BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,769
- 288,283
Kama uelewa ni finyu mie siwezi kukusaidia.
Sidhani kama kuna ukweli hapo..
Sidhani kama kuna ukweli hapo..
Wakuu, juzi nilisafiri kwa gari binafsi toka Moshi kuja Dar es salaam. Nilikuwa mwangalifu sana na speed limit hasa zile za 50.
Nilipofika Mombo nikasimamishwa na Trafiki wakasema kuna eneo lenye speed limit ya hamsini eti nilipita kwa speed 62/saa. Nikawaeleza kuwa sijavuka spidi hiyo kwenye kibao chochote tangu nitoke Moshi.
Eti wakanionyesha picha gari yangu waliyotumiwa na mmoja wao (nadhani atakuwa alijificha porini na speed camera) nikawambia hio sio conclusive evidence kuwa nilikuwa katika eneo la kwenda spidi 50 kwa vile hakuna ushahidi kuwa nilikuwa ndani ya eneo lenye spidi limit.
Hakuna picha ya kibao chochote kinachoonyesha gari langu lilikuwa katika eneo hilo. Walichoniambia hao trafiki eti kama nina shaka basi wanipeleke Mahakamani. Nikawaambia twendeni na mthibitishe kuwa kweli nilikuwa katika range ya 50km/hr na mkishindwa mtanilipa fidia za usumbufu.
Baada ya malumbano wakanirudishia Driving licence yangu wakaniambia we jamaa mbishi sana.
Nilichojifunza ni kuwa hawa trafiki wanapiga picha popote tu wanarushiana ili watengeneze malipo. Kwa kweli kuna maonezi makubwa sana barabarani. Wana JF wenzangu nimeona niwashirikishe katika hili tusikie na tusikie experience za wengine waliokumbwa na masaibu haya
Radar detector. Itakujulisha 999m kabla ya kuifikia camera ilipo. Kama camera wameset sehemu ya speed 80kmph simu itakuambia speed isizidi 80kmph mita 999 kabla haujaifikia police camera. Ili kuepuka kesi mbele fanya ku screenshot hata picha nne kama ushahidi wakikukamata maana speed yako ya gari inasoma moja kwa moja kwenye simu yakoKaka hyo app inaitwaje?
Mpk mtakapoacha KUFANYA makosa...na usifananishe polisi na tra kwa sab polisi/traffic unalipa unapokuwa na makosa tu lkn tra analipa kila mtu na idara nyingi tu za serikali zinatoza ada fine na tozo mbali mbali km vile mahakama kupitia fine halmashauri za vitongoji vijiji miji na majiji Je zote hizo ni TRAWanashindana na TRA kukusanya mapato!
Tra hawatozi fine Bali kodiSikuiz wamekuwa TRA. Ila ukiwadindia wanakuacha...
Mimi ninayo ile app ya kujua cameta ziko wapi. Cha kushangaza unaweza kuwa unaendesha gari polini kabisa na hakuna kibao cha 50 lkn utasikia simu ina toa alarm na kukujulisha kuwa kuna camera. Huo ni uthibitisho kuwa hela inatafutwa kwa lazima. Huu utaratibu wa kurusha picha ni mbovu hakuna mfano
Jina asee maana haya mambo mazrmazr sio ya kuwa nayo mwenyewe
Naomba unisaidie hiyo app mkuu
Inaitwaje hiyo mkuu itusaidie na sisi
hyo app inaitwaje ?
Kaka hyo app inaitwaje?
Ivi iyo app inapatikana playstore? Mkuu nijuze
Mnaona tutafaidi mkiitaja hiyo app ya kamera eeh?
speed cameras and traffics sygicApp inaitwaje mkuu
Nilikuwaga nayo hii... Hivi inafanya kazi kiuhakika kabisa au magumashi?
Mimi ninayo ile app ya kujua cameta ziko wapi. Cha kushangaza unaweza kuwa unaendesha gari polini kabisa na hakuna kibao cha 50 lkn utasikia simu ina toa alarm na kukujulisha kuwa kuna camera. Huo ni uthibitisho kuwa hela inatafutwa kwa lazima. Huu utaratibu wa kurusha picha ni mbovu hakuna mfano
Ulweli ni kwamba binadam hatoacha kufanya makosa. Sema tu labda yapungue.. lakin daima binadam hukosea tu. Hapo ndipo system wanapochotea hela ...coz wanajua no matter what watu watavurunda na hela watalipa.Mpk mtakapoacha KUFANYA makosa...na usifananishe polisi na tra kwa sab polisi/traffic unalipa unapokuwa na makosa tu lkn tra analipa kila mtu na idara nyingi tu za serikali zinatoza ada fine na tozo mbali mbali km vile mahakama kupitia fine halmashauri za vitongoji vijiji miji na majiji Je zote hizo ni TRA
Mi nadhani mleta mada amekosea jambo moja ambalo watanzania wengi wanalifanya.
Radar haikuwekwa kwa ajili ya kupiga vibao vya alama za barabarani.
Madereva wengi sana hawajui na hawakusoma kanuni na sheria za barabarani japo wanaweza kuendesha magari kutokana na kuwa wanamiliki magari au wamezaliwa kwenye familia zinazomiliki magari.
Kanuni ziko wazi kuwa maeneo yote yenye makazi ya watu speed ya gari isizidi 50 kph.
Pia maeneo yenye lona kali n.k.
Cha ajabu dereva anapigwa picha maeneo hayo halafu anakuja kutulalamikia hapa kuhusu vibao.
Miaka iliyopita hao hao wanaolalamikia radar walikua wakilalamikia kukithiri kwa ajali. Na cha ajabu waliokua wanalalamikiwa ni trafiki kama vile wao ndio wanaoendesha hayo magari huko barabarani.
Serikali na jamii imepata hasara kubwa sana kutokana na ajali za barabarani.
Kwa sasa ajali zinazotokana na magari makubwa kama Malori na mabasi zimepungua sana. Ajali zinazotokea mara kwa mara na zilizobaki ni za hao madereva wanaopenda kukaidi sheria na kubishana na serikali kwa kujifanya wajuaji wa kutafita vifaa vya kung'amua zilipo radar, ambao wengi wao ni madereva wa magari madogo na madereva wa bodaboda. Tochi za barabarani zimepunguza ajali kwa kiwango kikubwa sana ukilinganisha na kipindi cha kabla ya matumizi ya radar hasa ukizingatia kwa sasa kuna magari mengi sana barabarani.
Serikali haiwezi kukaa kimya na kuangalia madereva wachache wazembe wanaua maelfu ya watu barabarani eti kwa sababu wanataka kuwahi bila kuzingatia sheria za usalama barabarani.
Barabara zetu ni finyu na wananchi wanakimbilia kujenga na kufanya shughuli za kibiashara karibu na barabara.Ni wajibu wa serikali kudhibiti madereva ili kuepusha ajali kwa watuamiaji wote wa barabara.
Kuna wakati mmoja Rais mstaafu Mkapa aliwahi kusema kuwa alifika Marekani na kusikia msemo mmoja kuwa mwafrika akiwa anaendesha gari anakuwa "mwendawazimu" (Yaani hajali na hahofii kitu chochote. Anajiona kuwa yupo salama sana. Anakua jasiri sana. Kiburi sana . Dharau sana. Kujihisi ni mtu wa tofauti sana. Hagusiki na haambiliki. Mjuaji wa kila kitu n.k. )
Kwa kweli kwa mtu anayetokea Ukanda huo wa kaskazini ,mikoa ya Arusha na Kilimanjaro mwenye umri zaidi ya miaka 30 na mwenye akili timamu na kumbukumbu za kutosha hawezi kupuuza jitihada za serikali na jeshi la polisi katika kudhibiti mwendo kasi.
Miaka ya nyuma mtu akipanda basi kutoka Dar es salaam kwenda Moshi ilikua ni kama vile mtu swala anishi serengeti na kupita katikati ya kundi la Simba. Akifika salama bila kupata ajali ilikua ni kama bahati. Kuna makampuni ya mabasi yaliyokuwa yamejizolea jina baya la kuua watu kwa ajali, mpaka imani zikajengeka kuwa ni kafara za matajiri na madereva wao.
Hali kadhalika barabara ya Dar Moro ajali zilikua ni za kutazamia kila siku. Leo hii watu tunasafiri kwa amani kabisa. Wajinga wachache ndio bado wanakwepa tochi kwa kusafiri usiku na kujikuata wanaishia kupata ajali kwa kusinzia na mwendo kasi. Asubuhi wanajikuta wapo hospitalini au magari yao yakowa nyang"anyang"a na kuanza kulaumu trafiki kuwa hawazuii ajali. Watazizuia vipi kama watu hawataki kufuata sheria.
Na ukifanya utafiti wa kutosha utagundua kuwa ajali zilizobaki nyingi zinawahusu watumishi wa serikali wenye nafasi kwenye serikali kwa sababu wengi hawapendi kufuata sheria za usalama baranarani.
Ningeishauri serikali ya awamu hii ya tano baada ya kuhakiki vyeti vya watumishi wa umma sasa iwe ni zamu ya kuhakiki vyeti vya uderevya na vyuo waliposomea kuanzia wale wa magari binafsi. Haiwezekani kuwaacha watu watembee barabarani na vyombo vyenye uwezo wa kupoteza maisha ya watu wakati hawana elimu ya kutosha juu ya sheria na kanuni za matumizi sahihi ya vyombo hivyo .
Watu wachache kwa uzembe wao wanatumia muda mwingi kuwatukana na kuwakashfu askari wetu wa usalama barabarani bila kuangalia jamii kubwa iliyonufaika na udhibiti wa kwendo kasi.
Wakati utakapofika wa kuwa na barabara zenye viwango vya speed kubwa kila mtu atachagua barabara ya kupita kulingana na mwendo anaoutaka lakini kwa sasa tutumie barabara zilizopo kwa tahadhari kubwa kwani kila mtu anapita humo humo kuanzia madereva malearner na wale mahiri, wasukuma mikokoteni na watembea kwa miguu wote ni humo.
Maisha ya mtu hayana spea. Ndugu yako akikatwa miguu kwa uzembe wa dereva mwingine inauma sana unatamani ungekuwepo hapo ili naye umkate mguu au hata kichwa. Hasa unapoona dhahiri kuwa alikuwa anaendesha gari kwa mwendo kasi bila kujali watu wengine nao wanatakiwa watumie barabara hiyo.