jamani nyie wanaume

jamani nyie wanaume

Da! pole dada yangu kwani kidonda cha mapenzi huwa kinauma sana kuliko kidonda cha moto, nachoweza kukushauri ni kujitambua kuwa utu wako unathamani kiliko huyo mwanaume, kama amesema hakutaki basi usipoteze mda sana kwake wewe fanya hivi, achana nae endelea na shughuli zako ipo siku mungu atakuajalia kazi ya kipato kikubwa kulingana na elimu yako, pia tambua kuwa kunawanaume na kuna magumegume huyo hana msimamo, mimi nimekaa na mchumba kwa miaka mitano sasa na kila mtu anaishi kwake nilipenda kufunga ndoa mapema ila shule ndio inachelewesha mchakato, Mungu akipenda mwakani namaliza kila kitu chuo na ndoa, mahusiano hudumishwa na uaminifu ambao ni tunda la upendo, huyo bwana hajakupenda, ataendelea kukuumiza sana kama mtazidi kuwa wote. Imenigusa sana kwani najua nini maana ya kupenda. kwani unawatoto wangapi uluozaa nae?
 
^^
Hivi jamani leo nimepata utata,,hii post ya pili sasa,,UBOYFRIEND unaisha lini?
Miaka 3 unaishi nae bado unamwita boyfriend?
If that the case,,inaweza kuwa sababu ya yeye kutofunga ndoa na wewe!
3yrs tunaishi wote,,bado uniite boyfriend? Maanake akija mwingine akatangaza ndoa basi huyo ni mume?
^^
Nijuavyo mimi ukiishi na mwanaume miezi mitatu tayari ni mume.sasa miaka mitatu!akiondoka asiondoke na nguo tuu wagawane walivyochuma kwa muda wote huo.alaa!
 
Unalia kwani kaondoka na sura ama umbo lako??!!!! EBOOOOOOOOO!!!!!!!!!!!!!!!!! Amka oga tupia pamba yako ingia kitaa tafuta mahali kaa alone kula kunywa, huku ukipanga strategies!!!!!!!!!! yaani ungekuwa mdogo wangu ningekuwasha kibao utie akili....................DONT YOU HAVE PPLE IN UR RESERVE LIST?? ITS TIME TO CALL ONE ON BOARD and start to have fun. Huku ukipanga baada ya kupamba nini kifwate.............its so simple to deal na hawa wanaume wanyanyasaji kama unaakili kama yangu.
Nsee a muro, sikupatii picha. usimpotoshe kwa kumshauri kuwa na mwanaume mwingine kwa kukomoa. Anahitaji kutulia na kuamua. Kukukimbilia urafiki na mwanaume mwingine hakusaidii, anaweza kuingia kwa mwanaume mwingine exactly kama huyu aliye naye. Unafikiri ikitokea hivyo kitafuata nini... to commit suicide.
 
Pole Sana Mdada

Ila usilie tena, futa machozi na njoo kwangu mi niko tayari kwenda kwenu. ni PM tujuane nikufute machozi na kukupa raha

Wako kipenzi
 
Wewe endelea kukaa naye tu ukishusha mashine tu hapo ndio utakwa umefika Kigoma mwisho wa reli, yaani kwishney!
 
Piga moyo konde songa mbele sali sana mkumbuke Mungu kipindi hiki ambacho myo wako ndio unautawala ubongo wango.......yapo zaidi ya hayo so ona na chukulia ni mambo ambayo yanampata mwanadamu kama wewe na tena makubwa sana
 
Pole ila jamaa kama hakutaki vile coz keshakupa tru, achana nae haina jinsi
 
kwa mujibu wa sheria mkiishi pamoja kwa muda wa miezi 3 nyie ni mume na mke,ila ndoa hailazimishi ukilazimisha utateseka.na sio wanaume ndio tulivyo co wote ila usilazimishe tulia utapata atakae kuja kujitambulisha.

Duuuuh hii nayo mpya! kwa mujibu wa sheria gani iyo? una uhakika na unachokisema? au ni Hear-say tu?
 
Habari wana MMU,mimi ni msichana mwenye kazi yangu ya kuniingizia kipato kidogo, na elimu ya kawaida.Kikubwa ambacho kinaniuma sana mpaka naandika huku nalia,Nina BF wangu ambaye aliamishwa kikazi mkoa mwingine na baaadae akanitafutia kazi huko aliko na kuanza kuishi nae(kwa kweli sikuwa napenda kuishi nae bila ndoa).Miaka mitatu sasa imepita,ila jamaa sijawahi kumsikia hata siku moja kudokezea jambo la kwenda kujitambulisha kwetu.Chakushangaza sasa nikimwambia kuhusu swala la kwenda kwetu daaaah!anachonijibu sidhani kama ntakuja kukuoa wewe na ukae ukijua kwamba ukiamua ondoka au ubaki nikufuje tu,ila swala la mimi kwenda kwenu sahau.

nashindwa kuendele jamani,

Kusema ukweli, me bado sijaelewa unataka ushauri wa aina gani, na nini usichokielewa apo! Huelewi picha, huelewi maandishi AU huelewi vyote?
 
Kisheria wewe ni mke wake kidini sijui cha muhimu jua anakupenda kama huamini andoka usimwambie unaenda wapi na wala usimtafuke afu utakuja nielewa
 
Dah! Mbona kakupa makavu ivo spati picha umeumiaje polee..

Ndo shida ya "njoo tu ishi" amekukinai uyo atakua ameona mpungufu ambayo hatawezana nayo..

Lakin ajue hakuna aliyekamilika..tupa kule songa mbele
 
Nsee a muro, sikupatii picha. usimpotoshe kwa kumshauri kuwa na mwanaume mwingine kwa kukomoa. Anahitaji kutulia na kuamua. Kukukimbilia urafiki na mwanaume mwingine hakusaidii, anaweza kuingia kwa mwanaume mwingine exactly kama huyu aliye naye. Unafikiri ikitokea hivyo kitafuata nini... to commit suicide.
GHEEEEEEEEEEEEEEEEE!!
AM SUPER SMARTER NEVER SEEN AISEE!!!!!!!!!!!!!!!!!!1

Always nikijipanga lazima ni win, no matter how long will statergy take and how much it wwill cost me dude!!! am never a failure especially kwenye social life!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! The secret is out smart your enemy !!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Usiseme etii nitajaribu hiyo ni big noooooooooooooo hapa unasema I will outsmart him............

yaani ipo siku nitawapeni a short histry of my life the true one kisha utajua mjini kukoje................nilifeli darasa lkn sio maisha besttt!!!!!!!!!!
 
una bahati kwamba yeye yuko wazi na kisha weka wazi msimamo wake.usipoteze mda wako.tafakari na chukua hatua.maisha ni zaidi ya yeye kuwa na wew.he is a serious mistake u have done in yo life.consider its done.tazama mbele pengne huko ndio kuna chaguo lako sahii.pole.
 
Maskini weee! Inauma sana jamani, hapo ukute ulishajishaua unamume dah! ondoka tuu mamy tena kama mtoro wala usihangaike kumuaga,
 
We unampenda huyo bwana ako huna lolote,sasa ufanyaje wakati kashakwambia hana mpango wa kukuoa??,sasa unatak ushauri gani apa??...
 
ulifuata kazi au mvulana umewekwa wazi unataka nn chukua uamuzi mgumu hata kama itauma itapoa tu ila jiweke sawa kwanza
 
^^ Hivi jamani leo nimepata utata,,hii post ya pili sasa,,UBOYFRIEND unaisha lini? Miaka 3 unaishi nae bado unamwita boyfriend? If that the case,,inaweza kuwa sababu ya yeye kutofunga ndoa na wewe! 3yrs tunaishi wote,,bado uniite boyfriend? Maanake akija mwingine akatangaza ndoa basi huyo ni mume? ^^
Huyu anatakiwa kuomba division of matrimonial properties mahakamani coz yuko under presumption of marriage
 
ulifuata kazi au mvulana umewekwa wazi unataka nn chukua uamuzi mgumu hata kama itauma itapoa tu ila jiweke sawa kwanza
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom