Jamani wanaume heshimuni sana wake zenu

Mahondaw

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
67,019
168,057
Kuna mbaba hapa kapiga mkewe nusu kufa kisa tu mkewe kamfatilia mumewe na kumkuta yupo na kidumu. Mkewe akaanza kumshambulia hiko kidumu cha mumewe weeee mwanaume alimtukana tukana mkewe dhalilisha piga piga vua nguo zote mwanamke baki na chupi tu na mbele za watu jamani na ni mkewe wa ndoa.

Wanawake tuna Kazi kubwa kwakweli hebu jaribuni basi. Pamoja na shida ghadhabu mateso kuzaa kwa uchungu kubeba mimba miezi 9 kulala upande upande kufua mikojo kufua mavi usiku kuamka kubadilisha mtoto madaso sijui pampas and all the carings needed for a baby.

Hapo bado kukupikia kukufulia kukuandalia nguo navitu fulani fulani vyote hivi mtu unafanyiwa lakini bado. Wanaume mnatakiwa kutubembeleza sanaaaaa kutuangalia kwa jicho la Tatu kutudekeza mnooooooooo kutujali kupita maelezo kutunyenyekea kutusujudu kutuheshimu sana tena sanaaaa mtupakate ikiwezekana mtubebeee Kila mahali na si kutufanyia ndivo sivo.

ukiachiwa mtoto mdogo hakika atakufa siku hiohio kama si kumpeleka kwa bibi yake sijui Shangazi yake mamdogo ambae nae ni mwanamke kwanini usimpeleke kwa baba yako babu yako kaka yako mjomba wako????.

Pamoja na hayo yooooote mwanaume akukosee bado umbembelezee umnyenyekee ilhali yeye ndo mwenye kosa kisa tu eti ndoa ni uvumilivu na mwanamke anatakiwa kuheshimu mwanaume!!!! Inshallah Umemzalia watoto jamani bado tu uishi roho juu na maisha ya wasiwasi.

Alaaniwe mwanaume anayethubutu kunyanyua kinywa chake kumtusi mkewe. Alaaniwe mwanaume anayethubutu kunyanyua mkono wake kumpiga mkewe na Mungu baba akarehemu wanaume wa hivyo wasiojua thamani ya mwanamke.
Sisi tungekua na roho ngumu kiasi hiko kuwaua ni dakika sifuri.
 
mwnamke angesubiri nyumbani akauliza kwa upole mwanaume angemdanganya kwamba si kweli. Mwanamke angekubali huo uongo basi angepewa bonge la zawadi ila akijifanya mbabe matokeo ndo hayo.

Amevumilia sana inafikia hatua hiko kidada kumtambia mkewe na mwanaume hasemi kitu.. Alaaniwe
 
Kazi yangu mimi ni ulinzi...kuna mwanaume mwingine kazi yake ni rubani...mwingine ni mbeba zege etc etc...hivi unadhani risk ya hizi kazi ni mchezo? Mtu anakaa angani kwa ajili ya familia yake au anakesha kulinda mali against wahalifu unadhani ni mzaa? Alafu unatuambia kuwa tusiwapige sababu wanatufulia nguo!!!
Wewe ulipaswa kusema kitendo kilichofanywa ni cha kinyama, hapaswi kufanyiwa binadamu yeyote.....sio kwasababu mnatufulia nguo
 
Hakuna haja ya kufuatiliana kabisa hilo ni kosa kubwa sana.Timiza wajibu wako nyumbani wa kumuheshimu mume wako na kumuombea ili asione mwingine zaidi yako.Hakikisha na wewe mwanamke ni msafi kitabia na matendo.Mungu atakusimamia tu.Lakini mambo ya kumfuatilia mume achana nayo.
 
Ulikuwa unamfuatilia ili iweje? ungesubiri arudi home.
Wanawake msiendeshwe na hasira, mtaumizwa

Ila wanaume ndo muendeshwe na hasira?? Hata wanawake ni wanadamu na Wana mioyo pia
 
Soarce ya hayo matatzo yote ni mwanamke....
Bila ushawish kutoka kwa mwanamke mwanaume hawez kutenda ubaya kwa mke wake.. Kabla ya kuanza kulaani wanaume walaani kwanza wanawake wenzio...
Ktk hali ya kawaida mwanaume huchepuka na mwanamke na ndio maana siku zote adui wa mwanamke sio mwanaume bali ni mwanamke mwenzie...
Hizo laana ulizotushushia wanaume hapo juu na uzireflect kwa wanawake wenyew
 
Simuungi mkono huyo mwanaume maana si mzima kwa kitendo alichokifanya lakini pia kuna uzi wanawake waliupinga unyago (maarifa yaliyowalea mabibi zenu ambayo ndiyo yaliwafanya mzione ndoa zao zikiwa changa hadi uzeeni )sasa na mimi nawaambia hili

"ACHENI KUWAFANYA MARAFIKI NDIO WASHAURI WA NDOA ZENU NA PIA MWANAUME HACHUNGWI"
 
kumdhalilisha mkeo mbele za watu ni utomvu wa nidhamu ... sasa kafanya hayo yote anafikiria hicho kidumu kitaweza lea wanawe ? in case mkewe katangulia mbele za haki je watoto watamchukuliaje hicho kidumu kama si kutafutia watu dhambi ya chuki bure tu....

kingene wanawake kumfuatilia mwenzio ni vizuri ila usilete ubabe na isiwe sababu ya mafarakano kila mara ndani jiulize kwa nini anafanya hivyo je wewe ni source ukijua kuwa na wewe umechangia just mpotezee give him time mpotezee kadri uwezavyo fanya majukumu yako kama kawaida kubaliana na jifanye muelewa mwisho wa siku atageuza kibao na kujitafakari pia na kujiona anakosea na atajirudi... yani jitahidi kila asemacho huendi against him hasa kama aliwezi affect watoto.. mkumbushe majukumu yake muombe pesa uwezavyo kwa upole tu akikuambia sina mjibu sawa ila ningependa kesho ukipata naomba. na usiwe na huruma kwenye majukumu hasa yanayomuhusu

kumbuka wewe ni wathamani ulingani na kidumu wala mchepuko, jithamini , kuwa na upendo kwa wote mungu lazima atakuwa upande wako
 
Back
Top Bottom