Jamani wanaume heshimuni sana wake zenu

Jamani wanaume heshimuni sana wake zenu

unajua mpaka nanyanyua mkono wangu nampiga mwanamke ujue amenishawishi vya kutosha ndo maana nimempiga... laiti asingeanzisha vurugu kwa huyo kidumu unachosema yangeisha kistaarabu.. huwez jua huyo kidumu alikuwa nani yake.. wewe ndo unaona kidumu ila kwangu huenda ni mtu mwingine wa heshima sana!
 
Kuna mbaba hapa kapiga mkewe nusu kufa kisa tu mkewe kamfatilia mumewe na kumkuta yupo na kidumu. Mkewe akaanza kumshambulia hiko kidumu cha mumewe weeee mwanaume alimtukana tukana mkewe dhalilisha piga piga vua nguo zote mwanamke baki na chupi tu na mbele za watu jamani na ni mkewe wa ndoa.

Wanawake tuna Kazi kubwa kwakweli hebu jaribuni basi. Pamoja na shida ghadhabu mateso kuzaa kwa uchungu kubeba mimba miezi 9 kulala upande upande kufua mikojo kufua mavi usiku kuamka kubadilisha mtoto madaso sijui pampas and all the carings needed for a baby.

Hapo bado kukupikia kukufulia kukuandalia nguo navitu fulani fulani vyote hivi mtu unafanyiwa lakini bado. Wanaume mnatakiwa kutubembeleza sanaaaaa kutuangalia kwa jicho la Tatu kutudekeza mnooooooooo kutujali kupita maelezo kutunyenyekea kutusujudu kutuheshimu sana tena sanaaaa mtupakate ikiwezekana mtubebeee Kila mahali na si kutufanyia ndivo sivo.

ukiachiwa mtoto mdogo hakika atakufa siku hiohio kama si kumpeleka kwa bibi yake sijui Shangazi yake mamdogo ambae nae ni mwanamke kwanini usimpeleke kwa baba yako babu yako kaka yako mjomba wako????.

Pamoja na hayo yooooote mwanaume akukosee bado umbembelezee umnyenyekee ilhali yeye ndo mwenye kosa kisa tu eti ndoa ni uvumilivu na mwanamke anatakiwa kuheshimu mwanaume!!!! Inshallah Umemzalia watoto jamani bado tu uishi roho juu na maisha ya wasiwasi.

Alaaniwe mwanaume anayethubutu kunyanyua kinywa chake kumtusi mkewe. Alaaniwe mwanaume anayethubutu kunyanyua mkono wake kumpiga mkewe na Mungu baba akarehemu wanaume wa hivyo wasiojua thamani ya mwanamke.
Sisi tungekua na roho ngumu kiasi hiko kuwaua ni dakika sifuri.
Baby za siku,mbona ukavunja ahadi mamii,yaani ukaniacha naumia.
 
Majukumu kidogo yalibana ila nimerudi.. Ni hivi mke aliona dalili siku nyingiii na kusikia tetesi kwa wambea. Mara kwa mara mumewe akirudi hom Jioni huwa anatoka kidogo kwenda kwenye baa fulani tu ya jirani ambayo ndo hukutania na hiko kidada. sasa siku ya mke ndo kupanga na mwenzie eti Leo anaenda kufumania. Hio siku ndo kavaa hijabu eti mumewe asimjue. Mume wamekaa na mchepuko mke katokeza mume akamgundua vizuri tu mume akajifanya kunyanyuka kwenda haja nyuma mke kaanza kutukana mchepuko. Haa mume sijui alitoa mkanda wapi mwanamke alipigwa nusura afe na hakuna mtu kuingilia eti kisa ni mkewe.
Nimeamini waenda baa akili zao wote zinafanana, yaani kati ya wooote hakuna hata alojiongeza kumsaidia huyo mwanamke alokuwa anapigwa!!!
 
Huyo mwanaume ni wa wapi? Mwanamke hapigwi jamani khaaaa
Na huyo mwanamke nae hamnazo atashambulia vidumu vingapi, wajue tatizo liko wapi walitafutie ufumbuzi
Walivyo utajikuta umepigana na mtaa mzima,mwisho uonekane mwehu.
 
Anampenda sana ila ni hasira tu za Mwezi January, ndio maana yule Mgosi alimuita mwanae hilo jina! Ni mwezi wa kununa, hasira na visirani hadi February
 
Mungu hakusema tuwaheshimu.. Alisema tuwapende..
Kutii na kuheshimu ni kazi yenu..
 
Mungu hakusema tuwaheshimu.. Alisema tuwapende..
Kutii na kuheshimu ni kazi yenu..
And unajua upendo hushinda yote?
Ukimpenda utamuheshimu,kumtii,kumjali,kumtunza,kumlinda,kumthamini na vyote vya kufanana navyo.

Ukimpiga then umetoka kwenye misingi husika.
 
Mkeo kabisa!! ' mbele za watu kabisaa!!!!! Utakua na upungufu wa akili na ulaaniwe
Huyo mwanamke alitenda mbele za watu ili kumdhalilisha mumewe. Siafiki kitendo hicho, lakini yeye pia alikosa hekima. Halafu alipaswa kumshambulia mume, sio yule hawara
 
And unajua upendo hushinda yote?
Ukimpenda utamuheshimu,kumtii,kumjali,kumtunza,kumlinda,kumthamini na vyote vya kufanana navyo.

Ukimpiga then umetoka kwenye misingi husika.
Wanawake wa kupenda katika kizazi hiki cha Beijing? Wanawake mnaojazana humu jf mkiomba ushauri jinsi ya kuishi na mama mkwe kwa sababu anawatembeleeni!?
 
Wanawake wa kupenda katika kizazi hiki cha Beijing? Wanawake mnaojazana humu jf mkiomba ushauri jinsi ya kuishi na mama mkwe kwa sababu anawatembeleeni!?
Kwahiyo unapingana na Mungu? Kama hayo ndio mawazo yenu then basi hata usiwalaumu.
Bora hao waloomba ushauri kuhusu kuishi na mama mkwe kuliko nyie mlojazana kuelezana namna za kuchepuka na kupiga wake zenu.
 
Huyo mwanamke alitenda mbele za watu ili kumdhalilisha mumewe. Siafiki kitendo hicho, lakini yeye pia alikosa hekima. Halafu alipaswa kumshambulia mume, sio yule hawara
Kwahiyo unashindana na mkeo na kulipana visasi? Ndio akili yako ilipooishia? Hivi ile akili mloambiwa muitumie huwa mnaitumia wapi?
 
Kuna mbaba hapa kapiga mkewe nusu kufa kisa tu mkewe kamfatilia mumewe na kumkuta yupo na kidumu. Mkewe akaanza kumshambulia hiko kidumu cha mumewe weeee mwanaume alimtukana tukana mkewe dhalilisha piga piga vua nguo zote mwanamke baki na chupi tu na mbele za watu jamani na ni mkewe wa ndoa.

Wanawake tuna Kazi kubwa kwakweli hebu jaribuni basi. Pamoja na shida ghadhabu mateso kuzaa kwa uchungu kubeba mimba miezi 9 kulala upande upande kufua mikojo kufua mavi usiku kuamka kubadilisha mtoto madaso sijui pampas and all the carings needed for a baby.

Hapo bado kukupikia kukufulia kukuandalia nguo navitu fulani fulani vyote hivi mtu unafanyiwa lakini bado. Wanaume mnatakiwa kutubembeleza sanaaaaa kutuangalia kwa jicho la Tatu kutudekeza mnooooooooo kutujali kupita maelezo kutunyenyekea kutusujudu kutuheshimu sana tena sanaaaa mtupakate ikiwezekana mtubebeee Kila mahali na si kutufanyia ndivo sivo.

ukiachiwa mtoto mdogo hakika atakufa siku hiohio kama si kumpeleka kwa bibi yake sijui Shangazi yake mamdogo ambae nae ni mwanamke kwanini usimpeleke kwa baba yako babu yako kaka yako mjomba wako????.

Pamoja na hayo yooooote mwanaume akukosee bado umbembelezee umnyenyekee ilhali yeye ndo mwenye kosa kisa tu eti ndoa ni uvumilivu na mwanamke anatakiwa kuheshimu mwanaume!!!! Inshallah Umemzalia watoto jamani bado tu uishi roho juu na maisha ya wasiwasi.

Alaaniwe mwanaume anayethubutu kunyanyua kinywa chake kumtusi mkewe. Alaaniwe mwanaume anayethubutu kunyanyua mkono wake kumpiga mkewe na Mungu baba akarehemu wanaume wa hivyo wasiojua thamani ya mwanamke.
Sisi tungekua na roho ngumu kiasi hiko kuwaua ni dakika sifuri.
Dah.. This is so sad

Kuhusu huyo mwanamke kumpiga huyo mwanamke mwenzie, sio sawa kwa sababu huwezi jua aliambiwa nini na huyo mwanaume wakati anatongozwa, lakini hapaswi kulaumiwa pia kwani kila mtu ana namna yake ya kurespond kwenye situation ya hasira tukumbuke kuwa inauma sana kushare mapenzi na mtu unayempenda.

Kuhusu huyo mwanaume kumpiga mkewe na kuside na huyo mchepuko wake hii sio hali ya kawaida, ni unyama uliopitiliza ambao ukiangalia kiroho huo ni ushetani unaohitaji Mungu aingilie kati (umekutwa na mchepuko but still unapata ujasiri wa kumpiga mke wako) hapa kuna tatizo kubwa ambalo neither huyo mwanamke (mke) nor mwanaume can solve.. Kibinadamu solution haiwezi kupatikana unless kuachana tu hii ndoa ilishakufa moyoni especially kwa huyo mwanaume. Kwa upande wa huyo mwanamke since ndio ameonekana bado anahitaji hiyo ndoa iendelee aingie kwenye sala tu ndio kitu cha mwisho kilichobaki kutatua mgogogoro wa ndoa hiyo. Hayo mambo kibinadamu yameshindikana. Pole nyingi zimfikie huyo mama.
 
Nimeamini waenda baa akili zao wote zinafanana, yaani kati ya wooote hakuna hata alojiongeza kumsaidia huyo mwanamke alokuwa anapigwa!!!

Wee anaethubutu kumsaidia nae kipigo vilevile eti Waache ampige coz ni kesi ya mume na mke so wengine msiingilie
 
Back
Top Bottom