Jamani wanaume heshimuni sana wake zenu

Jamani wanaume heshimuni sana wake zenu

Wanawake mna roho ya kijasiri sana.
Yani na vituko vyote tunavyowafanyia ni wachache wanaotia sumu kwenye chakula maana nyinyi ndiyo mnatupikia na kutufanyia mambo mengi kutuua dakika sufuri.
Walaaniwe wote ambao hawaheshimu wake zao ....m**** zao

Santeee

Ila ni ujinga pia kupigana na mwanamke mwingine aliyefuatwa na mumeo.

Mwenye ahadi ya kulinda penzi lenu ni mumeo sio huyo mwanamke.
Hata huyo mwanamke aliamua kujidhalilisha.

Ila huyo mwanaume ana matatizo.

kumdhalilisha mkeo mbele za watu ni utomvu wa nidhamu ... sasa kafanya hayo yote anafikiria hicho kidumu kitaweza lea wanawe ? in case mkewe katangulia mbele za haki je watoto watamchukuliaje hicho kidumu kama si kutafutia watu dhambi ya chuki bure tu....

kingene wanawake kumfuatilia mwenzio ni vizuri ila usilete ubabe na isiwe sababu ya mafarakano kila mara ndani jiulize kwa nini anafanya hivyo je wewe ni source ukijua kuwa na wewe umechangia just mpotezee give him time mpotezee kadri uwezavyo fanya majukumu yako kama kawaida kubaliana na jifanye muelewa mwisho wa siku atageuza kibao na kujitafakari pia na kujiona anakosea na atajirudi... yani jitahidi kila asemacho huendi against him hasa kama aliwezi affect watoto.. mkumbushe majukumu yake muombe pesa uwezavyo kwa upole tu akikuambia sina mjibu sawa ila ningependa kesho ukipata naomba. na usiwe na huruma kwenye majukumu hasa yanayomuhusu

kumbuka wewe ni wathamani ulingani na kidumu wala mchepuko, jithamini , kuwa na upendo kwa wote mungu lazima atakuwa upande wako

miss chagga;
Kumbe siku nyingine huwa una hekima?? Hayo ndo maneno msumari kwa wamama wenzio. Kumfuatilia mumeo ni kujitakia bp bureeee. Haya, alivyo mfuma, alimtenda nini huyo mume?? Sana sana ni matusi yakujitusi mwenyewe tu unamtukana mwanamke mwenzio. Mara ujifunge khanga ati kumpiga binti wa watu. Ndo unakumbwa na kibano from 2 people. Utawaweza??
Ungejiendea home, jifanye ka hukuona. Jitambue kuwa weye ndo mkubwa kwao. Ka ingelikuwa rahisi, kwa nini asithubutu kumleta home?? Hiyo tu, ingelimfanya mama wa watu atambe kwa hicho kidumu. Lakini unaenda leta fujo kwa watu. mshahara, kipigo kitakatifu. Pole zake

Hata kama mkewe kafanya kosa kumfuatilia mmewe ndiyo amdhalilishe kiasi hicho? Huyo mwanamme anamatatizo au yawezekana hata baba yake alikuwa anamfanyia mama yake mambo kama hayo haiwezekani mtu mwenye akili timamu ukamvue mkeo nguo hadhatani akapimwe akili sio bure..... pia huo mchepuko alichofanyiwa mwenzio nawe kisubilie tuhicho kituko cha udhalilishaji kitakukuta tu maumivu ya mkewe lazima yawapate mme na mchepuko

Hukupata hat picha ya kukamilisha story?

Majukumu kidogo yalibana ila nimerudi.. Ni hivi mke aliona dalili siku nyingiii na kusikia tetesi kwa wambea. Mara kwa mara mumewe akirudi hom Jioni huwa anatoka kidogo kwenda kwenye baa fulani tu ya jirani ambayo ndo hukutania na hiko kidada. sasa siku ya mke ndo kupanga na mwenzie eti Leo anaenda kufumania. Hio siku ndo kavaa hijabu eti mumewe asimjue. Mume wamekaa na mchepuko mke katokeza mume akamgundua vizuri tu mume akajifanya kunyanyuka kwenda haja nyuma mke kaanza kutukana mchepuko. Haa mume sijui alitoa mkanda wapi mwanamke alipigwa nusura afe na hakuna mtu kuingilia eti kisa ni mkewe.

Pole!lakini na wewe jamani huyo si ni kuku wako,mbona wamshikia manati?ungemngojea tu jioni akiingia umchinje.By the way unajua huko mchepukoni alisema nini!mke wangu ashafariki kitambo...hivyo natafuta mwengine.

Mungu anamuona

kama unanifuatilia sana kwa nini nisikudunde umenifumania na michepuko vurugu za nini ? kwani hatuwezi Ku solve case kistaarabu? nasema HAPA KUPIGA TU! maana hakuna namna

Kuna mbaba hapa kapiga mkewe nusu kufa kisa tu mkewe kamfatilia mumewe na kumkuta yupo na kidumu. Mkewe akaanza kumshambulia hiko kidumu cha mumewe weeee mwanaume alimtukana tukana mkewe dhalilisha piga piga vua nguo zote mwanamke baki na chupi tu na mbele za watu jamani na ni mkewe wa ndoa.

Wanawake tuna Kazi kubwa kwakweli hebu jaribuni basi. Pamoja na shida ghadhabu mateso kuzaa kwa uchungu kubeba mimba miezi 9 kulala upande upande kufua mikojo kufua mavi usiku kuamka kubadilisha mtoto madaso sijui pampas and all the carings needed for a baby.

Hapo bado kukupikia kukufulia kukuandalia nguo navitu fulani fulani vyote hivi mtu unafanyiwa lakini bado. Wanaume mnatakiwa kutubembeleza sanaaaaa kutuangalia kwa jicho la Tatu kutudekeza mnooooooooo kutujali kupita maelezo kutunyenyekea kutusujudu kutuheshimu sana tena sanaaaa mtupakate ikiwezekana mtubebeee Kila mahali na si kutufanyia ndivo sivo.

ukiachiwa mtoto mdogo hakika atakufa siku hiohio kama si kumpeleka kwa bibi yake sijui Shangazi yake mamdogo ambae nae ni mwanamke kwanini usimpeleke kwa baba yako babu yako kaka yako mjomba wako????.

Pamoja na hayo yooooote mwanaume akukosee bado umbembelezee umnyenyekee ilhali yeye ndo mwenye kosa kisa tu eti ndoa ni uvumilivu na mwanamke anatakiwa kuheshimu mwanaume!!!! Inshallah Umemzalia watoto jamani bado tu uishi roho juu na maisha ya wasiwasi.

Alaaniwe mwanaume anayethubutu kunyanyua kinywa chake kumtusi mkewe. Alaaniwe mwanaume anayethubutu kunyanyua mkono wake kumpiga mkewe na Mungu baba akarehemu wanaume wa hivyo wasiojua thamani ya mwanamke.
Sisi tungekua na roho ngumu kiasi hiko kuwaua ni dakika sifuri.

Majukumu kidogo yalibana ila nimerudi.. Ni hivi mke aliona dalili siku nyingiii na kusikia tetesi kwa wambea. Mara kwa mara mumewe akirudi hom Jioni huwa anatoka kidogo kwenda kwenye baa fulani tu ya jirani ambayo ndo hukutania na hiko kidada. sasa siku ya mke ndo kupanga na mwenzie eti Leo anaenda kufumania. Hio siku ndo kavaa hijabu eti mumewe asimjue. Mume wamekaa na mchepuko mke katokeza mume akamgundua vizuri tu mume akajifanya kunyanyuka kwenda haja nyuma mke kaanza kutukana mchepuko. Haa mume sijui alitoa mkanda wapi mwanamke alipigwa nusura afe na hakuna mtu kuingilia eti kisa ni mkewe.

Mimi nilifikiri mumewe anafanya umalaya kumbe anafatilia kadada kamoja tu ? Hapa shida iko wapi ?

kumdhalilisha mkeo mbele za watu ni utomvu wa nidhamu ... sasa kafanya hayo yote anafikiria hicho kidumu kitaweza lea wanawe ? in case mkewe katangulia mbele za haki je watoto watamchukuliaje hicho kidumu kama si kutafutia watu dhambi ya chuki bure tu....

kingene wanawake kumfuatilia mwenzio ni vizuri ila usilete ubabe na isiwe sababu ya mafarakano kila mara ndani jiulize kwa nini anafanya hivyo je wewe ni source ukijua kuwa na wewe umechangia just mpotezee give him time mpotezee kadri uwezavyo fanya majukumu yako kama kawaida kubaliana na jifanye muelewa mwisho wa siku atageuza kibao na kujitafakari pia na kujiona anakosea na atajirudi... yani jitahidi kila asemacho huendi against him hasa kama aliwezi affect watoto.. mkumbushe majukumu yake muombe pesa uwezavyo kwa upole tu akikuambia sina mjibu sawa ila ningependa kesho ukipata naomba. na usiwe na huruma kwenye majukumu hasa yanayomuhusu

kumbuka wewe ni wathamani ulingani na kidumu wala mchepuko, jithamini , kuwa na upendo kwa wote mungu lazima atakuwa upande wako
word

Huyo mwanaume ni wa wapi? Mwanamke hapigwi jamani khaaaa
Na huyo mwanamke nae hamnazo atashambulia vidumu vingapi, wajue tatizo liko wapi walitafutie ufumbuzi

Inaelekea huyo kidumu hajajua kuwa "kila muosha huoshwa" leo kwa mwenzie kesho itakuwa kwake na huenda akapata aibu mara mbili ya hiyo aliyofanyiwa mwenzake.

Mana wanaume sio viumbe vinavyoridhika hata umbebe mgongoni jua atachana mbeleko tu na pia huyo mke ajifunze ikiwa mume anajali familia hayo mengine aachane nayo.

Back
Top Bottom