briophyta plantae
Senior Member
- Feb 18, 2017
- 114
- 129
Arusha ni jiji lenye hadhi yake ya kipekee katika nchi yetu.kwanza ni jiji la kitalii na pili lina utamaduni wake wa kipekee sana.
Changamoto ipo katika mtazamo kabla hujalifikia hili jiji,picha unayokuwa nayo kichwani ni kwamba arusha ni mji mzuri sana,uliostaarabika sana na wenye elimu,biashara na ubunifu wa kibiashara,mpangilio mji na usafi,watalii kibao n.k
Nilikuwa arusha kwa siku tatu juzi tu na kwakweli ni mkoa wa kipekee sana ila ndo hvyo kila kizuri hakikosi kasoro:
KWA MOROMBO kwenye nyama choma. Asee hii sehemu ni maarufu sanaa,hata nikiwa mbeya,dar na mwanza nilikuwa nikipasikia sanaa, na nyama inachomwa sana hapa,ila pako local vibaya mnoo, na hivi vi mvua mvua aisee ni kuchafu sanaa. Hii sehemu kwa heshima na umaarufu wake nashauri tu pangeandaliwa mazingira yake yawe mazuri na ya kipekee hata kwenye AFCON patakuwa na wageni wengi sana hapa nina uhakika.
SOKO LA KILOMBERO: Moja ya eneo ambalo ustaarabu ni sifuri ni hapa kilombero,hapana mpangilio wa kitu chochote, foleni, uchafu, miundombinu, maji taka ndo usiseme,mikokoteni,bodaboda n.k. Hapo hapo kuna kama mall kubwa tu(wanapaita TFA) na supermarket ya maana kabisa (shopers) watalii wanapishana hapo ni kuingia na kutoka ila hayo mazingira sijui yanaleta picha gani. Serekali isaidie kufanya namna hapa maana hata hiyo barabara ukiiona.
DALADALA: Daladala za huku unaingia mzima tu, ila unashuka ukiwa unachechemea,huko ndani ni kubanwa,kukunjwa,kupangwa yani tafrani. Kwa jiji kama Arusha hapana aisee hii sio sawa kuwa na vigari kama hv eti ndio usafiri wa umma. Kwanza ndio vinafanya foleni inakuwa kubwa na ni vibovu hatari, ANGALIZO:-bajaji nazo ni zakuwekewa mipaka,mtakuja kuona umuhimu wake
MIPANGO MIJI: Hawa watu huwa sijuagi kazi yao hasa ni nini maana hii miji hata kupagwa inapangwa sasa,watu wanajenga shaghalabagala,hata ukija katikati ya mji kuna nyumba za ajabu ajabu.kuna kipindi nilikuja tena arusha, hapa kaloleni kulikuwa kuna mtaa unaitwa magorofani,saiv yale majengo wamebomoa halafu what next 😂😂😂 hakuna kitu kinafanyika pale, watu wanapaki magari tu na kuna bar wanalewa kuanzia asubuhi mpaka jioni.ukija ule mtaa wa kaloleni nyuma ya polisi kwenda tank la maji,wamebomoa zile nyumba zote za kizamani ila hapajaendelezwa chochote,kumekuwa msitu tu, siongelei ungaltd wala ngarenero,nipaache tu.
MIUNDOMBINU: Barabara nyingi ni mbovu sana na pia haziwezi kumudu ongezeko la matumizi ya barabara kwa sasa, magari ni mengi, parking hakuna so watu wanapaki barabarahi tu na kusababisha foleni zisizo za lazima, miferiji ya maji mingi imeziba na michafu mnoo, huko Sakina, Ngaramtoni, Mianzini, Ungaltd hakuna barabara za mitaa ile ni mito ya kupitisha maji.
Samaki mkunje angali mbichi,huu mji unazidi kukua,kama ni kubadili baadhi ya mambo kuuweka mji uwe sawa na maridadi muda ni sasa,huko mbeleni kazi itakuwa ni ngumu haswa kukishaharibika kabisa.
Nawasilisha kwenu.