Nairobifly
Member
- May 3, 2012
- 75
- 26
Wiki hii vyombo vingi vya habari hususan
magazeti yameripoti vifo vya watu waliokufa kutokana na njaa katika Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro (NCA). Mbali na vifo hivyo kuripotiwa lakini pia kuna habari kuwa wananchi wanaoishi eneo hilo wameanza kukimbialia maeneo mbalimbali ndani ya nchi na hata nchi jirani ya Kenya kwa lengo la kutafuta maisha na pia baadhi ya familia zimeanza kusambaratika. Sababu ya mlipuko wa njaa ktk eneo hilo ni baada ya serikali kukataza kilimo cha kujikimu (subsistance cult.). Ikumbukwe kuwa eneo hilo linatambulika kama ardhi mseto (multiple land use). Kitendo cha serikali kunyima kilimo hicho ilionekana ni ukiukwaji wa haki za binadamu na baadhi ya wataalam akiwemo gwiji wa masuala ya sheria Prof.ISSA SHIVJI hasa ktk kitabu chake cha THE MASAI RIGHT IN NCA. Katika utafiti wake kuhusu suala la kilimo ktk eneo hilo alimshirikisha vyema tena kwa karibu mtaalam/mhe. TUNDU LISSU kama research ass.wake. Ninacho amini kama mfuasi wa cdm ni kwamba cdm ni mkombzi wa mtz, swali langu ni kwanini cdm au uongozi wake ukiwemo wewe LISSU mko kimya wakati watz wanaangamia kwa njaa? Kama upo humu nakuomba useme chochote kwani unafahamu fika kuhusu kinachowakumba watz wenzetu huko. Karibuni kwa kuchangia wandugu