member wanakuwa hawana point za kuchangia hivyo wanaandika ili waongeze number ya post zao.

  hakika sasa JF haina jipya zaidi ya kuwa doro
   
 7. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #7
  Mar 18, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Mpendwa,
  Kama mtu hana cha kuchangia kwani lazima aseme kitu?
  Hebu fikiria uko darasani, somo linaendelea, mwalimu anauliza swali na huna jibu. Je utathubutu unyooshe kidole utamke upuuzi tu mradi uonekane umesema? Hata kama unajificha nyuma ya jina bandia, nadhani ni uungwana kujitahidi kujijengea heshima.Unavyojionyesha hapa JF hata kama watu hawakufahamu, ni tabia yako iliyojificha penda usipende. Ukionyesha tabia za ujinga hapa ujue ndani mwako una ujinga uliojificha ambao unajitahidi sana mbele za watu kuuzuia usitoke ukakuaibisha.Sijui kama kuutoa hapa JF unakusaidia kama tiba fulani?
   
 8. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #8
  Mar 18, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  Kweli WOS watu wanaharibu. Wengine huwa tunafatilia tu kama hatujui hatucomment kitu ila unaona kabisa makusudi ya watu.
  Nafikiri kikubwa ni kuwaignore hao watu. Tukiona wameingizia mambo yao yasiyohusiana na topic tunawapotezea. Kulumbana nao ni kupoteza muda. Kuna threads nyingi sana humu za kusoma.
   
 9. Avatar

  Avatar JF Gold Member

  #9
  Mar 18, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 676
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 35
  True!..
   
 10. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #10
  Mar 18, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Ni kweli yote uliyosema WoS.
  Naungana na wewe kwanza kwa kushauri wanaJF, inapotokea mtu akaingiza mambo yasiohusiana na mada tumshukie wote kwa dhati.
  Pili, kama alivyosema Husninyo wachangiaji wasimjibu 'kupotezea' wanavyosema,wamwache abwate peke yake watu wajikite kwenye mada.
  Mwisho, MoD hawa watu wanaovuruga taratibu waangaliwe kwa jicho mujarabu.
   
Loading...