Jamani wajawazito wanatozwa pesa vituo vya afya vya serikali

vibee

Member
Mar 5, 2014
49
21
Wanajamvi habari zenu,
Katika hili numeamua kulianika kwa maana nimekwenda katika kituo cha afya na wife na kumkuta Dr in charge was kituo na kututoza 12000 Tsh KWA ajili ya kumpima wife.

Kiukweli huyu jamaa hafai kwa maana usipolipa hampati huduma.Ningeomba wanajamvi huyu jamaa ashughulikiwe.
 
Mkuu Lete Habari Kamili Wajawazito Na Watoto Chini Ya Miaka Mitano Ni Bure
Taja Sehemu Ya Hicho Kituo
 
Hiyo bure iko kwenye makaratasi na majukwaa ya wanasiasa, lakini huku field sio kabisa.

Vituo vingi vya kutolea huduma za afya ni majengo na watoa huduma tu(kama wapo) lakini vitendea kazi, dawa na vifaatiba hakuna.

POLENI WATANZANIA
 
Ujinga Ni Kuacha Kushtaki Sehemu Stahili Na Kuleta Habari Isiyoeleweka Hapa Jf! So Sisi Ndo Tuotee Jina La Hiyo Hospitali Na Daktari?
 
Serikali yangu inasema kwamba wafuatao wanapaswa kupewa matibabu bure:
  1. watoto chini ya miaka mitano
  2. wanawake wajawazito
  3. wazee zaidi ya miaka 60
  4. +/- wasiojiweza

Ila kiuhalisia, hili linawezekana tu pale ambapo vifaatiba, dawa na documentation papers zinapatikana. Kuna dawa ambazo mama mjamzito anatakiwa apewe bure kwa mfano zile za kuongeza damu, za minyoo, n.k. Pia kadi anapaswa apatiwe bure na ndimo mnaandikwa taarifa zake za huo ujauzito. Cha ajabu, Serikali mara nyingi tu huwa hawapeleki hivi vitu vituoni ila kwenye majukwaa ya siasa wanasema vipo na mtavikuta bure. Hili huwa linawapa wagonjwa/ wateja wakati mgumu sana na pia watoa huduma za afya huwa na wakati mgumu kujieleza kwao kwamba hawana hivyo vitu.

Ila pia kwa upande mwingine, wahudumu wanaweza wakawa wameasi viapo vyao na kuona wakati huu wa ujauzito kama 'cash cow' na hivyo kuanza kuwanyanyasa na kuwachangisha wateja wao pesa.

Nasikitika kwamba mwisho wa siku, anaeumia ni mlipa kodi mwenzangu.
 
Kweli mwisho wa siku anayeumia ni mlipa kodi. Lakini, hoja iliyopo menzani ni huyu bwana kwamba mkewe ametakiwa atoe shilingi elfu 12 kinyume cha sera ya huduma za afya, huyo anayekusanya hizo pesa anatoa wapi hivyo vifaa tiba katika kituo cha kutoa huduma mali ya serikali ambayo yenyewe imeshindwa kupeleka hivyo vifaa hapo kwenye kituo chake!

Kama serikali imeshindwa kutoa vifaa tiba, ieleweke hivyo lakini suala la kugeuza vituo hivyo kuwa ni sehemu ya kukusanya fedha za wagonjwa nafikiri halijakaa sawa na wahusika wachukuliwe kuwa ni wezi sawa na wezi wengine.

Mto mada unafanya makaosa kwa kuendelea kuchelewa kutaja kituo ulichokumbana na kadjhia hiyo na nenda mbele utaje muda na siku ambayo tukio limetokea na pia taaja jina la mhusika. Name and shame!
 
Wanajamvi habari zenu,
Katika hili numeamua kulianika kwa maana nimekwenda katika kituo cha afya na wife na kumkuta Dr in charge was kituo na kututoza 12000 Tsh KWA ajili ya kumpima wife.Kiukweli huyu jamaa hafai kwa maana usipolipa hampati huduma.Ningeomba wanajamvi huyu jamaa ashughulikiwe.

endekeza uchoyo utakufa unajiona,hii ndo tanzania bana,bila kununua haki mambo hayaendi.utajikuta unakufa na hakuna mtu wa ku responsible.hasara kwako
 
Mbona kidogo sanaa Mkuu. Elfu 12 tuu unalia hivyo ?! Au ulitaka ukalie chips kuku ukitoka clinic ? Elewa kwasasa hakuna kitu cha buree. Usisahau ule usemi , "Akili za kuambiwaa "
 
Mbona kidogo sanaa Mkuu. Elfu 12 tuu unalia hivyo ?! Au ulitaka ukalie chips kuku ukitoka clinic ? Elewa kwasasa hakuna kitu cha buree. Usisahau ule usemi , "Akili za kuambiwaa "

Kwako ndogo kwake ni kubwa, pia hata wewe ulizonazo kuna matajiri bongo wataona ni za kununulia pipi watoto.
 
Kwako ndogo kwake ni kubwa, pia hata wewe ulizonazo kuna matajiri bongo wataona ni za kununulia pipi watoto.

Sasa kama kugaramia upimaji wa ujauzito analia hivyo, kulea mtoto ataweza ?! Nguo , Chakula, na baadae Shule si ndo ataikimbia family kabisa.
Jipangeni jamani. Ujauzito sio dharura, ni swala la kupanga. Bure bure imekwisha siku hizi. Tusidanganyane.
 
Kwani kodi kazi yake ni nini? Na hiyo sera imewekwa ili itekelezwe, sasa jamaa anatoa feedback ya implementation ya sera wewe unamwona hafai. Inaonekana wewe unaongea kwa sababu una health insurance ya ofisi yako. Hivi unajua rate ya poverty kwa sasa Tanzania?

Kwenye hiyo picha chini unafikiri wote wanaipenda hali hiyo?

Tanzania_mothers_459847artw.jpg

Tafuta sababu ya Naomi Campbell kulia kiasi hicho kama kafiwa (picha hapo chini)
Naomi%20lia.jpg
 
watanzania ni shida sana.
mnapenda mno vya bure.
usikute huyu kaenda anataka dr ‘fulani' ndio amuone huyo mgonjwa aafu anataka iwe bure.
hakuna vya bure siku hizi.

kuna mtu aliwahi kupiga simu kwa dr jumamosi anaomba amuone mkewe kaumia mkono kaambiwa ampeleke hospitali ya private ndio amuone.
jamaa akaanza kulalamika eti oooho unajua pale ni gharama na sababu kibao!!!
sasa we unataka kumtoa dr wikiend kwake, asafiri aje akuonee mgonjwa wako bure???
hakuna cha bure siku hizi.
 
Kwani kodi kazi yake ni nini? Na hiyo sera imewekwa ili itekelezwe, sasa jamaa anatoa feedback ya implementation ya sera wewe unamwona hafai. Inaonekana wewe unaongea kwa sababu una health insurance ya ofisi yako. Hivi unajua rate ya poverty kwa sasa Tanzania?

Kwenye hiyo picha chini unafikiri wote wanaipenda hali hiyo?

Tanzania_mothers_459847artw.jpg

Tafuta sababu ya Naomi Campbell kulia kiasi hicho kama kafiwa (picha hapo chini)
Naomi%20lia.jpg

Bongo wanaolipa kodi kikamilifu ni wafanyakazi tuu. Kwenye kila kitu wanaotuokoa ni wafadhili. Hadi hizo Clinic na wodi za wazazi zoote ni misaada.

Imefikia wakati tuambiane ukweli. Huduma za a uzazi bure imeshindikana. Hii itasaidia watu kupanga uzazi. Lasivyo, tutaendelea kuzalisha ma-jobless na wezi.
 
Mkuu sio za uzazi pekee hata za watoto na wazeee na wale wa msamaha....serikali inashindwa kulipa deni la MSD kwasababu inanunua dawa na mwisho wa Siku inazitoa bure ukizingatia almost asilimia 70 ya wagonjwa wetu ndo hao wazazi,wazee na watoto.
 
Yaani upande wakinamama wajawazito ni shida sana unaweza kufa kwa gloves tu kama hujaenda nazo hutopata huduma lambda ununue kwa Nesi husika.mi huwa najiuliza hivi izi wanazouziwa wagonjwa manesi wanazipata wapi kwa kweli inauma sana ukizingatia mtu unakatwa hela chungu nzima Za kod.kwa kweli hospital za serikali wanatakiwa wabadilike
 
Sasa kama kugaramia upimaji wa ujauzito analia hivyo, kulea mtoto ataweza ?! Nguo , Chakula, na baadae Shule si ndo ataikimbia family kabisa.
Jipangeni jamani. Ujauzito sio dharura, ni swala la kupanga. Bure bure imekwisha siku hizi. Tusidanganyane.

Mkuu umenivunja mbavu!!
Bei ya pampers na wipes ataiweza??

Kimsingi hakuna huduma za bure ...hiyo inayoitwa bure kuna mfadhili kalipia na siku akigoma ndio hivyo tena.
 
Wanajamvi habari zenu,
Katika hili numeamua kulianika kwa maana nimekwenda katika kituo cha afya na wife na kumkuta Dr in charge was kituo na kututoza 12000 Tsh KWA ajili ya kumpima wife.

Kiukweli huyu jamaa hafai kwa maana usipolipa hampati huduma.Ningeomba wanajamvi huyu jamaa ashughulikiwe.

hujataja ni wa kituo gani cha afya? ulienda lini na mkeo?ilikuwa jumangapi na saa ngapi? jina lake nani? sasa hapa unataka tumshughurikiaje ikiwa hata jina lake hukulitaja na ni wa kituo gani?jipange upya.
 
Back
Top Bottom