NyaniMzee
JF-Expert Member
- Nov 24, 2010
- 396
- 727
Wakuu, juzi nilisafiri kwa gari binafsi toka Moshi kuja Dar es salaam. Nilikuwa mwangalifu sana na speed limit hasa zile za 50.
Nilipofika Mombo nikasimamishwa na Trafiki wakasema kuna eneo lenye speed limit ya hamsini eti nilipita kwa speed 62/saa. Nikawaeleza kuwa sijavuka spidi hiyo kwenye kibao chochote tangu nitoke Moshi.
Eti wakanionyesha picha gari yangu waliyotumiwa na mmoja wao (nadhani atakuwa alijificha porini na speed camera) nikawambia hio sio conclusive evidence kuwa nilikuwa katika eneo la kwenda spidi 50 kwa vile hakuna ushahidi kuwa nilikuwa ndani ya eneo lenye spidi limit.
Hakuna picha ya kibao chochote kinachoonyesha gari langu lilikuwa katika eneo hilo. Walichoniambia hao trafiki eti kama nina shaka basi wanipeleke Mahakamani. Nikawaambia twendeni na mthibitishe kuwa kweli nilikuwa katika range ya 50km/hr na mkishindwa mtanilipa fidia za usumbufu.
Baada ya malumbano wakanirudishia Driving licence yangu wakaniambia we jamaa mbishi sana.
Nilichojifunza ni kuwa hawa trafiki wanapiga picha popote tu wanarushiana ili watengeneze malipo. Kwa kweli kuna maonezi makubwa sana barabarani. Wana JF wenzangu nimeona niwashirikishe katika hili tusikie na tusikie experience za wengine waliokumbwa na masaibu haya